Yeremia 2: Mwongozo wa Maombi

November 13, 2020 in Mwongozo wa Maombi by TGVS

Mwongozo wa Maombi Unaoshabihiana na “Mpango wa Usomaji Biblia” wa leo: Yeremia 2/ Dhima:Lakini uovu wako umeandikwa mbele Yangu.” /24-BSG-2B, (Yeremia 2:21-22)/ Wimbo: Come unto me, all ye who are weary! [Mwandishi: J. Spencer Tilton]


 

Andiko Msingi: “Nami nalikuwa nimekupanda, mzabibu mwema sana, mbegu nzuri kabisa; umegeukaje, basi, kuwa mche usiofaa wa mzabibu-mwitu machoni Pangu? Maana ujapojiosha kwa magadi, na kujipatia sabuni nyingi, lakini uovu wako umeandikwa mbele Yangu, asema Bwana MUNGU.” (Yeremia 2:21–22)

Maelezo ya Ufunguzi: Andiko hili husisitiza vina vya dhambi ya Israeli: walikuwa wamechafuliwa na hatia kiasi kwamba hakuna kiwango cha sabuni wala magadi inayoweza kuwanadhifisha. Kumbuka, “Israeli walikuwa utakatifu kwa Bwana; malimbuko ya uzao Wake.” (Aya ya 3). Mungu aliichagua Israeli na kuitenga, akiwa amesahimishwa (takaswa) kwa ajili ya makusudi yake matakatifu (Kut. 19:5-6; Kumb. 7:6; 14:2; 26:19). Lakini hapa tunaona ushupavu wa kuondoa kutoka katika wajibu huu mtakatifu. Badala ya kuendelea kuwa mwaminifu kwa Yehova, waliasi, wakamwacha, na kuienendea miungu mingine.

Wapendwa, tunapokuja katika Kipindi cha Maombi leo, tunaalikwa—kutubu dhambi zetu. Toba halisi ni kubadili nia, moyo na mtindo wa maisha. Ni kuepuka matendo maovu (Gal. 5:19-22) na kushikilia mienendo bora ya Kikristo (Filp. 4:8). Toba unahusiana na imani katika Bwana Yesu Kristo. Mfano wa mwanampotevu hutufundisha sisi kwamba kama “tukirudi” kwa Mungu, atatupokea!

Maadili ya Kukuza: Maungamo, Toba, Utii kwa Mungu.

Dhambi za Kuepuka/Kuungama: Hebu tuzingatie kifupi maelezo ya dhambi ya Israeli katika sura hii — Ibada ya sanamu: waliabudu sanamu batili na kuinajisi nchi (Yer. 2:4–11, 20, 23–30); Kumwacha Mungu: badala ya kuchagua chemchemi ya maji hai, wao walijichimbia visima vibovu visivyohifadhi maji (Yer. 2:12–13); ushirika mwovu: Misri na Ashuru; walichukuliwa uhamishoni kama matokeo ya hilo (Yer. 2:18–19, 36–37).

Dhambi zingine – [1] Kushindwa au kukataa kuelewa, manufaa ya nidhamu kutoka kwa Mungu, marudi, mafundisho [2] Kutelekeza upendo wa Mungu na utii Kwake, ugeugeu juu Yake; [3] Ibada ya sanamu, ukahaba wa kiroho; [4] Kuwatesa maskini; [5] Kiburi cha kiroho: kujidhania kutokuwa na dhambi (Yer. 2:33-34); [6] Kuwatumainia watu badala ya Mungu.

Jambo la Kumshukuru Mungu Kwalo: upendo & rehema ya Mungu. Israeli alikuwa biarusi wa Mungu kupitia agano lililofanyika pale Sinai, lakini walikuwa wamesahau wajibu wa uhusiano wa agano lao. Walimwacha Mungu na kumwasi. Katika sura hii, Mungu anawaendea—kwa kuonesha Dhambi Mahususi. Pengine huu unaweza kuwa wito wa uamsho kwa ajili yetu sote (cf. Isa. 1:18-20)

Watu wa Kuombewa: Wale wanaoficha dhambi zao. Mungu anatukumbusha tu kwamba udhalimu wetu “umeandikwa” mbele Yake. “Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.” (Mithali 28:13)

Masuala ya Kuombea: Kukosa shukrani kwa Mungu; Uovu; Kujiamini (bandia); Kurudi nyuma; Ugumu wa moyo; Kujihusianisha na uovu; Ibada ya sanamu; Msamaha wa Mungu – kuondolewa kwa dhati/hatia yetu.

Ahadi ya Leo: “Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.” (1 Yohana 1:9–10)

Pamoja katika Maombi: Kwa makini tafuta maudhui ya maombi yako katika Yeremia 2. Hebu zingatia vipengele vifuatavyo vya maombi — Sifa: Msifu Mungu jinsi alivyo na afananavyo. Maungamo: Kiri na Geuka [tubu] kutoka kwenye hali yako ya dhambi (angalia ‘Dhambi za Kuepuka/Kuungama’ hapo juu). Shukrani: Mshukuru Mungu kwa ajili ya tabia Yake, Matendo Yake, na baraka Zake za kila siku. Dua: Mwombe Mungu akidhi mahitaji yako kimwili na kiroho. Usahimifu: Jiadhimishe katika kutii mapenzi ya Mungu. Maombezi: Mwombe Mungu akidhi mahitaji ya wengine.

Hatua ya Maamuzi: Fuata utaratibu huu rahisi “Kuomba kwa Maandiko,” halafu wasilisha maombi yako mbele za Mungu. Fungua Biblia yako sasa katika Yeremia 2: kadiri usomavyo, tulia katika kila andiko na kuligeuza kuwa sala! Kama unavyo Mahitaji ya Maombi, tafadhali yaandike hapa chini na mtu fulani atayaombea.


 

Sala: Baba, tunakushukuru kwa neno Lako katika Yeremia 2. Tunakushukuru kwa neno Lako ambalo “li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.” (Waebrania 4:12)

Tunakiri dhambi zetu – kukosa kwetu shukrani, kutoamini, kiburi, lakini juu ya yote, uasi. Ee Bwana, Wewe wajua dhambi zetu: maana japo tujaribu kuzisafisha kwa “magadi, na kujipatia sabuni nyingi, lakini uovu wako umeandikwa mbele Yako” (Yer. 2:22). Zitwae basi, dhambi zetu zote, BWANA, “Unioshe kabisa na uovu wangu, Unitakase dhambi zangu. Maana nimejua mimi makosa yangu Na dhambi yangu i mbele yangu daima.” (Zaburi 51:2–3, ESV)

Tunakushukuru kwa tabia Yako isiyobadilika—upendo, rehema, fadhili kwetu, wadhambi. Tunakushukuru kwa ajili ya matendo Yako ya uumbaji na ukombozi. Tunakushukuru kwa ajili ya karama za kiungu, na baraka za kila siku utukirimiazo.

Baba, tunaomba kwa ajili ya mahitaji ya wengine katika wasaa huu: wagonjwa miongoni mwetu (watu wengi wapoteza maisha katika kipindi cha mtanduko huu wa Kovidi-19; wengi ni wagonjwa; wengi wanakufa; wengi wamepoteza matumaini). Turehemu Ee BWANA! Wengi wamekuaisi na hawana habari kwamba mlango wa rehema unafunga hivi karibuni, na kwamba Kristo anakuja, na hata yu mlango! Turehemu Ee BWANA.

Tufundishe kutii mapenzi Yako, amri Zako, Sheria Yako. Tufundishe kuamini na kusisima katika ahadi za Mungu zisizoweza kushindwa! Tusamehe BWANA. Tutakase na kututia muhuri kwa ajili ya Ufalme Wako. Tunakushukuru Bwana, nasi tunaomba mambo haya, tukiamini na kutumaini katika jina la Yesu Kristo, Amina.

Comments
Print Friendly, PDF & Email