Danieli 2: Mwongozo wa Ibada

February 10, 2021 in Mwongozo wa Ibada by TGVS

Danieli 2: Mwongozo wa Ibada/ 27-BSG-2A, (Danieli 2:1-49)/ Dhima: Jiwe lililochongwa bila kazi ya mikono/ Wimbo: Yesu Anakuja Tena! (NK 161).


 

UCHUNGUZI: Kuanzishwa kwa ufalme wa Mungu wa utukufu – (Danieli 2; 7; cf. 1 Kor. 15:24; 2 Thes. 1:7–8; 2 Pet 3:12; Ufu. 19:6-9, 11–16; 21:1-5).

TAFAKARI: Danieli sura ya 2 inaeleza juu ya “ndoto aliyopewa mfalme katika ishara za sanamu iliyoundwa kwa madini mbalimbali yakitawanda kwa kupungua thamani kutoka kwenye dhahabu hadi udongo na hatima kuharibiwa kwa jiwa lenye asili turufushani. Mfalme na wenye hekima wake hawana uwezo wowote wa kuikumbuka ndoto husika au kutambua umuhimu wake. Lakini hatima ya mataifa iko mkononi mwa Mungu wa mbinguni anayedhihirisha maudhui ya ndoto kwa Danieli na kubainisha ufafanuzi wa kieskatolojia wa ndoto husika. Ufunuo wa kiungu unaweka wazi kuhusu hukumu itakayoangamiza falme za ulimwengu wa sasa mwovu na kuanzisha utaratibu mpya wa Mungu ulimwenguni. Taanani iko katika siku za mwisho na uanzishwaji wa ufalme wa Mungu wa milele.” (Douglas Bennett, Symposium on Daniel: Introductory and Exegetical Studies, 1986, 2, 345–346).

MAANA YA KIIBADA: Nawe ukatazama hata Jiwe likachongwa bila kazi ya mikono, nalo jiwe hilo likaipiga sanamu miguu yake, iliyokuwa ya chuma na udongo, likaivunja vipande vipande.” Mara saba Maandiko yanamwita Yesu Kristo, ishara ya nguvu na udaima. Katika sura hii, Kristo — Jiwe lililoiseta Sanamu ya Metali – litayaseta mataifa kuwa vipandevipande! Tafadhali zingatia kwamba Jiwe hili litakuwa “milima mikubwa, likaijaza dunia yote.” Ufalme wa Kristo “utasimama milele na milele” (Danieli 2:34, 35, 44).

Unabii huu utatimizwa wakati wa Ujio wa Pili. Ujio Wake siyo mwisho wa ulimwengu, bali mwanzo wa “mbingu mpya na nchi mpya” (Ufu. 21:1-5). Mlima ni alama ya nguvu ya udaima. Kristo atakapokuja katika uweza na utukufu mwingi (Marko 13:26), Yeye aliye thabiti kupiga pia atakuwa thabiti kuokoa (Ebr. 7:25). Ili kuielewa sura hii vema zaidi, tunaangalia dhana nyingi kutoka kwa mtume Paulo, huku akizungumza juu ya Kristo, anaandika: “Hapo ndipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme Wake; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu. Maana sharti amiliki Yeye, hata awaweke maadui Wake wote chini ya miguu Yake.” (1 Wakorintho 15:24–25) Wapendwa, hivi karibuni sana, “Ufalme wa dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo Wake.” (Ufu. 11:15). Atatawala milele na milele! Na Jina Lake liko juu ya kila jina, na ndivyo itakavyokuwa hivyo milele! (Filp. 2:9).

SAUTI YA INJILI: Sehemu hiyo imeandikwa kana kwamba Mungu anazungumza nawe moja kwa moja — kwa sababu Yeye anafanya hivyo. Bwana ananiambia nini asubuhi ya leo? Mwanangu, miaka mingi sana iliyopita, nilimpatia Nebekadneza, mfalme wa Babeli, ndoto. Ndoto hii ilimfadhaisha kiasi kwamba asingeweza tena kulala. Kw ajinsi hiyohiyo, nazungumza nawe kama ninavyojaribu kuzungumza na Nebukadneza: muda unatoweka; hivi karibuni ghadhabu yangu itawapata watoto wa uasi (Kol. 3:5-6). Hivi karibu, Kristo Kristo ataonekana mawinguni Naye atawatwaa wenye haki kwenda katika ufalme Wanguwa haki na wa milele (Mat. 24:30; Ufu. 1:7). Je uko tayari kwa ajili ya kutokea kwa Kristo?

Shauku Yangu: Kwa neema ya Mungu, nataka kujifunza kikamilifu mafunuo ya unabii wa Danieli na Ufunuo. Nataka kuwashirikisha kweli hizi wale wanaonizunguka ili tuwe tayari kwa ajili ya Ujio wa Pili.

Iweni na Siku Yenye Baraka: “Na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi Yake; bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele.” (Danieli 2:44)


 

Kuabudu Kupitia Uimbaji: Piga Panda! (NK 161).

1. Piga panda na ya makelele; Yesu yuaja tena!
Ipate sauti, imba sana; Yesu yuaja tena!

[Kibwagizo] “Anakuja, anakuja; Yesu yuaja tena!”

2. Itoe mwangi sana vilima; Yesu yuaja tena!
Yuaja kwa utukufu mwingi, Yesu yuaja tena!

3. Itangazwe mahali po pote; Yesu yuaja tena!
Mwokozi aliye tufilia, Yesu yuaja tena!

4. Kuona machafuko twajua Yesu yuaja tena!
Mataifa ya kasiriana, Yesu yuaja tena!

5. Maradhi, hofu hutuhubiri Yesu yuaja tena!
Taabu, njaa hutulilia Yesu yuaja tena!

 

Comments
Print Friendly, PDF & Email