Yeremia 20: Maswali & Majibu.

November 15, 2020 in Mwongozo wa Biblia by TGVS

Mwongozo wa Kujifunza Biblia/ Yeremia 20, (24-BSG-20J)/ Maswali na Majibu.


 

[1] Nini unachojua kuhusu Pashuri, mwana wa Imeri?— (1-2) Alikuwa kuhani, ambaye pia alikuwa afisa mkuu katika nyumba ya BWANA.

[2] Nini ambacho Pashuri alimfanyia Yeremia? (2) Alimtwaa Yeremia na kushurutisha apigwe, au kuchapwa viboko 40 (cf. Kumb. 25:2–3). “akamtia katika mkatale uliokuwa pale penye lango la juu la Benyamini, lililokuwa katika nyumba ya Bwana.”

[3] Mikatale ni nini? — “kifaa cha kutesea chenye matundu matano, ambapo shingo, mikono miwili, na miguu miwili huingizwa, kiwiliwili kikikunjwa katika mkao wa kubinuka (Yer. 29:26). Kutokana na neno la Kiebrania “geuka,” au “umiza.” Hii huashiria ukatili wa Pashuri.” [Commentary Critical and Explanatory on the Whole Bible, 1:526].

ZINGATIA: Pashuri “alidumisha utaratibu ndani ya viunga vitakatifu. Kitabaini, Pashuri anachagua kudumisha utaratibu kwa kumtesa nabii wa Bwana badala ya kushughulika na desturi zilizoinajisi hekalu (zilizobainishwa na Yeremia katika sura ya 7). Upinzani waliopitia manabii wote wa AK huashiria upinzani aliokabili Yesu kama nabii mkuu (Luka 11:49–51).” –[NIV Biblical Theology Study Bible/ Jer. 20:1]

[4] Kwa nini nabii amwadhibu mtu fulani? (1–2) Makuhani walikuwa katika kiini cha upinzani dhidi ya Yeremia (Yer. 11:21) sababu mojawapo ni kwamba walikuwa walengwa wa ukosoaji wake mkali zaidi (Yer. 1:18). Walikuwa sehemu ya mifumo ya mamlaka kuu katika Yerusalemu ambayo Yeremia alitangaza kwamba yalikuwa yanaelekea mwisho wake (Yer. 18:18).

[5] Nini kilichotokea siku inayofuata? (3) “Nabii huyu aliachiliwa huru kutoka katika mateso ya mkatale baada ya usiku mmoja, lakini hili halimaanishi kwamba aliachiliwa kifungoni wakati huu. Ni dhahiri kwamba Yeremia alitumia muda mwingi sana gerezani wakati akiandika jumbe zake kwa ajili ya Mfalme Yehoyakimu” (angalia PK 433; angalia Yer. 36:5).—(SDA BC 4:431).

[6] Je maneno “Magor-misabibu” humaanisha nini? (3) Kimsingi, “utisho kila upande.” “Maneno yayohayo hufasiriwa kama “hofu kila upande” (Zab. 31:13; Yer. 6:25; 20:10). Inawezekana kwamba nabii huyu alipata faraja katika Zab. 31, na kwamba, kwa sababu ya tumaini lake katika Mungu kama Mkombozi wake, alitumia maneno “hofu kila upande” kwa ajili ya mtesi wake, badala yake mwenyewe kama alivyofanya mtunga-Zaburi (angalia Zab. 31:9–16).” —(SDA BC 4:431).

[7] Yeremia alipoachiliwa huru kutoka kwenye minyororo yake siku iliyofuata, alikataa kubadili jumbe zake za onyo. Kwa kweli, alishadidia zaidi kuhusu ukubwa wa hukumu inayokaribia sana juu ya taifa na watesi wake. Nini ambacho Yeremia alitabiri kuhusu Pashuri? (3-6)

Kwa kumteulia jina jipya Pashuri – “Magor-Misabibu,” alikuwa akisisitiza kwamba Pashuri, familia yake na marafiki zake wangezungukwa na utisho. Alitangaza kwamba adui (Wababeli) wangewateka na kuwachukua utumwani; pia, alitangaza kwamba Mungu angemruhusu adui ajitwalie utajiri wote wa taifa hilo: Tena mali zote za mji huu, na mapato yake yote, na vitu vyake vya thamani vyote pia, naam, hazina zote za wafalme wa Yuda!” (v. 5).

[8] Kwa nini Yeremia alimshutumu Mungu juu ya udanganyifu? (7) Mwanzoni, alidhani kwamba Mungu alikuwa amemwacha. “Pengine malalamiko yalikuwa mwitiko wa usiku wa msongo wa nabii akiwa katika mikatale (angalia vs. 2, 3). Katika hali yake ya fadhaa, Jeremia alionekana kuchukulia kwamba kazi yake imeshindikana, kushindwa kulikozidishwa uchungu zaidi kwa hofu iliyomlemea kwamba Mungu asingetimiza ahadi Zake (angalia Yer. 1:8–10; cf. Yer. 15:10, 17; Yona 4:1–4).” — (SDA BC 4:431).

[9] Nini kilitokea pale Yeremia aliposema asingemtaja BWANA au asingenena tena katika jina Lake? (9) Moyo wake ulipatwa na maumivu ya kuungua moto, ukiwa umefungiwa mifupani mwake.

ZINGATIA: ”Endapo malengo kweli hutoka kwa Bwana, utapata hisia za kina ndani yako kwamba lazima uyatimize ili kumtii Bwana na kuwaletea wengine manufaa. Hutaweza kufanya vinginevyo.” (NKJV Charles F. Stanley Life Principles Bible Notes/ Life Lessons: Jer. 20:9)

[10] Marafiki wa Yeremia – marafiki zake wa karibu na aliowategemea – wakaanza kunong’onezana, “hofu ziko pande zote.” Kwa nini walikuwa wakinong’onezana hivyo na kutamka maneno hayo ya kashfa? (10)

“Hili lilikuwa jina ambalo Yeremia alikuwa amempatia Pashuri (v. 3). Pengine baadhi waliokuwa wamemsikia Yeremia akilitumia sasa walikuwa wakimwiga kwa kulitumia kama majazi (jina la utani) ya Yeremia. Ujumbe wa nabii kuhusu hukumu haukupendwa kabisa kiasi kwamba umati walitamani kumsakama. Mtazamo mwingine ni kwamba Yeremia alielezea mnong’ono huo kama utisho aliosika mahali popote alipoenda (kila sehemu).” –[NIV Quest Study Bible/ Jer. 20:20].

Comments
Print Friendly, PDF & Email