Danieli 1: Maswali na Majibu

February 9, 2021 in Mwongozo wa Biblia by TGVS

Mwongozo wa Kujifunza Biblia/ Danieli 1, (27-BSG-1J)/ Maswali na Majibu


 

[1] Danieli alikuwa nani? Kuzaliwa na nasaba yake vimeachwa katika sintofahamu kabisa isipokuwa kwamba alikuwa kijana wa kidini kutoka Yerusalemu. Alikuwa wa ukoo wa kifalme, pengine wa nyumba ya Daudi. Alichukuliwa utumwa na Nebukadneza wa Babeli.

[2] Zungumzia kuhusu Uandishi na Tarehe ya Kitabu cha Danieli. “Fasili kadhaa huonesha kwamba mwandishi ni Danieli (Dan. 8:15, 27; 9:2; 10:2, 7; 12:4, 5), ambaye jina lake humaanisha “Mungu ni Mhukumu Wangu.” Aliandika katika nafsi ya kwanza kuanzia Dan. 7:2 na kuendelea, na hutofautishwa na watu wengine watatu wenye jina la Danieli katika AK (cf. 1 Nyak. 3:1; Ezra 8:2; Neh. 10:6). Wakati akingali shababi, pengine takriban umri wa miaka 15, Danieli alitekwa kutoka kwenye familia yake ya kisharifu huko Yuda, akahamishiwa Babeli ili akadhilimishwe katika utamaduni wa Babeli kwa ajili ya jukumu la kusaidia katika kushughulika na Wayahudi waliohamishwa. Akiwa hapo alitumia sehemu iliyosalia ya maisha yake marefu (miaka 85 au zaidi). Alitumia vema fursa ya uhamishoni, kwa kufanikiwa kumtukuza Mungu kwa tabia yake na utumishi. Haraka aliinuka katika hadhi ya afisa mtawala kwa uteuzi rasmi wa kifalme na akatumika kama msiri wa wafalme pamoja na nabii katika falme mbili za ulimwengu, yaani, Babeli (Dan. 2:48) na Umedi-Uajemi (Dan. 6:1, 2). Kristo alimthibitisha Danieli kama mwandishi wa kitabu hiki (cf. Mat. 24:15).” [John MacArthur, The MacArthur Bible Handbook, (Nashville, TN: Thomas Nelson Publishers, 2003), 216–217].

[3] Wakati gani Danieli alitwaliwa kwenda Babeli? Katika mwaka wa tatu wa kumiliki kwake Yehoyakimu, mfalme wa Yuda (1:1). “Pale Nebukadneza alipokuja kuishambulia Yerusalemu katika mwaka wa tatu wa Yehoyakimu, katika majuma machache au, si zaidi ya miezi michache kabla y akifo cha babaye, bado hakuwa mfalme. Lakini Danieli, akirekodi matukio haya, huenda katika mwaka wa kwanza wa Koreshi (v. 21), takriban miaka 70 baada ya kufanyika matukio yaliyobainishwa, anamwita Nebukadneza “mfalme wa Babeli.” Wakati Danieli alipofika Babeli alikuwa kijana mateka, tayari, Nebukadneza alikuwa mfalme. Tangu wakati huo na kuendelea, alimwona Nebukadneza akitawala kwa miaka 43. Hivyo, inaonekana kuwa jambo la asili kabisa kwamba Danieli angemwita “mfalme.” (SDA BC 4:756).

[4] Wapi ambapo Nebukadneza aliweka vyombo alivyochukua kutoka katika nyumba ya Bwana huko Yerusalemu?Akavichukua mpaka nchi ya Shinari” (1:2b) “Baadhi ya vyombo na samani za hekalu la Mungu vilijumuisha vikombe vya dhahabu na fedha na vyombo vingine vilivyotumika katika sherehe hekaluni

huko Yerusalemu. Hezekia alikuwa amewaonesha Wababeli hazina hizi miaka mia kabla ya tukio hili (cf. Isa 39:2, 4), na Isaya alikuwa ametabiri kwamba wakati fulani vingetwaliwa kwenda Babeli (Isa 39:6). Nebukadneza alijitwalia sehemu tu (“baadhi”) ya hazina za hekalu katika wakati huu; zilizosalia zingetwaliwa katika mashambulio yaliyofuatia. Takriban miaka sitini na sita baadaye, Belshaza angevileta vyombo hivi katika karamu yake na kuvinajisi (cf. 5:2–4). Vyombo hivi vilitwaliwa kwa sababu ya thamani yake (dhahabu na fedha) na kama nyara za vita (cf. 1 Sam 5:2; 21:9).” [Stephen R. Miller, Daniel, The New American Commentary, (Nashville: Broadman & Holman Publishers, 1994), 18:58].

Zingatia: “Bila Nebukadneza alitwaa vyombo vya hekaluni vilivyo bora na vyenye thamani zaidi ili kuvitumia katika utumishi wa mungu wake Marduku. Kiasili hakuacha chochote zaidi ya kilichohitajika kutekelezea kaida za kila siku kwenye hekalu la Jerusalemu. Kulikuwa na nyakati tatu ambapo Wakaldayo walitwaa vyombo vitakatifu hadi Babeli: (1) katika kampeni iliyorekodiwa kwenye ujumbe huu, (2) wakati Jerusalemu ilipotwaliwa mwishoni utawala wa Yehoyachini mnamo mwaka 597 K.K. (2 Wafalme 24:13), na (3) mwishoni mwa utawala wa Zedekia, ambapo, katika mwaka 586 K.K. baada ya kuzingirwa muda mrefu, Yerusalemu ilitekwa na kuangamizwa (2 Wafalme 25:8–15). Uharibifu wa hazi za Yerusalemu uliofanywa na majeshi ya Babeli ulikuwa utimizwaji wa unabii wa Isaya uliotangazwa takriban karne moja kabla ya hapo (Isa. 39:6). Kuhusu mustakabali wa Sanduku la Agano, angalia maelezo juu ya Yer. 37:10.” (SDA BC 4:756–757).

[5] Zipi sifa za wale waliochaguliwa wafundishwe maarifa na lugha ya Wakaldayo? Vijana ambao hawakuwa na dosari yoyote, wenye sura nzuri, wenye karama katika hekima yote, wenye maarifa na wepesi kuelewa, waliokuwa na uwezo wa kutumika katika ikulu ya mfalme (1:4)

[6] Kwa nini Nebukadneza awaelimishe viongozi wa wateka? (1:4) “Wakati wowote Wababeli walipouteka mji fulani, waliwaondoa maafisa wa kifalme, askari, maafisa, mafundi, wasanifu na watu wenye utajiri (2 Flm. 24:14). Wengi walifundishwa kuhusu historia Babeli, utamaduni wake na fikra husika ili waweze kutumika kama watumishi wa kiraia. Kwa namna hii, waliimarisha utawala wao juu ya watu na nchi walizoteka.” (NIV Quest Study Bible)

[7] Majina gani waliyopewa Waebrania vijana hawa?  “Mkuu wa matowashi akawapa majina; alimwita Danieli, Belteshaza; na Hanania akamwita Shadraka; na Mishaeli akamwita Meshaki; na Azaria akamwita Abednego.” (Danieli 1:7)

“Kwa mujibu wa fasili ya 3, “mkuu wa matowashi” alikuwa Ashpenazi, aliyewateulia majina vijana mateka hawa ili kuwasimilisha kirahisi zaidi katika utamaduni wao mpya. Pengine halikuwepo kusudi kwa upande wa Wababeli kuwatweza au kuwadhalilisha mateka hawa kwa badiliko hili la majina. Wayahudi walionekana kukubali kwa suala halisia ukweli kwamba walipaswa kuwa na majina ya udhaibuni juu ya yale ya Kiebrania. Mfano, Yusufu alipewa na Farao jina la Kimisri (Mwa. 41:45), na Hadasa anajulikana kwa jina lake la ughaibuni kama Esta (Esta 2:7). Lacocque anabaini vema kwamba vijana hawa Waebrania hakuwa na uchaguzi katika suala husika. Wayahudi wengi katika nyakati za Agano Jipya walikuwa na majina ya Kiyunani pamoja na Kiebrania (au Kiarami). Mfano ni Petro (Kiyunani), aliyekuwa akiitwa Kefa katika Kiarami (cf. Yohana 1:42). Sauli naye anajulikana vema zaidi kwa jina lake la Kirumi kama Paulo.” [Stephen R. Miller, Daniel, The New American Commentary, (Nashville: Broadman & Holman Publishers, 1994), 18:64–65].

[8] Nini ambacho Danieli alikusudia moyoni mwake kwamba asingefanya? Kwamba asingejitia unajisi kwa chakula cha kifahari cha mfalme, wala mvinyo aliokunywa (1:8)

[9] Kwa nini Danieli alipinga ulaji wa chakula cha mfalme? “Zilikuwepo sababu kadhaa kwa nini Myahudi mtauwa angeepuka kula chakula cha kifalme: (1) Wababeli, kama yalivyo mataifa mengine ya kipagani, walikula nyama najisi; (2) hayawahi hawakuwa wamechinjwa kwa usahihi kwa mujibu wa sheria ya Walawi (Law. 17:14, 15); (3) sehemu ya chakula cha wanyama iliyoliwa kwanza ilitolewa sadaka kwa miungu ya kipagani (angalia Matendo 15:29); (4) matumizi ya chakula na vinywaji vya kifahari yalikuwa kinyume cha kanuni makini za mafundisho kiasi na kujitawala; (5) kwa Danieli na marafiki zake kulikuwa na na shauku ya ziada ya kuepuka mlo wa nyama. Vijana hawa wa Kiebrania waliazimu kutofanya chochote ambacho kingevuruga maendeleo ya kimwili, kiakili, na kiroho.” [Francis D. Nichol, Ed., The Seventh-Day Adventist Bible Commentary, (Review and Herald Publishing Association, 1977), 4:760].

[10] Pale mfalme alipowatahini vijana hawa wa Kiebrania kuhusiana na hekima na ufahamu, walionekanaje? “Akawaona kuwa walifaa mara kumi zaidi ya waganga na wachawi [wasomi] waliokuwa katika ufalme wake” (1:20, AMP).

Comments
Print Friendly, PDF & Email