Yeremia 38: Maswali ya Kujadili

December 4, 2020 in Maswali ya Kujadili by TGVS

Mwongozo wa Kujifunza Biblia/ Yeremia 38: Maswali ya Kujadili/ Yeremia 38, (24-BSG-38K)


 

TAFAKARI NA KUJADILI – [1] Durusu Yeremia 38:17-18. Yeremia haina maneno yoyote mapya kwa ajili ya Mfalme Zedekia; Yeremia hurudia tu kile alichomwambia hapo kabla (angalia Yer. 27:1–15). Wababeli walikuwa mawakala wa Mungu wa hukumu dhidi ya Yuda, na mfalme na watu wa Yuda lazima waafikiane neo kwa ajili ya usalama wao. Upinzani dhidi yao utakuwa ujinga na ubatili. Ni bora kujisalimisha kwao na kutii mapenzi ya Mungu.

Wapendwa, hakuna Injili Mpya. Ujumbe wa Mungu ni rahisi sana kuanzia Mwanzo hadi Ufunuo: Tubuni Mpatanishwe Kwangu! Kwa nini inatokea kwamba kuna uasi mkubwa sana katika kizazi hiki? Ni kwa vile wahubiri wameishiwa Mahubiri Mapya? Au ni kwa sababu ya ugumu wa mioyo? Linganisha na kujadili maneno ya Kristo kuhusu hali ya watu mara tu kabla ya Ujio Wake wa Pili (Luka 17:26-32).

[2] Katika aya ya 7-13, tunaona jinsi BWANA anavyowainua mawakala, kutoka maeneo yasiyotarajiwa kabisa, kwa ajili ya ukombozi wa watu Wake. Hapa alikuwepo Ebedmeleki, towashi wa Ethiopia– (mgeni na Mmataifa)—aliyeguswa kushughulikia hatima ya nabii wakati watu wote katika nchi walikuwa wakiridhia kifo chake. Linganisha hili na Mfano wa Msamaria Mwema, Mmataifa pia (Luka 10:25-37) aliyemwokoa mhanga kutoka kwa wanyang’anyi, alimleta kwa mganga wake na kugharamikia matibabu yake — wakati ambapo wala si Kuhani au Mlawi angemwonea huruma.

[3] “Nawaogopa Wayahudi waliowakimbilia Wakaldayo” (Yer. 38:19) “Kwa mara nyingine tena, udhaifu wa tabia wa Zedekia unajionesha. Kulikuwa na mwenendo wa tabia wa kufuatwa ambapo alijua kuwa sahihi, lakini alikosa ujasiri wa kufanya maamuzi wa kuufuata.” (Thompson). Mfalme anahofu mambo tofauti. Badala yake angepaswa kuwa na hofu dhidi ya BWANA na kumtii Yeye (v. 20). Andika orodha ya mambo yanayokutisha sana. Mara ngapi umekosa ujasiri wa wa kumtumaini BWANA katikati ya hali hizo? Je hivi sote tuna hatia kuhusu hili? Ni aya zipi nyingine zaidi kwenye Maandiko tunazoweza kutumia kufikishia ujumbe huu?

[4] “Mtu yeyote asipate habari ya maneno haya” (Yer. 38:24). Udhaifu wa Zedekia unastaajabisha sana: hawezi kuhakikisha usalama wa Yeremia, jambo aliloapa hapo awali (Yer. 38:16), isipokuwa maafisa wake wakiwekwa gizani. Pale maafisa wa mfalme wanapomuuliza Yeremia kuhusu mazungumzo yake na mfalme, anafanya kama alivyoomba mfalme. Yeremia aoneshi kile ambacho Mungu alimwambia Zedekia, bila shaka akiamini kwamba ilimhusu mfalme na Mungu. ZINGATIA: Hii ilikuwa “kusema ukweli, wala si jambo lingine lolote bali ukweli, lakini si ukweli wote.” Kile ambacho Yeremia alithibitisha hapa ni kuuficha ukweli? Je analazimika kukiri ukweli kwa wauaji hawa wanaotafuta kumuua?

KUCHUNGUZA ZAIDI –[5] Sura hii, miongoni mwa mambo mengine, hutukumbusha uzoefu wa waumini katika maisha haya → chuki, mateso, kusumbuka kwa ajili ya Mungu. Yeremia alidumu kuwa mwaminifu kwa wito/wajibu wake. Ni maandiko gani mengine ya Biblia unayoweza kutumia kwenye mada ya mateso kwa ajili ya Mungu? Yesu Kristo alifundisha (kwa kanuni na mfano) licha ya upinzani, hatari, mateso, masumbufu, hata mauti. Kwa nini alijikita katika utume Wake licha ya haya yote? Ni kilichomfanya adumu kusonga mbele? Ni somo gani la maisha tunaloweza kujifunza kutoka kwa Yeremia na Kristo kwa ajili ya kizaji hiki?

KUJITATHMINI –[6] Katika sura hii, tunaona udhaifu wa Mfalme Zedekia: pale ambapo kundi moja la maafisa wake (wakuu wanne) wanapokula njama za kumuua Yeremia, mfalme hafanyi lolote la kuwazuia wasitende hivyo, lakini mtumishi wake mwingine–(Ebedimeleki, towashi wa Ethiopia) — anapotaka  kumwokoa Yeremia, anamuunga mkono. Linganisha hili na njama dhidi ya Danieli (Yer. 38:4-10, cf. Dan. 6:1-5). Ni mara ngapi umekosa fursa iliyopo “ndani ya uwezo wako” kufanya jambo jema, kwa sababu tu ya usahihi wa kisiasa? Au kwa sababu ulitaka kutimiza shauku ovu za washirika wako?

KWA MAISHA YA LEO –[7] “Ndipo wakuu wakamwambia mfalme, Twakuomba, mtu huyu auawe, kwa kuwa aidhoofisha mikono ya watu wa vita, waliobaki katika mji huu, na mikono ya watu wote, kwa kuwaambia maneno kama hayo; maana mtu huyu hawatafutii watu hawa heri, bali shari. (Yeremia 38:4) Kimsingi walikuwa wakishutumu kwamba maneno ya Yeremia yalikuwa yakiwakatisha tamaa askari! Ujumbe endelevu wa Yeremia kuhusu anguko la Yerusalemu, bila kushangaza, uliwakatisha tamaa wale wanaousikia. Ndiyo maana haishangazi basi kwamba wakati Waadventista wanapotangaza ujumbe wa hukumu (Ufu. 14:6-12) ulimwengu huwachukia. Wahubiri wengi waaminifu watatupwa gerezani (Ufu. 2:10) kwa kushutumiwa kwamba wanatangaza “mahubiri ya chuki,” kwa kuita dhambi kwa jina lake, kwa kusisitiza hitaji la kudumisha Sheria ya Mungu (ikiwa ni pamoja na Sabato), nk. Jinsi gani unajiandaa kuwasaidia wahubiri hawa wasimame imara katikati ya upinzani huu? Jinsi gani wito wa Yeremia, ufaradhishwaji, uwakifishwaji, kila mahali hukuimarisha wakati ukitenda kazi katika shamba la BWANA katika siku hizi za mwisho?

KUCHUNGUZA KWA KINA ZAIDI –[9] Zedikia alikuwa mtu mwenye tabia ya kutisha ilioje! Hakika alikuwa na usadikisho thabiti kuhusu maneno ya Mungu: alitetemeka alipoyasikia maneno hayo, hata hivyo aliridhia kumuua mhubiri. Nini tofauti kati ya Zedikia na Feliki? (Durusu na kujadili hukumu ya Paulo mbele ya Feliki, Matendo 24).

UMUHIMU KWA MTU BINAFSI –[10] Wajibu: Penda Usipende, Wajibu wa Mwisho Humwangukia Kiongozi

“Matumizi mabaya ya mamlaka siyo tu pale viongozi wabaya wanapotenda kwa ubinafsi, bali pale viongozi wema wanapopuuza kufanya kile wanachopaswa kutenda. Katika hili, Mfalme Zedekia alikasimisha wajibu asioupenda kwenda kwa mwingine, akijitangaza kukosa uwezo wa kutenda. Mfalme alikosa ujasiri wa kutumia mamlaka yake kumlinda nabii wa Mungu.

Yeremia, kwa upande mwingine, aliendelea kuwajibika kwa ajili ya wito mgumu. Alitangaza uangamivu wa watu wake mwenyewe, akimtaja Babeli kama mtekelezaji husika. Hebu fikiria wewe ni mwinjilisti unasimama kanisani leo, ukitangaza kwamba alikuwa akiwainua wakomunisti ili kuwaadhibu Wamarekani. Unatangaza kwamba Mungu hajali lolote kuhusu Tamko la Uhuru au Katiba; kwa kweli, mambo tunayosisitiza yanamchukiza Mungu. Kama ukijaribu kuacha kutangaza ujumbe huu, unakuwa mwasi. Maneno husika yanachoma ndani yako, hivyo unalazimika kuzungumza. Hivyo unaendelea kutekeleza wajibu huo, siyo ule ambao ni mashuhuri. Ndivyo alivyokuwa Yeremia na ujumbe wake.” (NKJV Maxwell Leadership Bible/ Yeremia 38:1–6)


 

 

MWISHOSauri ya Injili/ Mwongozo wa Kujifunza Biblia/ Yeremia 38: Maswali ya Kujadili.

Comments
Print Friendly, PDF & Email