Yeremia 3: Maswali na Majibu.

November 16, 2020 in Mwongozo wa Biblia by TGVS

Mwongozo wa Kujifunza Biblia/ Yeremia 3, (24-BSG-3J)/ Maswali na Majibu.


 

[1] Ni wapi huoneshwa kwamba udhalimu wa Israeli ulikuwa na simile kuliko ule wa Yuda? “Bwana, akaniambia, Israeli mwenye kuasi amejionesha kuwa mwenye haki kuliko Yuda mwenye hiana.” (Yer. 3:11)

[2] Jinsi gani Israeli ilikuwa na haki zaidi kuliko Yuda? (3:11) “Wakati ule ufalme wa kaskazini wa Israeli ulipomwacha Bwana, takriban karne moja kabla ya wakati wa Yeremia, ulikuwa umepuuza maonyo ya nabii. Ufalme wa kusini wa Yuda, hata hivyo, ulikuwa umepuuza siyo tu manabii bali hata mfano wa kile kilichokuwa kimeipata Israeli. Watu wa Yuda walikuwa wameshuhudia uangamivu wa Israeli na watu wake wakichukuliwa utumwani na Ashuru, lakini walishupaa katika dhambi yao, hali iliyowafanya wawe na haki pungufu kuliko Israeli isiyo na imani.” (NIV Quest Study Bible).

  • ZINGATIA – “Unafiki ulikuwa chukizo kwa Mungu kama uasi wa wazi (PP 523). Ukweli kwamba Yuda ilikuwa na fadhila nyingi zaidi ulikuza hatia yake. Miongoni mwa fanaka za Yuda zilikuwa zifuatazo: (1) Mfuatano endelevu wa wafalme kutoka katika nyumba ya Daudi. Wakati miaka yake yote ya uwepo kama ufalme, nasaba moja tu ilitawala. Matokeo yake, aliepushwa misukosuko ya kisiasa iliyomkumba jirani yake wa kaskazini. (2) Uwepo ndani ya mipaka yake wa Hekalu na udhihirisho wazi wa uwepo wa Mungu kwenye Hekalu. (3) Uwepo ndani ya mipaka yake wa idadi kubwa ya makuhani na Walawi, wawakilishi rasmi wa ibada ya Mungu. (4) Mfano wa onyo kutokana na anguko la Israeli kwa miaka mia.
  • Kwa kuzingatia fadhila zote hizi, Yuda akawa mwenye hali isiyovumilika ya kukosa imani, mnafiki, na mwenye kiburi. Hivyo, Israeli, licha ya uasi wake wazi, alikuwa na hatia kidogo kuliko Yuda (angalia Eze. 16:51, 52; 23:11; Mat. 12:41, 42; Luka 18:14). “Kadiri maarifa ya mapenzi ya Mungu yawavyo makubwa zaidi, ndivyo ziwavyo kubwa zaidi dhambi za wale wanaoyapuuza” (PP 584).” [The Seventh-Day Adventist Bible Commentary, 4:366].

[3] Mungu alimtuma Yeremia ‘kuelekea kaskazini,” mahali walikotwaliwa utumwani yale Makabila Kumi. NI ujumbe gani wa Upendo aliopewa kuwasilisha?Rudi, Ee Israeli usiye na imani, asema Bwana; sitafanya uso Wangu ukuangukie wala kukutazama kwa hasira, maana Mimi ni mwenye rehema, asema Bwana; sitadumisha hasira Yangu hata milele.” (Yeremia 3:12b, AMP)

[4] Ni kwa ahadi na unabii gani wa rehema ambapo Israeli wanaitwa katika toba?— (3:12–19) “Rudini enyi watoto wapogofu, ndipo nitaponya upogofu wenu.”

[5] Licha ya upogofu wao (kurudi nyuma), nini ambacho Mungu angewapatia Israeli? (3:15) Viongozi wa kiroho (wachungaji) “wanipendezao moyo Wangu, watakaowalisha kwa maarifa na fahamu.”

[6] Jinsi gani Israeli ilikuwa imemtendea Mungu? (3:20) Kama mwanamke mwenye hiana (asiye mwaminifu) amwachavyo mumewe.

[7] Nini jibu la watu kwa ahadi hii?— Yeremia 3:22–2522 “Rudini, enyi watoto waasi, Mimi nitaponya maasi yenu. Tazama, tumekuja Kwako; maana Wewe u Bwana, Mungu wetu. 23 Ni kweli, msaada haufai unaotazamiwa kutoka milimani, makutano yenye mshindo juu ya milima; ni kweli, wokovu wa Israeli ni katika Bwana, Mungu wetu. 24 Lakini kitu cha aibu kimeila kazi ya baba zetu tokea ujana wetu; makundi yao ya kondoo na ng’ombe, wana wao na binti zao. 25 Na tulale kwa aibu yetu, haya yetu na itufunike; kwa maana tumemwasi Bwana, Mungu wetu, sisi na baba zetu, tangu ujana wetu hata leo; wala hatukuitii sauti ya Bwana, Mungu wetu.”

  • ZINGATIA: “makutano yenye mshindo juu ya milima,” (v. 23) yaani, wingi wa waabudu kwenye vilele vya vilima na milima.

[8] “Aibu imeila kazi ya baba zetu tokea ujana wetu.” Unaelewa hili linamaanisha nini? (3:24) Mdokezo ni juu ya ibada ya Baali, ibada ya sanamu ya watu yenye kufedhehesha (cf. Yer. 11:13; Hosea 9:10), iliyoingizwa kipindi cha Waamuzi.

  • ZINGATIA: Ilikuwepo “idadi kubwa ya kondoo na mifugo waliotolewa kafara kwa miungu ya kipagani na watoto walioteketezwa kama kafara kwa Moleki, mungu moto wa Amoni” (Zab. 106:38; Yer. 7:31)” – (SDA BC 4:368).
Comments
Print Friendly, PDF & Email