Yeremia 2: Mwongozo wa Ibada

October 28, 2020 in Mwongozo wa Ibada by TGVS

Mwongozo wa Ibada Unaoshabihiana na “Mpango wa Usomaji Biblia” wa leo: Yeremia 2/ Dhima: Karipio la Mungu kwa Hali ya Yuda Kukosa Imani /24-BSG-2A, (Yeremia 2:1-37)/ Wimbo: We’ll tarry by the living waters! [Mwandishi: Franklin E. Belden]


 

UCHUNGUZI: Chemchemi ya Maji ya Uhai (Yer. 17:13; 18:14; Zab. 36:9; Isa. 55:1-2; Yn. 4:14; 7:37-39; Ufu. 21:6; 22:1, 17).

TAFAKARI: “Kwa maana watu Wangu hawa wametenda maovu mawili; wameniacha Mimi, niliye chemchemi ya maji ya uzima, wamejichimbia mabirika, mabirika yavujayo, yasiyoweza kuweka maji.” (Yeremia 2:13) “Sura hii imebeba karipio kali la Mungu dhidi ya watu Wake kwa kukosa imani kwa karne nyingi. Baada ya kuwakumbusha juu ya uaminifu Wake, aliwaalika wawasilishe shutuma zozote za makosa kwa upande Wake ambazo zingehalalisha hali yao ya kukosa utii na shukrani.”

MAANA YA KIIBADA: “Israeli ilikuwa imetenda dhambi mbili. Watu walikuwa wameacha “utukufu” wao (v. 11), Bwana aliyekuwa amewaleta nchi ya ahadi na sasa walikuwa wamekumbatia sanamu batili. Yeremia alilinganisha uamuzi huo na kubadilisha chemchemi ya maji yatiririkayo na visima vilivyopasuka visivyoweza kutunza maji. Wasikilizaji wa Yeremia wangeelewa ulinganifu huo, maana ilikuwa muhimu kusiliba visima vya mawe-chokaa penyevu ya Palestina kwa plasta ili viweze kutunza maji. Yuda alikuwa akifanya dhambi ileile iliyokuwa imewaletea uangamivu wa awali Ufalme wa Kaskazini kwa sababu ya desturi zake za ibada ya sanamu (cf. Eze 16:44–52; 23:1–48). Hivi yeyote leo angekuwa mpumbavu kiasi cha kuchuuza kisima cha chemchemi kwa kisima bovu? Kinachosikitisha, wengi hufanya hivyo. Baadhi ya “visima vilivyoharibika” leo ni kufukuzia utajiri, utawala, umaarufu, au anasa.” [F. B. Huey, Jeremiah, Lamentations, The New American Commentary, (Nashville: Broadman & Holman Publishers, 1993), 16:60, 64].

 SAUTI YA INJILI: Sehemu hiyo imeandikwa kana kwamba Mungu anazungumza nawe moja kwa moja — kwa sababu Yeye anafanya hivyo. Bwana ananiambia nini asubuhi ya leo? Mwanangu, Mimi ni Chanzo cha yote yenye kurutubisha, kunawirisha, na kufurahisha nafsi—Mimi ni “Chemchemi ya maji ya uzima.” Ridhaa halisi ya maisha inaweza tu kupatikana katiak Mwana, Yesu Kristo (1 Yohana 5:11–12). Utii kwa Neno Langu huleta matokeo ya kubarikiwa, kuridhika, na uzima wa milele. Kutengwa Nami ni kuangamia milele (Yohana 3:16). Je utatubu dhambi zako, na kuja Kwangu ili ubarikiwe?

Shauku Yangu: Kwa neema ya Mungu, nataka kukataa maisha yadanganyayo na yasiyoridhisha ambayo Shetani anaahidi, na kuelekeza fikra zangu kwa Kristo, Chemchemi ya Maji ya Uzima.


 

Uwe na Siku Yenye Baraka: “Walakini yeyote atakayekunywa maji yale nitakayompa Mimi, hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele.” (Yohana 4:14)

Comments
Print Friendly, PDF & Email