{"id":1830,"date":"2022-02-19T22:48:55","date_gmt":"2022-02-20T02:48:55","guid":{"rendered":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/?p=1830"},"modified":"2022-02-19T22:48:55","modified_gmt":"2022-02-20T02:48:55","slug":"dhambi-ya-yuda-na-tamari","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/archives\/1830","title":{"rendered":"Dhambi ya Yuda na Tamari"},"content":{"rendered":"<p><em>Mwanzo 38: <strong>Mwongozo wa Ibada<\/strong>\/ 1-BSG-38A, (Mwanzo 38:1-30)\/ <strong>Dhima<\/strong>: Dhambi ya Yuda na Tamari\/ <strong>Wimbo:<\/strong> Katika Wenye Dhambi (NK 121)<\/em><\/p>\n<hr \/>\n<p>&nbsp;<\/p>\n<p><span style=\"color: #ff00ff;\"><strong>Uchunguzi<\/strong>:<\/span> Fimbo ya enzi haitaondoka Yuda \u2013 (Mwa. 49:10; 2 Sam 2:4; 1 Nya. 5:2; Zab. 60:7; Mik. 5:2; Mat 1:1-2, 3; Mat 2:6; Ebr. 7:14; Ufu. 5:5).<\/p>\n<p><span style=\"color: #ff00ff;\"><strong>Tafakari<\/strong>:<\/span> Sura hii inawasilisha maelezo ya kisa cha Yuda na familia yake. Yuda, mwana wa nne wa Yakobo kwa Lea (Mwa. 29:35), alichukua nafasi kubwa miongoni mwa ndugu zake mapema maishani (Mwa. 37:26, 27; 43:3-10; 44:16-34; 46:28). Sura hii pia inafafanua mwenendo pujufu wa Yuda: uasi, uasherati, na unafiki. Hebu tuangalie uzembe na dhambi za Yuda: <u>Kwanza<\/u>, Yuda aliondoka nyumbani akaacha ushawishi wa baba yake mcha-Mungu (v. 1). <u>Pili<\/u>, alimwoa Shua, mke Mkanaani\/asiye muumini. Hii ilikuwa kinyume na mapenzi ya Mungu (1\u20132). Tatu, Yuda aliwalea watoto katika mazingira maovu; aliwapata wana watatu kupitia mkewe: Eri, Onani, na Shela (3\u201310). <u>Nne<\/u>, Yuda alikuwa kipofu kiroho: hakuweza kumwona Mungu akiwa kazini (v. 11). <u>Tano<\/u>, Yuda alifanya dhambi ya uasherati (12\u201319). <u>Sita<\/u>, Yuda hakuona haya kutenda dhambi miongoni mwa marafiki zake (20\u201321). <u>Saba<\/u>, Yuda alikuwa na maadili yaliyopotoka: alijishughulisha na mwonekano wake hadharani lakini hakujali sheria ya Mungu (22\u201323). <u>Nane<\/u>, Yuda alimhukumu Tamari: alikuwa mwepesi kuwahukumu wengine kwa ukali, lakini mzito kujihukumu mwenyewe (24\u201325); <u>Tisa<\/u>, Yuda alitubu, lakini kwa sehemu tu (26).<\/p>\n<p>Hatimaye, Mungu aliingilia kati na kuibatilisha dhambi na aibu ya Yuda\u2014Tamari alizaa mapacha (Peresi &amp; Zera) ambao hatimaye wangekuwa waumini wa kweli (27\u201330). Peresi, aliyetoka tumboni kwanza, alihesabiwa kuwa mzaliwa wa kwanza (Hes. 26:20). Peresi alikuwa akraba wa Mfalme Daudi (Ruthu 4:18\u201322) na hivyo akraba wa Yesu Kristo (Mat. 1:1).<\/p>\n<p><span style=\"color: #ff00ff;\"><strong>Maana ya Kiibada<\/strong>:<\/span> Kwa nini sura hii, kisa hiki chenye giza la uchafu, kimejumuishwa katika Biblia? Kwa nini kuwakfisha sura nzima kwa ajili ya Yuda? Yuda anahesabiwa kama mkuu mojawapo ya makabila 12 ya Israeli \u2013 \u201cKabila la Yuda.\u201d Kwenye Biblia, kabila la Yuda ni la maana sana kwa sababu ni kabila la kifalme ambamo Masihi angetokea (Mwa. 49:10). Kwa hiyo, chochote kinachohusiana na Yuda ni muhimu kwa mpango wa wokovu. Ndoa ya Yuda kwa Shua Mkanaani na uhusiano wake wa kimapenzi baadaye na mkamwana wake, Tamari, hufanya sura hii inuke. Wazo kuu ni hili: Masihi hakutoka katika ukoo wa watu watakatifu au masharifu (Yn. 8:41). Yuda na wanawe walitenda kwa namna iliyomchukiza Mungu. Akraba wa kibinadamu wa Yesu walikuwa wadhambi. Lakini Bwana asifiwe kwamba Yesu alikuja duniani kuokoa wadhambi (Mat 1:21). Sisi sote tunanuka mbele za Mungu aliye mtakatifu, lakini ni kupitia Kristo pekee ndipo tunaweza kukaribishwa tena katika familia ya Mungu. Amina?<\/p>\n<p><strong><span style=\"color: #ff00ff;\">Sauti ya Injili:<\/span> <\/strong>Sehemu hiyo imeandikwa kana kwamba Mungu anazungumza nawe moja kwa moja \u2014 kwa sababu Yeye anafanya hivyo. Bwana ananiambia nini asubuhi ya leo? Mwanangu, Biblia haifichi ukweli kwamba Yesu alitoka katika ukoo wa kibinadamu mchafu sana, mnajisi sana, na mdhambi sana, ule wa Yuda (Yn. 8:41). Lakini licha ya udhaifu wake aliourithi, kumbukumbu iko wazi kwamba Yesu alinidhamani Mimi (Yn. 8:29) na kamwe hakutenda dhambi (Yn. 19:4; 1 Yn. 3:5; 1 Pet 2:22; Ebr. 1:9; 4:15). Wewe, pia, unaweza kunidhamani Mimi na kuishi maisha matakatifu. Habari njema ni kwamba nitakupa rasilimali za kiungu ili uweze kufanya hivyo. Swali pekee ni hili: Hivi uko tayari? Je, unaweza kunikabidhi Mimi maisha yako? Je, utafuata mfano wa Yesu?<\/p>\n<p><strong><span style=\"color: #ff00ff;\">Shauku Yangu:<\/span> <\/strong>Kwa neema ya Mungu, nataka kutubu dhambi zilizoorodheshwa katika sura hii (angalia Mwongozo wa Maombi). Nataka kumshukuru Mungu kwa kunijumuisha mimi (mdhambi) katika familia Yake. Nataka kujitahidi kuufikia utakatifu na kujiweka tayari kwa Ujio wa Pili.<\/p>\n<p><span style=\"color: #ff00ff;\"><strong>Uwe na Siku Yenye Baraka<\/strong>:<\/span> \u201cKwa sababu ndio mlioitiwa; maana Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, <u>akawaachia kielelezo<\/u>, mfuate nyayo Zake. Yeye hakutenda dhambi, wala hila haikuonekana kinywani Mwake.\u201d (1 Petro 2:21\u201322)<\/p>\n<div class='share-to-whatsapp-wrapper'><div class='share-on-whsp'>Share on: <\/div><a data-text='Dhambi ya Yuda na Tamari' data-link='https:\/\/tgvs.org\/injili\/archives\/1830' class='whatsapp-button whatsapp-share'>WhatsApp<\/a><div class='clear '><\/div><\/div>","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Mwanzo 38: Mwongozo wa Ibada\/ 1-BSG-38A, (Mwanzo 38:1-30)\/ Dhima: Dhambi ya Yuda na Tamari\/ Wimbo: Katika Wenye Dhambi (NK 121) &nbsp; Uchunguzi: Fimbo ya enzi haitaondoka Yuda \u2013 (Mwa. 49:10; 2 Sam 2:4; 1 Nya. 5:2; Zab. 60:7; Mik. 5:2; Mat 1:1-2, 3; Mat 2:6; Ebr. 7:14; Ufu. 5:5). Tafakari: Sura hii inawasilisha maelezo ya <a class=\"read-more-link\" href=\"https:\/\/tgvs.org\/injili\/archives\/1830\"><br \/>&#8230;read more<\/a><\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":1561,"comment_status":"closed","ping_status":"closed","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"om_disable_all_campaigns":false,"_monsterinsights_skip_tracking":false,"_monsterinsights_sitenote_active":false,"_monsterinsights_sitenote_note":"","_monsterinsights_sitenote_category":0,"footnotes":""},"categories":[15],"tags":[],"class_list":["post-1830","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-mwongozo-wa-ibada"],"jetpack_featured_media_url":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-content\/uploads\/2020\/10\/Default-Featured-Image-2020.jpg","_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/1830","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=1830"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/1830\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":1831,"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/1830\/revisions\/1831"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/media\/1561"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=1830"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=1830"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=1830"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}