{"id":1860,"date":"2022-03-02T23:14:04","date_gmt":"2022-03-03T03:14:04","guid":{"rendered":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/?p=1860"},"modified":"2022-03-04T23:16:45","modified_gmt":"2022-03-05T03:16:45","slug":"mwanzo-48-usomaji-wa-biblia","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/archives\/1860","title":{"rendered":"Mwanzo 48: Usomaji wa Biblia"},"content":{"rendered":"<p><strong>Mwanzo 48:<\/strong><\/p>\n<p><strong>\u00a0<\/strong><\/p>\n<hr \/>\n<p><span style=\"color: #003366;\"><strong><em>1 <\/em><\/strong>Ikawa, baada ya mambo hayo, Yusufu akaambiwa, Tazama, baba yako hawezi; akawatwaa wanawe wawili, Manase na Efraimu, pamoja naye.<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #003366;\"> <strong><em><sup>2\u00a0<\/sup><\/em><\/strong>Naye akaarifiwa Yakobo ya kwamba, Angalia, mwanao Yusufu anakuja kwako. Israeli akajitia nguvu, akaketi juu ya kitanda.<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #003366;\"> <strong><em><sup>3\u00a0<\/sup><\/em><\/strong>Yakobo akamwambia Yusufu, Mungu Mwenyezi alinitokea huko Luzu, katika nchi ya Kanaani, akanibariki,<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #003366;\"> <strong><em><sup>4\u00a0<\/sup><\/em><\/strong>akaniambia, Mimi hapa, nitakuongezea uzao wako, na kukuzidisha, nami nitakufanya uwe kundi la mataifa; kisha nitawapa wazao wako nchi hii baada yako, iwe milki ya milele.<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #003366;\"> <strong><em><sup>5\u00a0<\/sup><\/em><\/strong>Basi sasa wanao wawili uliozaliwa katika nchi ya Misri kabla sijaja kwako Misri ni watoto wangu, yaani, Efraimu na Manase watakuwa wangu, kama Reubeni na Simeoni.<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #003366;\"> <strong><em><sup>6\u00a0<\/sup><\/em><\/strong>Na wazao wako utakaozaa baada ya hawa watakuwa wako; kwa jina la ndugu zao wataitwa katika urithi wao.<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #003366;\"> <strong><em><sup>7\u00a0<\/sup><\/em><\/strong>Na mimi nilipokuja kutoka Padan, Raheli akanifia katika nchi ya Kanaani, njiani, si mwendo mkubwa kabla ya kufika Efrathi. Nikamzika katika njia ya Efrathi, ndio Bethlehemu.<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #003366;\"> <strong><em><sup>8\u00a0<\/sup><\/em><\/strong>Israeli akawaona wana wa Yusufu, akasema, Ni nani hawa?<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #003366;\"> <strong><em><sup>9\u00a0<\/sup><\/em><\/strong>Yusufu akamwambia babaye, Hawa ni wanangu, Mungu alionipa hapa. Akasema, Tafadhali uwalete kwangu nami nitawabariki.<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #003366;\"> <strong><em><sup>10\u00a0<\/sup><\/em><\/strong>Na macho ya Israeli yalikuwa mazito kwa uzee, wala hakuweza kuona. Akawaleta kwake, naye akawabusu, na kuwakumbatia.<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #003366;\"> <strong><em><sup>11\u00a0<\/sup><\/em><\/strong>Israeli akamwambia Yusufu, Sikudhani ya kwamba nitakuona uso wako, na Mungu amenionyesha na uzao wako pia.<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #003366;\"> <strong><em><sup>12\u00a0<\/sup><\/em><\/strong>Yusufu akawatoa katika magoti yake, naye akainama kifudifudi<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #003366;\"> <strong><em><sup>13\u00a0<\/sup><\/em><\/strong>Yusufu akawaweka wote wawili, Efraimu katika mkono wake wa kuume, kuelekea mkono wa kushoto wa Israeli; na Manase katika mkono wake wa kushoto, kuelekea mkono wa kuume wa Israeli, akawasogeza karibu naye.<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #003366;\"> <strong><em><sup>14\u00a0<\/sup><\/em><\/strong>Israeli akanyosha mkono wake wa kuume akauweka juu ya kichwa cha Efraimu, aliyekuwa mdogo, na mkono wake wa kushoto akauweka juu ya kichwa cha Manase, huku akijua atiavyo mikono; maana Manase ndiye aliyezaliwa kwanza.<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #003366;\"> <strong><em><sup>15\u00a0<\/sup><\/em><\/strong>Akambariki Yusufu, akasema, Mungu ambaye baba zangu, Ibrahimu na Isaka, walienenda mbele zake, yeye Mungu aliyenilisha, maisha yangu yote, hata siku hii ya leo,<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #003366;\"> <strong><em><sup>16\u00a0<\/sup><\/em><\/strong>naye Malaika aliyeniokoa na maovu yote, na awabariki vijana hawa; jina langu na litajwe juu yao, na jina la baba zangu, Ibrahimu na Isaka; na wawe wingi wa watu kati ya nchi.<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #003366;\"> <strong><em><sup>17\u00a0<\/sup><\/em><\/strong>Yusufu alipoona kwamba babaye anaweka mkono wake wa kuume juu ya kichwa cha Efraimu, ikawa vibaya machoni pake. Akauinua mkono wa babaye auondoe katika kichwa cha Efraimu, ili auweke juu ya kichwa cha Manase.<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #003366;\"> <strong><em><sup>18\u00a0<\/sup><\/em><\/strong>Yusufu akamwambia babaye, Sivyo, babangu, maana huyu ni mzaliwa wa kwanza; weka mkono wako wa kuume kichwani pake.<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #003366;\"> <strong><em><sup>19\u00a0<\/sup><\/em><\/strong>Babaye akakataa, akasema, Najua, mwanangu najua, yeye naye atakuwa taifa, yeye naye atakuwa mkuu; lakini ndugu yake mdogo atakuwa mkubwa kuliko yeye, na uzao wake watakuwa wingi wa mataifa.<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #003366;\"> <strong><em><sup>20\u00a0<\/sup><\/em><\/strong>Akawabariki siku ile akasema, Katika ninyi Waisraeli watabariki, wakisema, Mungu na akufanye kama Efraimu na Manase. Akamweka Efraimu mbele ya Manase.<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #003366;\"> <strong><em><sup>21\u00a0<\/sup><\/em><\/strong>Israeli akamwambia Yusufu, Angalia, mimi ninakufa, lakini Mungu atakuwa pamoja nanyi, naye atawarudisha mpaka nchi ya baba zenu.<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #003366;\"> <strong><em><sup>22\u00a0<\/sup><\/em><\/strong>Nami nimekupa wewe sehemu moja zaidi kuliko ndugu zako, niliyoitwaa katika mikono ya Waamori, kwa upanga wangu na upinde wangu.<\/span><\/p>\n<p>&nbsp;<\/p>\n<p><strong>MASWALI YA KUJADILI:<\/strong><\/p>\n<hr \/>\n<p>1. Yusufu anaposikia baba yake anakaribia kufa anapeleka watoto wake ili wabarikiwe. Unafanya jitihada gani kupata baraka za wazazi wako kabla hawajafa?<\/p>\n<p>2. Wazee wenye umri na wenye kuijua vyema historia ya tulikotoka ni hazina. Kizazi cha sasa kinafanya jitihada kupata hazina hiyo sasa kabla haijatoweka kabisa?<\/p>\n<p>3. Efraimu na Manase watoto wa Yusufu waliingizwa katika orodha ya watoto wa Yakobo ili kukamilisha idadi ya kabila 12 za Israeli. Unadhani ni kwa nini Yakobo alifanya hivyo?<\/p>\n<p>4. Kwa nini Yusufu alitaka kuingilia kati utowaji wa mibaraka ya baba yake kwa watoto wake Efraimu na Manase?<\/p>\n<p>5. Unadhani ni kwa nini Yakobo alikumbusha tukio la kufiwa Raheli kwa mwanae Yusufu? Hii inaonesha jinsi alivyompenda Raheli na jinsi kifo hicho kilivyomwachia jeraha la kudumu?<\/p>\n<div class='share-to-whatsapp-wrapper'><div class='share-on-whsp'>Share on: <\/div><a data-text='Mwanzo 48: Usomaji wa Biblia' data-link='https:\/\/tgvs.org\/injili\/archives\/1860' class='whatsapp-button whatsapp-share'>WhatsApp<\/a><div class='clear '><\/div><\/div>","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Mwanzo 48: \u00a0 1 Ikawa, baada ya mambo hayo, Yusufu akaambiwa, Tazama, baba yako hawezi; akawatwaa wanawe wawili, Manase na Efraimu, pamoja naye. 2\u00a0Naye akaarifiwa Yakobo ya kwamba, Angalia, mwanao Yusufu anakuja kwako. Israeli akajitia nguvu, akaketi juu ya kitanda. 3\u00a0Yakobo akamwambia Yusufu, Mungu Mwenyezi alinitokea huko Luzu, katika nchi ya Kanaani, akanibariki, 4\u00a0akaniambia, Mimi <a class=\"read-more-link\" href=\"https:\/\/tgvs.org\/injili\/archives\/1860\"><br \/>&#8230;read more<\/a><\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":1561,"comment_status":"closed","ping_status":"closed","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"om_disable_all_campaigns":false,"_monsterinsights_skip_tracking":false,"_monsterinsights_sitenote_active":false,"_monsterinsights_sitenote_note":"","_monsterinsights_sitenote_category":0,"footnotes":""},"categories":[23],"tags":[],"class_list":["post-1860","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-usomaji-vidokezo"],"jetpack_featured_media_url":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-content\/uploads\/2020\/10\/Default-Featured-Image-2020.jpg","_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/1860","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=1860"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/1860\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":1861,"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/1860\/revisions\/1861"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/media\/1561"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=1860"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=1860"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=1860"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}