Danieli 3: Mwongozo wa Ibada.

February 11, 2021 in Mwongozo wa Ibada by TGVS

Danieli 3: Mwongozo wa ibada/ 27-BSG-3A, (Danieli 3:)/ Dhima: Ukombozi kutoka katika Tanuru la Moto/Wimbo: Guide me, O thou great Jehovah (SDAH 538).


 

Uchunguzi: Uradhi wa kustahimili Taabu, Maumivu, Mateso, Fedheha, Aibu, Mauti – (Ebr. 13:12–13; Yak. 1:2–4; 1 Pet 2:19–21, 22–25; 3:13–14; Ufu. 2:10).

Tafakari: “Mara ya mwisho tulipomsikia Mfalme Nebukadneza, kwa kweli alikuwa amevutiwa na uwezo wa Mungu wa Danieli katika kumwambia ndoto yake kuhusu sanamu kubwa yenye kichwa cha dhahabu. Hata alivutiwa zaidi kwa ufafanuzi husika: “Wewe (Nebukadneza) u kichwa kile cha dhahabu.” (2:38). Mfalme alikuwa amemwambia Danieli, “Hakika Mungu wenu ndiye Mungu wa miungu, na Bwana wa wafalme” (2:47). Kisha mfalme alikuwa amempandisha Danieli wadhifa awe mtawala juu ya jimbo lote la Babeli, makao makuu yakiwa katika maskani ya mfalme kwenye mji wa Babeli. Marafiki wa Danieli, Shadraka, Meshaki, na Abednego, wakawa watawala kwenye jimbo la Babeli (2:48–49). Hapa ndipo kisa hiki kuhusu marafiki wa Danieli huanzia. Ni miaka mingi baadaye. Ni bayana mfalme huyu alikuwa amesahau maungamo yake ya kuvutia, “Hakika Mungu wenu ndiye Mungu wa miungu, na Bwana wa wafalme” (2:47). Hatujui kama ulikuwa uzee au usahaulifu tu wa wazi, lakini kumbukumbu ya mfalme huyu ilikuwa duni.” [Sidney Greidanus, Preaching Christ from Daniel: Foundations for Expository Sermons, (Grand Rapids, MI; Cambridge, U.K.: William B. Eerdmans Publishing Company, 2012), 99–100].

Sasa, katika sura hii, mfalme ana wazo jipya kabisa—anatengeneza sanamu lote kwa dhahabu tupu, tofauti na lile kwenye ndoto yake. Hakuridhika na wazo kwamba ufalme mwingine ungechukua nafasi ya ufalme wake. Hivyo, kwa ukaidi, anatengeneza sanamu moja kubwa ya dhahabu. Hii ilikuwa kuonesha kwamba ufalme wake kamwe usingekuja kutwaliwa na mwingine, bali kwamba ungeendelea daima. Ilikuwa zaidi ishara ya ukaidi na uadi dhidi ya Mungu. Alikuwa akiuabudu ufalme wake mwenyewe na kujitukuza yeye binafsi kama kiongozi wake. Wapendwa, Mungu asingevumilia kiburi cha mfalme huyu; hivyo, aliingilia kati, kama ambavyo tutaona katika vipengele vingine kwenye Mwongozo huu wa Kujifunza.

Maana ya Kiibada: “Ndipo Nebukadreza akastaajabu, akainuka kwa haraka; akanena, akawaambia mawaziri wake, Je hatukutupa watu watatu, hali wamefungwa, katikati ya moto? Wakajibu, wakamwambia mfalme, Kweli, Ee mfalme. Akajibu, akasema, Tazama, mimi naona watu wanne, nao wamefunguliwa, wanatembea katikati ya moto hali hawana dhara; na sura yake yule wa nne ni mfano wa ‘mwana wa miungu.” (Daniel 3:24–25) Katika siku hii, Mungu alidhihirisha uwezo Wake usiokifani na kuwakomboa watoto Wake waaminifu!

“Kama ilivyo katika siku za Shadraka, Meshaki, na Abednego, ndivyo katika kipindi cha kufunga historia ya dunia, Bwana atenda kwa uwezo mkuu kwa niaba ya wale wanaoisimamia haki kwa uthabiti. Yule aliyetembea na mastahifu hawa wa Kiebrania kwenye tanuru la moto atakuwa pamoja na wafuasi Wake mahali popote walipo. Uwepo Wake wa kudumu utawafariji na kuwategemeza. Katikati ya wakati wa dhiki—dhiki ya namna ambayo haijawahi kutokea tangu limekuwepo taifa—wateule Wake watasimama bila kutikisika. Shetani pamoja na jeshi lake lote la uovu hawawezi kumwangamiza japo mdhaifu zaidi miongoni mwa watakatifu. Malaika wenye nguvu sharidi watawalinda, na kwa niaba yao Yehova atajidhihirisha kama “Mungu wa miungu,” mwenye uwezo wa kuokoa kabisa wale ambao wameweka dhamani yao Kwake.” (Prophets and Kings, uk. 2:513).

Sauti ya Injili: Sehemu hiyo imeandikwa kana kwamba Mungu anazungumza nawe moja kwa moja — kwa sababu Yeye anafanya hivyo. Bwana ananiambia nini asubuhi ya leo? Mwanangu, sura hii imejumuishwa kwenye Biblia ili kukuhakikishia kwamba Mimi ni Mungu jalali! Nina uwezo wa kukukomboa kutoka kwenye Tanuru liwakalo moto: tanuru la mambo magumu, maumivu, mateso, manyanyaso, aibu, au hata mauti. Wakati mwingine utakabiliwa na “majaribu ya moto.” Kwa juu juu inaweza kuonekana kwamba uko peke yako; lakini nataka kukuhakikishia kwamba “hauko peke yako!” (Isa. 43:2; Psa. 23:4). Uwepo Wangu utakuwa pamoja nawe—ili kukupatia amani, nguvu, na neema ya kustahimili! Katika saa hiyo muhimu ya majaribu, “simama imara kwa ajili ya kweli” Nami nitakutegemeza; na mwishowe, nitakupatia “taji ya uzima” (Ufu. 2:10). Je utadumu kuwa mwaminifu na kuzishikilia amri Zangu?

Shauku Yangu: Kwa neema ya Mungu nataka — 1. Kuepuka “kuitumikia miungu mingine” hata kama kukataa huko kunaweza kusababisha mauti; 2. Kumdhihirisha Kristo katika majaribu yangu–”hata kama akiniua,” bado “nitaithibitisha njia yangu mbele yake” (Ayubu 13:15, AMP); 3. Kumtii Mungu kwa kushika Amri Zake ikiwemo Sabato ya siku ya saba (cf. Ufu. 12:17; Ufu. 13:4, 6-8, 16-17).

Iweni na Siku Yenye Baraka: “Wapenzi, msione kuwa ni ajabu ule msiba ulio kati yenu, unaowapata kama moto ili kuwajaribu, kana kwamba ni kitu kigeni kiwapatacho. Lakini kama mnavyoyashiriki mateso ya Kristo, furahini; ili na katika ufunuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe.” (1 Petro 4:12–13)


 

Ibada Kupitia Uimbaji: Guide me, O thou great Jehovah (SDAH 538/ NK 156).

“UNIONGOZE, YEHOVA.”

1. Uniongoze, Yehova, Ni msafiri chini; Ni mnyonge, u hodari, ‘Nilinde kwa mkono: Unitunze, unilinde, Unionyeshe njia! Unionyeshe njia!

2. Na kisima cha uzima, Maji ya utabibu; Fungua kwa moyo wangu, Ninywe na kuponyeka! Uninyweshe, unilishe, Hata nimetosheka. Hata nimetosheka.

3. Wakati wa kuuvuka, Ule mto Yordani; Hofu yangu ufariji, ‘Nione uso wako: Nyimbo shangwe, Nyimbo shangwe, Nitaimba daima. Nitaimba daima.


 

MWISHO: Angalia Mwongozo wa Maombi katika kipengele kinachofuata/ Bwana Akubariki/

Comments
Print Friendly, PDF & Email