Mathayo 1: Ibada

April 25, 2021 in Mwongozo wa Ibada by TGVS

Mathayo 1: Mwongozo wa Ibada/ 40-BSG-1A, (Mathayo 1:18-25)/ Dhima: Kristo – Mwanadamu kamili, Mungu kamili/ Wimbo: “Live out Thy life within me” (SDAH 316).


 

Uchunguzi: Nasaba ya Yesu Kristo — (Mwa. 5:1–32; 11:10–26; Ruthu 4:18–22; 1 Nya. 1:1–4, 24–27, 34; 2:1–15; Mat. 1:2–17; Luka 3:23-38); Kuzaliwa kwa Yesu (Mat. 1:18-25; Luka 1:26-28; 2:1-7)

Tafakari: Sehemu ya kwanza ya sura hii inahusika na Nasaba ya Yesu Kristo. Sehemu ya pili hujadili kifupi kuhusu kuzaliwa kwa Yesu. Katika Mat. 1:18, Yusufu anafadhaika, akidhani kwamba Mariamu (mkewe mtarajiwa mjamzito) hakuwa mwaminifu. Bila kutaka kumwaibisha, anakusudia kuvunja uchumba wao kwa siri (v. 19). Katika ndoto, Yusufu anahakikishiwa tena kwamba ujauzito wa Mariamu umesababishwa na Roho Mtakatifu (v. 20). Malaika wanamwambia Yusufu kwamba Mariamu atamzaa Mwana ambaye watamwita jina Lake “Yesu” (v. 21). Mwana huyu, ambaye mimba Yake ilitungwa bila baba mwanadamu, ni utimizo wa unabii wa Isaya (Isa. 7:14). Fasili mbili za mwisho kuhusu Ndoa zinazofuata ndoto husika: Yusufu anamchukua Mariamu kuwa mkewe (vv. 24-25).

Maana ya Kiibada:“Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama Yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu.” (Mathayo 1:18)

“Kwa nini kuzaliwa kwa njia ya bikra ni muhimu kwa imani ya Mkristo? Yesu Kristo, Mwana wa Mungu, alikuwa awe huru dhidi ya asili ya dhambi iliyoritishwa kwa wanadamu wengine wote. Kwa sababu Yesu alizaliuwa na mwanamke, alikuwa mwanadamu; lakini akiwa kama Mwana wa Mungu, Yesu alizaliwa pasipo chembe yoyote ya dhambi. Yesu anazaliwa akiwa mwanadamu kamili na Mungu kamili. Mungu halida, asiye na ukomo alitwaa mapungufu ya ubinadamu ili aweze kuishi na kufa kwa ajili ya wokovu wa wote wamwaminio Yeye.

Kwa sababu Yesu aliishi kama mwanadamu, tunajua kwamba anaelewa kikamilifu dhahama na mapambano yetu (Waebrania/ 4:15–16). Kwa sababu Yeye ni Mungu, anayo uweza na mamlaka ya kutukomboa kutoka dhambini (Wakolosai 2:13–15). Tunaweza kumwambia Yesu mawazo yetu, hisia zetu, na mahitaji yetu. Amekuwa mahali tulipo sasa, Naye ana uwezo wa kusaidia.” [Bruce B. Barton, Matthew, Life Application Bible Commentary, (Wheaton, IL: Tyndale House Publishers, 1996), 15].

Sauti ya Injili: Sehemu hiyo imeandikwa kana kwamba Mungu anazungumza nawe moja kwa moja — kwa sababu Yeye anafanya hivyo. Bwana ananiambia nini asubuhi ya leo? Mwanangu, miaka zaidi ya 4000 kabla Kristo hajazaliwa huko Bethlehemu, nilikuwa na mpango wa kukuokoa wewe (Mwa. 3:15). Kristo alikuja ili kukufikia wewe: kufa kwa ajili yako Msalabani ili uweze kupata uzima wa milele (Yohana 3:16-17). Kwa sababu ya mauti ya Kristo, sasa unayo fursa ya kukiendea kiti cha enzi cha Mungu, ambako “kila baraka ya kiroko” iko katika Kristo, hata “uzima wa milele.” Lakini kwanza, lazima utubu dhambi zako. Je utafanya hivyo?

Shauku Yangu: Kwa neema ya Mungu, nataka – 1. Kuomba nizaliwe kwa Roho Mtakatifu (Mat 1:18); 2. Niwe na tabia sawa na ile ya Yusufu: haki (Mat 1:19); 3. Kuepuka mahusiano ya kimapenzi kabla ya ndoa (Mat 1:18-19, 25); 4. Kusikiliza, kutii, na kufuata amri/maelekezo ya Bwana (Mt 1:20); 5. Kuamini katika BWANA Yesu Kristo na wokovu aliyotimiza kwa ajili yangu pale kwenye Msalaba wa Kalvari; 6. Kumshukuru Mungu kwa ajili ya ahadi ya uwepo Wake pamoja nami: “Imanueli” (Mat 1:23).

Iweni na Siku Yenye Baraka: “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo (nguvu, fursa, haki) wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio (wanaolifuata, wanaolidhamani, na kulitegemea) jina Lake.” (Yohana 1:12, AMP)


 

Ibada Kupitia Uimbaji: “Live out Thy life within me” (SDAH 316) – “Uishi Ndani Yangu” (NK # 147)

  1. Tawala ndani yangu, Ee Yesu, Mfalme; Uwe kwangu majibu kwa maswali yangu; Uishi ndani yangu, Wewe, mwongozi; Utumishi ni wangu, Wako utukufu.
  2. Hekalu nimetoa, Umelisafisha; Sasa fahari yako Imulike ndani; Dunia iwe kumya, mwili sasa uwe; Mtumwa mtulivu Wa kukutii tu.
  3. Viungo vyake mwili, Vyote vikungoja; Tayari vikuutwa Kwenda, kusimama; Bila manumguniko au malaumu; Au kusumbuliwa, Pasipo majuto.
  4. Niwe na utulivu pasipo haraka; Tayari kungojea maagizo yako; Tawala ndani yangu, Ee Yesu, Mfalme; Uwe kwanfgu majibu kwa maswali yote.

 

Mwisho: Kutakuwa na Mwongozo wa Ibada ya Maombi katika kipengele kinachofuata (40-BSG-1B). Bwana Akubariki!

Comments
Print Friendly, PDF & Email