Danieli 5: Mwongozo wa Ibada

February 13, 2021 in Mwongozo wa Ibada by TGVS

Danieli 5: Mwongozo wa Ibada/ 27-BSG-5A, (Danieli 5:1-31)/ Dhima: Kuhesabiwa, Kupimwa, na Kukatawaliwa/ Wimbo: Hukumu Imeanzishwa (SDAH 416)


 

Uchunguzi: Anguko la Babeli (Danieli 5:1-31); Ubatili wa Sanamu/ Ibada ya Sanamu (Danieli 5:23, cf. Zab. 115:4-8; Hab. 2:18-19; Yer. 10:5, 15; 50:38; 51:17; Hab. 2:18).

Tafakari: Sura hii hujulikana vema kwa kirai – “Maandiko Ukutani.” Belshaza anaandaa “karamu kuu” wakati akiwaalika watu 1000 miongoni mwa watu wake mashuhuri. “Mivuto yote ambayo mali na mamlaka vingeweza kutiisha, viliongeza ufahari kwenye mandhari husika. Wanawake wazuri pamoja na vishawishi vyao ni miongoni mwa wageni waliohudhuria kwenye karamu hii ya kifalme. Watu farisi na wenye elimu walikuwepo. Wakuu na watawala walikunywa pombe kama maji na wakasherehekea chini ya ushawishi wake wa kutia wazimu.” (Prophets and Kings, uk. 523).

Mwenendo wa mfalme ni mwovu na mkaidi dhidi ya Yehova Mungu. Dhambi tatu mahususi zimebainishwa hapa – [a] Upujufu—karamu ya ulafi, ulevi na uasherati; [b] Usafihi—mfalme analinajisi Jina takatifu la Mungu na vitu vitakatifu vya Mungu wa Israeli, kwa kudai vikombe vilivyoletwa kutoka hekalu la Mungu viletwe na kutumiwa kwenye karamu isiyo takatifu; [c] Ibada ya Sanamu/Kufuru—mfalme na wageni wake wanaishangilia “miungu yao” ilhali wakinywa kutoka kwenye vikombe vilivyowakifishwa kwa Bwana. Ghafla, kiganja pweke kinaonekana “kikiandika ujumbe wa fumbo ukutani!” Wenye hekima hawawezi kuufafanua. Hatimaye, Danieli anaitwa ili kuufafanua. Ujumbe wa hukumu ukutani unafafanuliwa hivi: MENE, Mungu ameuhesabu ufalme wako na kuukomesha. TEKELI, umepimwa katika mizani nawe umeonekana kuwa umepunguka. PERESI, ufalme wako umegawanyika, nao wamepewa Wamedi na Waajemi.” (Danieli 5:26–28)

Maana ya Kiibada: “Katika usiku huo wa mwisho wa upuuzi wa wazimu, Belshaza na watumishi wake walikuwa wamejaza kipimo cha hatia yao na hatia ya ufalme wa Wakaldayo. Isingewezekana tena mkono wa Mungu wa kizuizi kuepushia mbali janga lililokuwa limekaribia. Kupitia kudra nyingi, Mungu alikuwa ametafuta kuwafundisha ustahivi kwa sheria Yake. “Tungependa kuuponya Babeli,” alitangaza kuhusu wale ambao hukumu yao sasa ilikuwa imefika mbinguni, “lakini haukuponyeka.” Yeremia 51:9. Kwa sababu ya upotovu wa kutisha wa moyo wa mwanadamu, mwishowe Mungu aliona vema kupitisha hukumu isiyobadilika. Belshaza angepaswa kuanguka, na ufalme wake ulisalimishwa kwenye mikono mingine.” (Prophets and Kings, uk. 530). Belshaza alikuwa “Tekeli” – “Umepimwa kwenye mizani, na imebainika umepungua!’ —Usiku huohuo Belshaza, mfalme wa Wakaldayo, akauawa. Na Dario, Mmedi, akaupokea ufalme, naye umri wake alikuwa na miaka sitini na miwili.” (Danieli 5:30–31)

Sauti ya Injili: Sehemu hiyo imeandikwa kana kwamba Mungu anazungumza nawe moja kwa moja — kwa sababu Yeye anafanya hivyo. Bwana ananiambia nini asubuhi ya leo? Mwanangu, watu wenye kiburi, wakaidi na watafuta-anasa za ulimwengu huu watakumbana na hukumu. Belshaza alikuwa amelisahau Neno Langu: hakujifunza kutokana na historia (kutoka kwa watangulizi wake). Aidha, alilinajisi Jina Langu takatifu na dhambi hiyo ilimgharimu ufalme wake na maisha yake hasa! Je utajifunza kutokana na historia? Je utajifunza kuzitii Amri Zangu, Maagizo Yangu, Neno Langu? Mwanangu, hivi karibuni Hukumu itawashukia –(Nah 1:6; Yer. 4:4; Mat 25:41; Ufu. 20:15; 21:8) — “watoto wote wa uasi” (Kol. 3:6). Je utazingatia “maandishi ukutani?” Je utasoma “alama za nyakati” (Luka 21; Mt 24) na kuwa tayari kwa ajili ya Kristo Yesu? Je utatubu ili uokolewe?

Shauku Yangu: Kwa neema ya Mungu, nataka kuheshimu Mungu kwa –1. Kuendelea kutii Amri, Maagizo, na Neno Lake; 2. Kuliheshimu Jina Lake takatifu; 3. Kumwomba Bwana anisamehe dhambi zangu, ili nisiweze kukutwa nikiwa “nimepungua” katika hukumu ya BWANA (1 Pet 4:17); 4. Kuwaelekeza upya watu wa ulimwengu huu watazame “Alama za Wakati,” na hivyo kujiandaa kwa ajili ya Ujio wa Pili wa Yesu.

Iweni na Siku Yenye Baraka: 11 Naam, tukiujua wakati, kwamba saa ya kuamka katika usingizi imekwisha kuwadia; kwa maana sasa wokovu wetu u karibu nasi kuliko tulipoanza kuamini. 12 Usiku umeendelea sana, mchana umekaribia, basi, na tuyavue matendo ya giza, na kuzivaa silaha za nuru. 13 Kama ilivyohusika na mchana na tuenende kwa adabu; si kwa ulafi na ulevi, si kwa ufisadi na uasherati, si kwa ugomvi na wivu. 14 Bali mvaeni Bwana Yesu Kristo, wala msiuangalie mwili, hata kuwasha tamaa zake. (Warumi 13:11-14)


 

Ibada Kupitia Uimbaji: Imeanzishwa Hukumu (NK 171)

“THE JUDGMENT HAS SET.”

1. Imeanzishwa hukumu mbinguni; Tutasimamaje pale; Apomapo Mungu hakimu kula wazo na tendo?

[Kibwagizo]: Tutasimamaje sote katika siku kuu ile? Dhambi zitu zitafutika ama zitatuangusha?

2. Wametangulia wafu kupimwa, Kitambo ndipo wahai; Watapokea neno la mwisho, Vitabuni mwa Mungu.

3. Tutasimamaje usiku ule, Siri zetu, kila moja; Zafunuliwa toka vitabu; Yesu atusaidie!

 

Comments
Print Friendly, PDF & Email