Yeremia 38: Maswali na Majibu

December 7, 2020 in Mwongozo wa Biblia by TGVS

Mwongozo wa Kujifunza Biblia/ Yeremia 38, (24-BSG-38J)/ Maswali na Majibu


[1] Yeremia angewezaje kuhubiri wakati akiwa kifungoni? (38:1) “Pengine Yeremia alikuwa huru kutembea kwenye uwanda wa ufalme. Huenda wengine wengi walikuwa pia katika uwanda wa ufalme. Baadhi, kama Yeremia, inawezekana walikuwa kizuizini. Wengine walikuwa huru kuja na kwenda kadiri walivyopenda. Pengine Yeremia alizungumza na yeyote ambaye angemsikiliza, japo siyo kama mhubiri mimbarini. Aliwaambia tu watu kile ambacho Mungu alikuwa akimwambia, pengine akizungumza na mtu mmoja kwa wakati.” (NIV Quest Study Bible Notes/ Jer. 38:1)

[2] Nani alitaka Yeremia auawawe? (38:1) Shefatia mwana wa Matani, Gedalia, mwana wa Pashuri, Yukali, mwana wa Shelemia, na Pashuri, mwana wa Malkiya.

[3] Kwa nini walitaka kumuua nabii? (38:2-4) Kwa sababu alitoa ujumbe wa onyo kwa mara nyingine tena. Walimwona kama msaliti, siyo mtafuta-amani. Yeremia alitamka dhahiri shahiri kwamba “mji huu utatiwa katika mikono ya jeshi la mfalme wa Babeli.”

[4] Ni ujumbe wa aina gani ambao nabii alitangaza wakati huu? “Bwana asema hivi, Akaaye ndani ya mji huu atakufa kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni; bali yeye atokaye kwenda kwa Wakaldayo ataishi, naye atapewa maisha yake yawe kama nyara, naye ataishi. Bwana asema hivi, Bila shaka mji huu utatiwa katika mikono ya jeshi la mfalme wa Babeli, naye atautwaa.” (Yeremia 38:2–3)

[5] Zedekia alitumia maneno gani katika kujibu ombi la wakuu? (38:5) “Mfalme Zedekia alisema, “Tazama, yu mikononi mwenu; maana mfalme hawezi kufanya lolote dhidi yenu.” (Yeremia 38:5, ESV)

[6] Wapi walikomtupa Yeremia? “Basi wakamtwaa Yeremia, wakamtupa katika shimo la Malkiya, mwana wa mfalme, lililo katika uwanda wa walinzi; wakamshusha kwa kamba. Na mle shimoni hamkuwa na maji, ila matope tu; naye Yeremia akazama katika matope hayo.” (Yeremia 38:6)

[7] Elezea mateso ya kikatili ambayo baada ya hapo yalimkabili Yeremia akiwa mikononi mwa wakuu wa Kiyahudi? (angalia 38:6).

“Maafisa hao walimchukua Yeremia na kumtumbukiza kwenye kisima cha Malkiya, kwenye uwanda wa mlinzi. Kisima hiki kilikuwa shimo kubwa lililochimbwa kwenye mwamba na kufunikwa kwa plasta. Kilitumika kukusanyia maji ya mvua wakati wa wintili ambayo yangetumiwa wakati wa musimu wa hari (cf. 2:13). Kisima hiki kilikuwa na kina kirefu kiasi kwamba walilazimika kumtumbukiza Yeremia humo kwa kutumia kamba. Huenda kwa sababu ya ukame wa muda mrefu (cf. 14:1–4), kisima hiki hakikuwa na maji. Kilikuwa tu na matope yaliyokuwa yametwama kwa chini kutokana na uchafu uliotiririkia humo kwa maji ya mvua. Halafu Yeremia akazama kwenye matope hayo. Hakika maisha yalikuwa hatarini. Maji au matope yangekuwa ya kina zaidi, bila shaka angezama au kusongwa hewa, na kifo kwa kukosa chakula yalikuwa matarajio ya hakika. Pia huenda watu walimrushia mawe Yeremia, wakikusudia kumwua moja kwa moja au kumjeruhi ili azame kwenye matope na kufa (cf. maelezo kuhusu Lam. 3:52–54).” [Charles H. Dyer, The Bible Knowledge Commentary: An Exposition of the Scriptures, 1985, 1, 1183].

[8] Je Ebedmeleki alikuwa nani, naye alimfanyia nini Yeremia? (7-13) “Jina lake humaanisha “mtumishi wa mfalme.” Cheo chake, saris, kinaweza kutumika kijumla kwa ajili ya afisa wa kifalme (Mwa. 37:36; 2 Flm 23:11) au hususan kwa ajili ya towashi (Esta 2:3). Andiko humhusianisha na eneo la Kushi, lililoko kusini mwa Misri, takriban katika eneo la Ethiopia ya sasa. Yeremia anaokolewa na mgeni anayetambua udhalimu aliotendewa na watu wa nchi yake mwenyewe.” (Faithlife Study Bible/ Jer. 38:7).

[9] Nukuu kiapo cha dhati ambacho Zedekia swore to Yeremia — “Basi Sedekia mfalme akamwapia Yeremia kwa siri, akisema, Kama Bwana aishivyo, Yeye aliyetufanyia roho zetu, sitakuua, wala sitakutia katika mikono ya watu hao wanaokutafuta wakuue.” (Yeremia 38:16)

[10] Ni kwa maneno gani ambayo Yeremia alitumia baada ya hapo kumshauri Zedekia? — “Ndipo Yeremia akamwambia Sedekia, Bwana, Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Kama ukitoka kwenda kwa wakuu wa mfalme wa Babeli, basi nafsi yako utaishi, wala mji huu hautateketezwa; nawe utaishi na nyumba yako.” (Yeremia 38:17)

[11] Nini ambacho Yeremia alisema kingekuwa matokeo ya kutotii ushauri huu? — “Bali ukikataa kutoka kwenda kwa wakuu wa mfalme wa Babeli, basi, mji huu utatiwa katika mikono ya Wakaldayo nao watauteketeza, hata na wewe hutajiepusha na mikono yao.” (Yeremia 38:18)

[12] Maneno gani alitumia Zedekia kuelezea hofu yake kwa Yeremia, kutokana na mwenendo wake mwovu na wa fedheha? — “Mfalme Sedekia akamwambia Yeremia, Nawaogopa Wayahudi waliowakimbilia Wakaldayo, wasije wakanitia katika mikono yao, nao wakanidhihaki.” (Yeremia 38:19)

[13] Nukuu maneno ambayo Yeremia alimtumia kumnasihi Zedekiah ili autii ushauri wake — “Lakini Yeremia akasema, La! Hawatakutoa. Nakusihi, uitii sauti ya Bwana katika hayo ninayokuambia; ndivyo itakavyokufaa, na nafsi yako utaishi.” (Yeremia 38:20)

[14] Nukuu maneno Zedekiah kwa nabii kufuatia tukio la mahojiano yao ya mwisho— “Ndipo Sedekia akamwambia Yeremia, Mtu yeyote asipate habari ya maneno haya, nawe hutakufa. Lakini kama wakuu wakisikia ya kuwa nimenena nawe, nao wakija kwako, na kukuambia, Tufunulie sasa uliyomwambia mfalme; usimfiche, nasi hatutakuua; na pia uliyoambiwa na mfalme; basi, utawaambia, Nalimwomba mfalme asinirudishe nyumbani kwa Yonathani, nisije nikafa humo.” (Yeremia 38:24–26)

[15] Je ni muda mrefu kiasi gani Yeremia alidumu gerezani? “Basi Yeremia akakaa katika uwanda wa walinzi hata siku ile Yerusalemu ulipotwaliwa.” (Yeremia 38:28)

[16] Je Yeremia alikuwa wapi siku ile Yerusalemu ilipotwaliwa? — (Angalia aya ya 28) “Mkasa unahitimisha kwa kauli kwamba Yeremia alisalia kwenye uwanda wa mlinzi “hata siku ile Yerusalemu ulipotwaliwa.” Sura hii katika Kiebrania huhitimisha kwa maneno, “Hivi ndivyo Yerusalemu ilivyotwaliwa,” ambayo ni utangulizi wa mkasa unaofuata. Kwa tahamuli, miaka arobaini ya Yeremia kujinasibisha na Neno la Mungu ilikuwa imemleta hisia ya kuwa na kusudi maishani mwake ambayo kwa kiasi kikubwa ilibadilisha maisha yake (angalia wito wake, 1:4–10). Uzoefu wake ulileta kiwango fulani cha ukomavu ambao mwanzoni aliukana aliposema, “mimi ni mtoto” (1:6). Huduma yake ilisababisha uadui kutoka kwa watu wake, hata kutoka kwa familia yake, pamoja na mateso halisi ya kimwili na vitisho vya mauti. Lakini utii wake kwa huduma aliyompatia Bwana ulimbariki kwa ushirika pamoja na Mungu ambao wachache walipata. Alitumia maneno neʾum Yahweh (“asema Bwana”) zaidi ya mwingineyo katika AK (mara 176; angalia 1:8 kwa ajili ya maelezo ya kirai hiki). Miaka yake ya unasibishaji ulimletea uzoefu tele na mbalimbali pamoja na watu tofautitofauti, wema na wabaya, marafiki na maadui. Utii wake ulimpeleka maeneo mengi—kifungo cha shimoni, kwenye kisima, na uhamishoni Misri. Kwa Yeremia, kuifanya kazi ya Bwana kulimaanisha chochote isipokuwa maisha maridhawa.” [F. B. Huey, Yeremia, Lamentations, The New American Commentary, (Nashville: Broadman & Holman Publishers, 1993), 16:340].

 

Comments
Print Friendly, PDF & Email