Yeremia 3: Mwongozo wa Maombi

October 29, 2020 in Mwongozo wa Maombi by TGVS

Mwongozo wa Maombi Unaoshabihiana na “Mpango wa Usomaji Biblia” wa leo: Yeremia 3/ Dhima: Mambo Yasababisha Uzinzi wa Kiroho/24-BSG-3B, (Yeremia 3:8-9)/ Wimbo: I lay my sins on Jesus, [SDAH # 298].


 

Andiko Msingi: Yeremia 3:8–9  — 8 Nami nikaona, wakati nilipokuwa nimemwacha Israeli mwenye kuasi, nikampa hati ya talaka kwa sababu hiyo ya kuzini, dada yake, Yuda mwenye hiana, hakufanya hofu; bali yeye naye akaenda akafanya mambo ya ukahaba. 9 Hata ikawa, kwa sababu alikuwa mwepesi wa kufanya ukahaba, nchi ikatiwa unajisi, naye akazini na mawe na miti.

Maelezo ya Ufunguzi: Hebu tuzingatie kifupi hali zinazopelekea uzinifu wa kiroho. Kwanza, Hakuna Hofu ya Mungu (Yer. 3:8). Katika Ujumbe wa Malaika wa Kwanza, tunahimizwa “Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu Yake imekuja” (Ufu. 14:7a). Kumcha Mungu ni kuchukia dhambi na kuepuka uovu. Leo watu wengi hawamchi Mungu. Tunapaswa kuwa kama Mtume Paulo, alizimu “kunidhamisha” mwili wake na “na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa.” (1 Kor. 9:27)

Pili, kupoteza hisia ya dhambi: Yuda alifanya ukahaba “na mawe na miti” (Yer. 3:9). Dhambi ni ugonjwa wenye hila na wa kuhuzunisha sana. Huanza kidogo, mara nyingi kwa maridhiano, kisha tunakufa ganzi kwayo, na ghafla, kila kitu huwa cha kawaida. Kwa maneno mengine, tunapoteza hisia ya maagizo matakatifu ya Mungu maishani mwetu. Hebu sikiza onyo la BWANA— “Ole wao wasemao kwamba uovu ni wema, na kwamba wema ni uovu; watiao giza badala ya nuru, na nuru badala ya giza; watiao uchungu badala ya utamu, na utamu badala ya uchungu!” (Isaya 5:20, ESV)

Zingatia Neno la Mungu kwenye mada ya Dhambi– [A] Dhambi inahuzunisha (Mwa. 18:20)—kihisia na kimapenzi; [B] Dhambi hututenda na Mungu (Isa. 59:1-2); [C] Dhambi ni rekodi iliyoandikwa ambayo huacha alama yake, “imechorwa kwa kalamu ya chuma” (Yer. 17:1); [D] Dhambi ni hesabu ya kuongeza (siyo kutoa)—huongezwa daima (Isa. 30:1). Kwa kawaida dhambi haisimami pekee. Dhambi moja huhusisha kutendwa kwa nyingine. Dhambi moja inapotendwa, mara nyingi ni muhimu kutenda zingine ili kutekeleza na kukamilisha mpango mzima wa uovu. Kielelezo: Dhambi ya Daudi na Bathsheba; [E] Dhambi hujipatia ujira (Rum. 6:23); Ujira wake: hukumu na jehanamu (Ufu. 20:14-15).

Wapendwa, tunapokuja katika Kipindi cha Maombi leo, tunaalikwa—kutathmini dhambi zetu, Kuungama na Kutubu. Dhambi zote ni za kutisha machoni pa Mungu mtakatifu, na zinahitaji kufanyiwa toba mara moja.


 

Maadili ya Kukuza: “Ungama uovu wako tu; ya kwamba umemwasi Bwana, Mungu wako” (Yer. 3:13a); usiige njia ya ibada ya sanamu za Israeli ya Kaskazini iliyoasi.

Dhambi za Kuepuka/Kuungama: Unafiki; Ibada ya sanamu (uzinzi wa kiroho).

Jambo la Kumshukuru Mungu Kwalo: Karama ya Mungu ya Toba & Urejeshwaji.

Zingatia matokeo ya pekee ajabu ya Toba (Yer. 3:14-18):

  1. Tutawekwa huru kutoka utumwani (dhambi)
  2. Tutapewa walezi wa kweli wacha-Mungu (wachungaji, wazee, nk.).
  3. Tutapata fanaka ya ongezeko la umati, katika mwili wa waumini wa kweli
  4. Tutaabudu katika enzi hasa ya Mungu Mwenyewe—katika uwepo Wake
  5. Tutashuhudia uanzishwaji wa ufalme wa Mungu duniani
  6. Tutashuhudia uongofu wa Mataifa
  7. Tutaona urejeshwaji na muunganiko mpya wa Israeli
  8. Tutapewa urithi wa nchi tuliyoahidiwa.

Watu wa Kuombewa: Israeli ya Kiroho Pogofu. Waombee washiriki wa kanisa waliorudi nyuma, ili warejee kwa BWANA na kutubu–kwa sababu Mungu ni mwenye rehema; kwa sababu walikuwa wametenda dhambi, wamemwasi; kwa sababu walikuwa wamemkaidi Mungu na kuzikacha amri Zake (Yer. 3:12-13).

Masuala ya Kuombea: Ukahaba (Uzinzi), Talaka miongoni mwa waumini, Ibada ya kipagani, Unafiki, Ugumu wa moyo, Wachungaji watauwa katika makanisa mahalia, Ungamo la dhambi, Kumkaribia Mungu.

Ahadi ya Leo: “Mtafuteni Bwana, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yu karibu; Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie Bwana, Naye atamrehemu; Na arejee kwa Mungu wetu, Naye atamsamehe kabisa.” (Isaya 55:6–7)

Pamoja katika Maombi: Kwa uangalifu, tafuta maudhui ya maombi yako katika Yeremia 3. Zingatia vipengele vifuatavyo vya maombi — Usabihifu: Msifu Mungu jinsi alivyo na anavyofanana. Maungamo. Kiri na Kugeuka ([tubu] dhambi zako (angalia ‘Dhambi za Kuepuka/Kuungama’ hapo juu). Shukrani: Mshukuru Mungu kwa ajili ya tabia Yake, matendo Yake, karama Zake, na baraka Zake kila siku. Dua: Mwombe Mungu akusaidie ili utimize mahitaji yako kiroho na kimwili. Usahimifu: Jiadhimu nafsi kuyatii mapenzi ya Mungu. Maombezi: Mwombe Mungu mahitaji ya wengine.

Hatua ya Maamuzi: Fuata utaratibu huu rahisi wa “Kuomba Ukifuata Maandiko” halafu wasilisha maombi yako mbele ya Mungu. Fungua Biblia yako katika Yeremia 3: kadiri unapoisoma, tulia katika kila andiko na kuligeuza kuwa ombi! Kama una Mahitaji ya Kuombea, tafadhali yaandike hapa chini, na mtu fulani atayaombea.

Comments
Print Friendly, PDF & Email