Ezekieli 30: Maombi

January 21, 2021 in Mwongozo wa Maombi by TGVS

Ezekieli 30: Maombi/ Januari 21, 2021/ 26-BSG-30B, (Ezekieli 30:1-26)/ Dhima: Hukumu ya Mungu juu ya Misri/ Wimbo: Imeanzishwa Hukumu (SDAH 416)

Ezekieli 30:22–24 — 22 Basi Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, Mimi ni juu ya Farao, mfalme wa Misri, nami nitamvunja mikono yake, mkono ulio wenye nguvu, na huo uliovunjika, Nami nitauangusha upanga ulio katika mkono wake. 23 Nami nitawatawanya Wamisri kati ya mataifa, na kuwatapanya kati ya nchi mbalimbali. 24 Nami nitaitia nguvu mikono ya mfalme wa Babeli, na kuutia upanga Wangu katika mkono wake, bali mikono ya Farao nitaivunja, naye ataugua mbele yake, kwa mauguzi ya mtu aliyetiwa jeraha ya kumfisha.


 

Kirai Muhimu: “Watajua ya kuwa Mimi ndimi Bwana.” (Eze. 30:8, 19, 25, 26).

Maelezo ya Ufunguzi: Tena na tena, Mungu aliyapatia mataifa haya onyo, lakini yalikataa kutubu, kumjua Yeye na kumkiri kama Mturufu wa Mbinguni na Duniani. Matokeo yalikuwa yapi? Uharibifu na uangamivu kamili. Kwa jinsi hiyohiyo, Mungu anatamani kwamba tuje Kwake ili tuokolewe! Anataka kutubariki! Anataka kuwa na uhusiano binafsi pamoja nasi – kuwa Mungu wetu nasi watu Wake! Henoko alienenda na Mungu kila siku. Sisi nasi tunaweza—kwa kutii amri Zake na kuwasiliana Naye katika maombi

Maadili ya Kukuza: Maungamo ya Dhambi; Sahama/ Heshima kwa Mungu; Toba ya kweli; Kutangaza Siku ya BWANA ijayo!

Dhambi za Kuepuka/Kuungama: Kiburi (Eze. 30:6); Kushindwa kutambua (kukiri) kwamba BWANA ni mkuu kuliko mtawala yeyote wa kidunia, na kwamba Yeye ni Mtawala Turufu wa Ulimwengu (Eze. 30:8, 19, 25, 26); Kusujudia sanamu, vinyago, nk. (Eze. 3013).

Jambo la Kumshukuru Mungu Kwalo: 1. Anatuma mfululizo wa Maonyo kabla ya Hukumu/ 2. Huwanyenyekesha wenye Kiburi: Mikono ya Farao itavunjwa, na watu wake watatawanywa (Eze. 30:20–26)/ 3. Amepanga siku (ameandaa) ambapo atawahukumu watu wa ulimwengu kwa haki (Matendo 17:31)/ 4. Ataikomesha dhambi na kurejesha utakatifu na haki milele/ 5. Jesus Kristo ni Jemadari Hodari! Sisi tunaomfuata Yeye ni “zaidi ya washindi na pia ushindi mkuu kupitia Yeye aliyetupenda [sana kiasi kwamba alitufia]” (Rum. 8:37, AMP).

Watu wa Kuombea: Farao Mwasi, mfalme wa Misri (cf. Eze. 29:2-3) — Waombee wanadamu wote wamkiri na kumstahi Mungu kama Mtawala Turufu wa Ulimwengu.

Mambo ya Kuombea: Ibada ya Sanamu, rehema ya Mungu katikati ya Hukumu, Ushindi dhidi ya Kiburi, maandalizi kwa ajili ya Siku ya BWANA.

Hitaji Mahususi: Fedha za kujenga Akademi ya TGV, Kanisa, Kituo cha Habari, na Kituo cha Huduma ya Afya.

Ahadi ya Leo: “Ila kwa rehema Zako nyingi hukuwakomesha kabisa, wala kuwaacha; kwa maana Wewe u Mungu mwenye neema, mwenye rehema.” (Nehemiah 9:31)


 

OMBI LA KUHITIMISHA

Mwongozo wa Kujifunza Biblia/ Ombi la Kuhitimisha/ Ezekieli 30, (26-BSG-30Z)/ Januari 21, 2021/ Je kuna ombi kwa ajili yangu kuomba/kuliakisi katika sura hii? Ndiyo.

 

Sala: Baba, tunakushukuru kwa ajili ya Neno Lako katika Ezekieli 30. Tunakushukuru kwa ajili ya karama ya uhai; kwa ajili ya fursa nyingine ya kuisikia Injili na kufanya mabadiliko stahiki maishani mwetu.

Baba, tuliona oroha ya Dhambi Mahususi katika sura hii — Kiburi (Eze. 30:6); Kushindwa kutambua (kukiri) kwamba Wewe ni mkuu zaidi kuliko utawala wowote duniani, na kwamba Wewe pekee ndiye unastahili kusifiwa na kuabudiwa (Eze. 30:8, 19, 25, 26); Kuabudu sanamu, vinyago, nk. (Eze. 30: 13). Tunakiri dhambi hizi, na kwa dhati tunaomba msamaha, utakaso na ushindi dhidi yazo. Tusaidie kutubu/kutangaza kwamba Wewe ni “BWANA Mungu,”– Mtawala wa Mbingu na Dunia.

Tunakushukuru kwa ajili ya tabia Yako isiyobadilika – Rehema, Neema, Uvumilivu, wingi wa Wema na Kweli, “mwenye kuwaonea huruma watu elfu elfu, mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi.” (Kut. 34:6-7). Turehemu, BWANA mpendwa, na tafadhali usituadhibu kwa ajili ya dhambi hizi ambazo tena na tena tumezitenda kwa upumbavu dhidi Yake.

Tunakushukuru kwa ajili ya matendo yako ya Hukumu. Hebu Roho Wako atusaidie kukumbuka kwamba Hukumu inaendelea sasa hivi; kwamba haina budi “kuanza katika nyumba ya Mungu” —yaani, sisi! (1 Pet. 4:17); na kwamba hatuna budi kuwa tayari sasa, kabla mlango wa rehema haujafungwa na ghadhabu ya Mungu kuwajia “wana wa uasi” (Efe. 5:6).

Tunakushukuru kwa ajili ya baraka za kila siku; kwa ajili ya Karama na Ahadi za Karama – Ndiyo, kwa ajili ya ujio wa “Siku ya BWANA!” Tusaidie tusiiogope Siku hii, bali badala yake tuwe katika hali ya matarajio: tukikesha na kuomba, tukiisha maisha ya usahimifu -maisha matakatifu – (mwenendo, tabia takatifu, na utauwa); tukionesha ustahivu adhimu kwa Mungu wetu shanani; ilhali tukitazamia kwa dhati na kungojea ujio wa Siku ya BWANA – wakati ule ambapo mbingu zitaangamizwa kwa moto, na mawadi au viasili vitayeyuka katika moto mkali! (2 Pet. 3:11–12)

Baba, tafadhali tusaidia kukidhi mahitaji yetu – (kimwili & kiroho). Baba, tunasihi kwa ajili ya rasilimali na nyenzo za kujengea Kituo, Kampasi, Shule itakayoitwa kwa Jina Lako. Ni shauku yangu ya dhati kuiona hii Miongozo ya Kujifunza ikichapishwa siku moja na kutangazwa mubashara kwenye Redio/Televisheni, ili watu Wako waweze kusoma, kusikiliza, kufahamu Injili Yako, na kuokolewa. Tafadhali ridhia ombi hili kadiri ya mapenzi Yako.

Baba, vilevile tunaomba mahitaji ya wengine: wengi wanalia; wengi wanatoa machozi ya huzuni; wengi wamewapoteza wapendwa wao; wengi hawana kazi; wengi wangali wakifa kwa Kovidi-19 pamoja na maradhi mengine; wengi wamepoteza Tumaini—tafadhali rehema, BWANA mpendwa!

Hebu Roho Wako atufundishe kuyatii mapenzi Yako, Amri Zako na Maagizo Yako. Samehe, BWANA mpendwa, tutakase, na kutuandaa kwa ajili ya ufalme Wako. Tunakushukuru, Baba, nasi tunaomba haya tukiamini na kutumaini katika Jina la Yesu Kristo, Amina.


 

TAFAKARI: “Imeanzishwa Hukumu” (NZ # 171)/ “The Judgment Has Set”

Imeanzishwa hukumu mbinguni; Tutasimamaje pale
Apomapo Mungu hakimu kula wazo na tendo?

Tutasimamaje sote katika siku kuu ile?
Dhambi zitu zitafutika ama zitatuangusha?

Wametangulia wafu kupimwa, Kitambo ndipo wahai,
Watapokea neno la mwisho, Vitabuni mwa Mungu.

Tutasimamaje usiku ule, Siri zetu, kila moja,
Zafunuliwa toka vitabu; Yesu atusaidie!

 

 

 

 

 

Comments
Print Friendly, PDF & Email