Yeremia 21: Maswali na Majibu.

November 16, 2020 in Mwongozo wa Biblia by TGVS

Mwongozo wa Kujifunza Biblia/ Yeremia 21, (24-BSG-21J)/ Maswali na Majibu.


 

 

[1] Bainisha ujumbe uliotumwa na mfalme Zedekia kwenda kwa Yeremia (1). Pashuri mwana na Malkiya; na Sefania mwana wa Maaseya.

Mfalme Zedekia aliwatuma watu hawa wawili kwa Yeremia akiwa na ombi. “Pashuri, mmojawapo wa maafisa wa mfalme, baada alimrai mfalme amwue Yeremia kwa uhaini (cf. 38:1–4). Sefania alifuata baada ya Yehoyada (29:25–26) kama kuhani wa pili kwa cheo baada ya kuhani mkuu, Seraya (52:24). Hivyo Sefania alikuwa kiongozi wa pili mkuu zaidi wa kidini katika Yuda. Baadaye, kufuatia anguko la Yerusalemu (52:24–27), Sefania aliuliwa na Nebukadneza.” [Charles H. Dyer, The Bible Knowledge Commentary: An Exposition of the Scriptures, 1985, 1, 1155].

[2] Nini ujumbe wa Zedekia kwa Yeremia? (2) “Tafadhali utuulizie habari kwa Bwana; kwa maana Nebukadreza, mfalme wa Babeli, analeta vita juu yetu; labda Bwana atatutendea sawasawa na kazi Zake zote za ajabu, ili aende zake akatuache.” (Yeremia 21:2)

[3] Nini tamko la Mungu kwa Mfalme Zedekia? (4-7). Badala ya kumsaidia, Mungu alikusudia kumtumia Babeli kama wakala Wake wa haki na hukumu.

 • Mungu angezifanya silaha za mfalme zisifae kitu (4a).
 • Mungu angemruhusu adui aingie ndani ya mji (4b).
 • Mungu angeinua mkono Wake katika hasira, ukali, na ghadhabu (5).
 • Watu wengi wa Yuda na mifugo yao wangekufa kwa sababu ya tauni kali (6).
 • Wengi wangekufa vitani na wengine kutokana na njaa: kwa sababu ya kuhusuriwa na Babeli (7a).
 • Wengi miongoni mwa wahanga wangeuawa kama wahalifu kwa upanga (7b).
 • Wachache wangeachwa, wangeoneshwa rehema, au shufaka (7c)

ZINGATIA:

 • “Bwana anapuuza ombi la Zedikia kwa sababu alimwasi Bwana pamoja na Babeli (2 Flm. 24:19). Matokeo yake, Bwana asingempigania Zedikia; angempinga (v. 5), akihakikisha anashindwa (v. 7).” [NIV Biblical Theology Study Bible/ Jer. 21:4-7]
 • “Yeremia anawataarifu wawakilishi wa mfalme kwamba juhudi zao ni bure. Mungu hataondoa adhabu ya watu Wake. Wababeli watakuja karibu zaidi, wakisogea bila kuzuiwa, hadi mwishowe watakuja “katikati ya mji huu…. Mara nyingi katika historia yao, Israeli ilikuwa imewakabili maadui wenye nguvu zaidi kwa ujasiri, wakitumaini kwamba Bwana alikuwa pamoja nao. Lakini sasa “Mungu wa Israeli” (v. 4) anatangaza kwamba yu upande wa Wakaldayo wavamizi. Juhudi za Israeli hazina tumaini.” (SDA BC 4:433).

[5] Inaonekana kwamba Mungu alikuwa amegeuka na kuwaacha watu Wake. Kwa nini Mungu awapingane na watu Wake? (5) Kwa sababu ya uasi.

“Zipo sababu kadhaa: (1) Watu Wake walikuwa warudiarudia kutenda dhambi, wakivunja ahadi za agano walizoapa. (2) Walikuwa wamekataa wito wa Mungu daima kupitia manabii waliowahimiza watubu. (3) Sasa walikabiliwa adhabu ya hakika. Wakati mwingine Mungu huwatumia watu wadhambi au mataifa maovu kama mawakala Wake wa hukumu. Angalia makala, ‘Je Mungu huwatumia watu waovu kutenda mema?’ (Hab. 1:6).” [NIV Quest Study Bible/ Jer. 21:5].

[6] Nini tamko la Mungu kwa wakazi wa Yuda? (8-10) Twofold—

Kwanza, aliwapatia uchaguzi: njia ya uzima au njia ya mauti — “Nawe waambie watu hawa, Bwana asema hivi, Tazama naweka mbele yenu njia ya uzima, na njia ya mauti.” (Yeremia 21:8)

 • Zingatia kwamba, kama wangebaki mjini, wangekufa; kama wangeondoka mjini na kujisalimisha, wangeepuka mauti na kuishi (angalia Yer. 39:9; 52:15)
 • Linganisha: Kumbukumbu 11:26–2826 “Angalieni, nawawekea mbele yenu hivi leo baraka na laana; 27 baraka ni hapo mtakapoyasikiza maagizo ya Bwana, Mungu wenu, niwaagizayo leo; 28 na laana ni hapo msiposikiza maagizo ya Bwana, Mungu wenu, mkikengeuka katika njia niwaagizayo leo, kwa kuandama miungu mingine msiyoijua.”

Pili, alikusudia kuiletea Yerusalemu masahibu: kutekeleza hukumu kwa sababu ya maovu yao — “Maana nimeweka uso Wangu juu ya mji huu niuletee mabaya, wala nisiuletee mema, asema Bwana; utatiwa katika mkono wa mfalme wa Babeli, naye atauteketeza.” (Yeremia 21:10)

[7] Nini nasihi ya Yeremia kwa mfalme na familia yake? — kwa nyumba ya kifalme ya Yuda, na warithi wa utawala wa kifalme? (11-12). Lazima mfalme atende haki, yaani, lazima amwokoe mhanga kutoka kwa mhalifu. Sababu: ghadhabu ya Mungu hudai haki na hukumu.

 • ZINGATIA: Mungu angemtetea mhanga; ghadhabu ya Mungu ingechoma kama moto usiozimika dhidi ya uovu wa mfalme.

[8] Nini tamko la Mungu kwa wakazi wa Yerusalemu? (13-14). Walikuwa wamehukumiwa kwa sababu ya kujitegemea nafsi, kujitosheleza. Kwa sababu hawakumtumaini Mungu; kwa sababu ya dhambi zao. Hivyo wangeangamizwa kwa moto wa Mungu wa hukumu (Yer. 21:14).

 

 

Comments
Print Friendly, PDF & Email