Yeremia 1: Mwongozo wa Maombi

October 28, 2020 in Mwongozo wa Maombi by TGVS

Mwongozo wa Maombi Unaoshabihiana na “Mpango wa Usomaji Biblia” wa leo: Yeremia 1/ Dhima: Uhakikisho wa Mungu kwa Yeremia/24-BSG-1B, (Yeremia 1:17-19)/ Wimbo: “Anywhere with Jesus I can Safely Go!” [Mwandishi: Jessie Brown Pounds (1887)]


 

Yeremia 1:17–19 — 17 “Haya basi, wewe jifunge viuno, ukaondoke ukawaambie maneno yote niliyokuamuru; usifadhaike kwa ajili yao, nisije nikakufadhaisha wewe mbele yao. 18 Maana, tazama, nimekufanya leo kuwa mji wenye boma, na nguzo ya chuma, na kuta za shaba, juu ya nchi yote; juu ya wafalme wa Yuda, na juu ya wakuu wake, na juu ya makuhani wake, na juu ya watu wa nchi hii. 19 Nao watapigana nawe; lakini hawatakushinda; maana Mimi nipo pamoja nawe, asema Bwana, ili nikuokoe.”

Maelezo ya Ufunguzi: Wapendwa, tunapokuja katika Kipindi cha Maombi leo, tunaalikwa— kutafakari juu ya maisha ya nabii Yeremia. Kwanza, aliitwa na Mungu. Halikadhalika, kila mmmoja wetu ameitwa na kutakasa na Mungu na kupewa wajibu maalum: Utume Mkuu (Mat 28:19-20). Pili, Yeremia alidharauliwa, alichukiwa, aliteswa (alifungwa gerezani), na kukataliwa na watu; lakini Mungu alikuwa ameahidi kuwa pamoja naye hata katikati ya masahibu (Yer. 1: 7-8, 17-19).

Wapendwa, katika siku za mwisho, kila mmoja wetu ameitwa kuutahadharisha ulimwengu kuhusu hukumu ijayo (Ufu. 14:6-12; 16; 18-19). Lazima tusimame mbele ya mataifa kama mashuhuda wa Yehova Mungu. Lazima tusimame kwa ajili ya Kweli na Haki. Katika nyakati hizi za uasi tashabiha (usiokifani), lazima tudhihirishe kielelezo cha Maisha na Tabia ya kumwabudu Mungu pekee wa kweli! Lazima tuzungumze waziwazi dhidi ya dhambi na hitaji la jamii yote ya wanadamu kutubu, kudumisha Amri za Mungu na kujiandaa kwa ajili ya Marejeo ya Pili! Haitakuwa kazi rahisi. Jukumu hili litakabiliwa upinzani toka kila mahali, lakini hatupaswi kuyumba, hatupaswi kuogopa, kwa sababu tunamtumikia Mungu aliye hai. Sikiza ahadi hii — “Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito, haitakugharikisha; uendapo katika moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza.” (Isaya 43:2). Yule aliyetuita atatuongoza, atatulinda, na kutukimu! Kazi yetu ni kumtumaini, Naye atatenda yaliyosalia. “Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba Yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu.” (Wafilipi 1:6) Je unao ujasiri wa kutosha kuziamini ahadi hizi?

Maadili ya Kukuza: Utii, Ujasiri, Imani, Kumtumaini BWANA.

Dhambi za Kuepuka/Kuungama: Hofu, kusita, udhuru wa kutoifanya kazi ya Mungu; mashaka dhidi ya Mungu; kumwacha Mungu; ibada ya sanamu; kutozingatia amri ya Mungu ya ‘Kwenda’ (Yer. 1:17).

Zingatia Udhuru Saba ambao kwa kawaida huwasilishwa kwa kupuuza wajibu:

  • Kukosa umahiri binafsi [Musa, 3:11; 4:1, 10];
  • Udhuru wa dhambi [Rum. 2:1; Yn. 15:22; Rum. 1:20];
  • Shinikizo la masumbufu ya maisha haya [Luka 14:16-20];
  • Ugumu wa watawala, wasimamizi, waajiri [Mat 25:24-25];
  • Dai la kutoona, kutotambua, au kutogundua mahitaji [Mat 25:44-45];
  • Uvivu/matatizo ya kutojishughulisha [Mit. 22:13];
  • Udhaifu binafsi [Yeremia, 1:6];
  • Kukosa wadhifa wa kijamii [Gideoni, Waamuzi 6:15].

Jambo la Kumshukuru Mungu Kwalo: [1] Mungu ni Hakimu mwaminifu; Yeye ni BWANA; anajua yote; maarifa ya Mungu juu ya binadamu (Zab. 139); mustakabaini wa Mungu (Yer. 1:4-5). [2] Ulinzi dhidi ya hatari tajisimu (halisi), maadui.

Watu wa Kuombewa: Wale watendao kazi katika shamba la Bwana la mizabibu —(Wachungaji, Wamishenari, Wahubiri, Wainjilisti, nk.)—wamtumaini Bwana na kuifanya kazi Yake bila hofu.

Masuala ya Kuombea: Utakaso; kuwezeshwa kiroho kuifanya kazi ya Mungu; ujasiri wa kuifanya kazi ya Mungu katikati ya upinzani; kuitikia wito wa Mungu: utii kwa Neno Lake, Amri na Sheria Zake; utayari wa kuishi au kufanya kadiri ya mapenzi Yake; kuenenda katika njia Zake.

Ahadi ya Leo: “Lakini sasa, Bwana aliyekuhuluku, Ee Yakobo, Yeye aliyekuumba, Ee Israeli, asema hivi, Usiogope, maana nimekukomboa; nimekuita kwa jina lako, wewe u Wangu. Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito, haitakugharikisha; uendapo katika moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza.” (Isaya 43:1–2)

Hatua ya Maamuzi: Tumia wasaa fulani kuombea dhambi zilizobainishwa/na mambo yaliyoorodheshwa hapo juu. Endapo una Mahitaji ya Kuombea, tafadhali yaandike hapa chini, na mtu fulani atayaombea. Mungu akubarikini!


 

Sala: Baba, tunakushukuru kwa neno Lake katika Yeremia 1. Tunakushukuru kwa mpango bora ulionao kwa ajili ya kila mmoja wetu. Kwa ajili ya maarifa Yako: ulitujua kale na kale, kabla hatujazaliwa, hata kabla ya kuwekwa msingi wa ulimwengu huu. Tunakushukuru kwa kutuumba, kutuokoa, na kutuita kwa “wito mtakatifu, siyo kwa sababu ya matendo yetu, bali kadiri ya kusudi na neema Yako, tuliyopewa katika Kristo Yesu, kabla ya kuanza wakati” (2 Tim 1:9).

Mara nyingi tuko kama Yeremia. Tunakuja na udhuru wa kutoifanya kazi Yako. Tatizo letu ni dhambi na kutoamini. Dhambi hutunyima ujasiri tunaopaswa kuwa nao ili kukaribia enzi Yako ya Neema (Ebr. 4:16). Hivyo, tusaidie kutenda kama Wakristo: kuichukia Dhambi na kupenda Haki. Tusimame tukiwa jasiri na imara, tukidai ahadi Zako, na kuifanya kwa uaminifu kazi ambayo umetupatia. Tusaidie tujifunge viuno katika kujitayarisha! Tuamke na kuuambia ulimwengu yale ambayo umetuamuru (Yer. 1:17).

Kadiri tunapoanza Kitabu hiki, hebu tumwone Kristo katika kila sura inayowasilishwa. Hebu tudumishe umakini wa kina kwenye Maelekezo ya Kiungu yanayobainishwa hapa. Hebu Roho Wako atufundishe masomo maridhawa yaliyomo katika kurasa ya Kitabu hiki. Tusamehe kutoamini kwetu, mashaka, hofu, kusita, udhuru wa kutoifanya kazi Yako. Tukumbushe kila mmoja wetu kwamba– “Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache” (Mat 9:37); na kwamba “sasa ni wakati mwafaka wa kuamka usingizini; maana sasa wokovu wetu u karibu nasi zaidi kuliko tulipoanza kuamini.” (Rum. 13:11). Tunakushukuru Baba, nasi tunaomba haya, tukiamini na kutumaini katika jina la Yesu Kristo, Amina.


 

Ibada katika Wimbo: Katika Mwitikio wetu katika somo la leo, nikualike tutafakari maneno ya Wimbo # 133 – “Po pote na Yesu naweza kwenda!”

PO POTE NA YESU, NAWEZA KWENDA.
“Anywhere with Jesus I can Safely Go!”

Po pote na Yesu nina furaha, anitumako Yesu ndiyo raha; Asipokuwako hapanifai, akiwapo Yesu mimi sitishwi.

[Chorus]: Po pote, po pote, sina mashaka; Po pote na Yesu, naweza kwenda.

Akiwapo Yesu si peke yangu, na nijapotupwa akali wangu; Ajaponiongoza njia mbaya, niwapo na Yesu ninashukuru.

Akiwapo Yesu naweza lala, naweza pumzika hata kiyama; Kisha nitakwenda kwake milele, akiwapo Yesu furaha tele.

 

Comments
Print Friendly, PDF & Email