Walawi 18: Maswali ya Kujadili

May 1, 2022 in Mwongozo wa Biblia by TGVS

Mwongozo wa Kujifunza Biblia/ Walawi 18, (3-BSG-18K)/ Maswali ya kuzingatia wakati ukichunguza sura hii kwa kina zaidi.

 


Tafakari na Kujadili – [1] Kwa mujibu wa Walawi 18, familia ya karibu (mahusiano ya mwili: wazazi, mama wa kambo, dada, wajukuu, dada wa kambo, shangazi, mkamwana, na shemeji)—wamezuiliwa kuwa wenzi wa kimapenzi. Je, makatazo haya bado yanawabana watu hadi leo? Unaweza kumwambia nini mtu fulani anayedai kwamba hizi zilikuwa sheria za AK? Ni Maandiko gani ya Agano Jipya unayoweza kutumia kupinga hoja zao?

[2] Shetani amefaulu katika kupindisha na kupotosha mahusiano ya kimapenzi kwa kuondoa yale mema na sahihi (mapenzi kati ya mume na mke) na badala yake ameweka tamaa, ponografia, uzinzi, ubakaji na ushoga. Jinsi gani unaweza kumsaidia mtu anayepambana na ponografia?

[3] Kuilinda Nyumba ya Mungu: Ni hatua gani zinazopaswa kuchukuliwa leo kwenye nyumba za Kikristo ili kuhakikisha kwamba watoto wanaolelewa katika nyumba hizo hawaangukii kwenye mtego wa Ibilisi? Nini huchochea tamaa, ubakaji na mapenzi haramu? Tunawezaje kujilinda wenyewe vilivyo dhidi ya dhambi hizi, tukijua kwamba miili yetu ni “mahekalu” anamostakimu Roho wa Mungu?

[4] Kwa mujibu wa BWANA, ushoga ni chukizo: kirihifu, upotovu, udhia, uchusho (toebah, Law. 18:22). Kwa nini hivyo?

[5] Waisraeli waliposhindwa kufuata maagizo ya Mungu yaliyo wazi na badala yake wakakubali mtindo wa maisha wa mataifa ya kipagani yaliyowazunguka, wakafifisha hasa matokeo ya ushuhuda wao. Leo, makanisa mengi yamefikiri kwa kujidanganya kwamba lazima wauige ulimwengu ili kuufikishia injili! Kama ungekuwa kwenye nafasi ya uongozi kwenye kanisa lako mahalia, ungezungumziaje suala hili?

Kwa Usomaji Zaidi – [6] Sura hii inazungumzia mahusiano mengi pujufu – uwakifishaji au kuwatoa kafara watoto kwa Moleki (Law. 18:21). Moleki ni nini? Na ni mambo gani muhimu tunayojifunza leo hapa?

Kuchunguza kwa Kina Zaidi – [7] Jinsi gani Agano Jipya linaakisi mafundisho ya Walawi 18? Bainisha aya mahususi kisha jadili zaidi.

Kwa ajili ya Kujitathmini – [8] Dhambi (dhambi zote) huifanya nyumba ya Mungu kuwa najisi, na kumfukuza atoke nyumbani Mwake (Isa. 59:1-2). Je, umetumia muda wa kuyachunguza maisha yako kuhusu dhambi (masuala) mahususi ambayo pengine hukutengana na BWANA?

Kwa Ajili ya Maisha ya Leo – [9] Kuwalea watoto katika karne hii ya 21 ni jambo la kufadhaisha na lenye changamoto sana. Mtoto wa rika la balehe anaweza kukwambia, “hii ni nchi huru,” au “nitafanya kile ninachotaka kufanya,” au “achana nami!” Ukiwa mzazi mtauwa, unapaswa kuitikiaje? Je, unawaruhusu wafuate njia yao mbaya (chaguzi, marafiki, mahusiano), na hivyo kuwaruhusu waendelee katika dhambi zao na kuvuna matokeo ya kusikitisha?

Umuhimu kwa Mtu Binafsi – [10] Mungu alishuka ili kuangamiza Sodoma na Gomora kwa ajili ya machukizo yao (Mwa. 19). Hivi karibuni, BWANA atashuka tena ili kuuangamiza ulimwengu huu kwa ajili ya dhambi zake—(dhambi & machukizo ambayo hayakufanyiwa toba). Jinsi gani unaweza kuitumia sura hii ili kufanya mkutano mkuu wa injili juu ya dhambi zilizoorodheshwa hapa na hitaji la haraka la “watu wote” Kutubu, “Kuiandaa njia ya BWANA, na Kuyanyoosha mapito Yake?” (Mat 3:3)


 

[11] Ni hatua gani unazoweza kupanga kuchukua ili kuitikia yale ambayo umejifunza hadi kufikia sasa? Kumbuka: Lengo kuu la Somo lolote la Biblia linapaswa kuwa maisha yaliyobadilika, si maarifa ya kiakili tu, kupata taarifa zaidi.

Comments
Print Friendly, PDF & Email