{"id":1862,"date":"2022-03-03T23:17:01","date_gmt":"2022-03-04T03:17:01","guid":{"rendered":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/?p=1862"},"modified":"2022-03-04T23:19:34","modified_gmt":"2022-03-05T03:19:34","slug":"mwanzo-49-usomaji-wa-biblia","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/archives\/1862","title":{"rendered":"Mwanzo 49: Usomaji wa Biblia"},"content":{"rendered":"<p><strong>Mwanzo 49:<\/strong><\/p>\n<p><strong>\u00a0<\/strong><\/p>\n<hr \/>\n<p><span style=\"color: #003366;\"><strong><em>1 <\/em><\/strong>Yakobo akawaita wanawe, akasema, Kusanyikeni, ili niwaambie yatakayowapata siku za mwisho.<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #003366;\"> <strong><em><sup>2\u00a0<\/sup><\/em><\/strong>Kusanyikeni, msikie, enyi wana wa Yakobo, Msikilizeni Israeli, baba yenu.<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #003366;\"> <strong><em><sup>3\u00a0<\/sup><\/em><\/strong>Reubeni, u mzaliwa wangu wa kwanza, Nguvu zangu, na malimbuko ya uwezo wangu. Umewapita wengine kwa ukuu na kwa nguvu.<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #003366;\"> <strong><em><sup>4\u00a0<\/sup><\/em><\/strong>Umeruka mpaka kama maji, basi usiwe na ukuu, Kwa sababu ulikipanda kitanda cha baba yako, Ukakitia unajisi; alikipandia kitanda changu.<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #003366;\"> <strong><em><sup>5\u00a0<\/sup><\/em><\/strong>Simeoni na Lawi ni ndugu; Panga zao ni silaha za jeuri.<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #003366;\"> <strong><em><sup>6\u00a0<\/sup><\/em><\/strong>Nafsi yangu, usiingie katika siri yao, Fahari yangu usiungane na kusanyiko lao, Maana katika ghadhabu yao walimuua mtu, Na kwa ukaidi wao walikata mshipa wa ng&#8217;ombe;<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #003366;\"> <strong><em><sup>7\u00a0<\/sup><\/em><\/strong>Ghadhabu yao na ilaaniwe, maana ilikuwa kali, Na hasira yao, maana ilikuwa haina huruma. Nitawagawa katika Yakobo, Nitawatawanya katika Israeli.<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #003366;\"> <strong><em><sup>8\u00a0<\/sup><\/em><\/strong>Yuda, ndugu zako watakusifu, Mkono wako utakuwa shingoni mwa adui zako. Wana wa baba yako watakuinamia.<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #003366;\"> <strong><em><sup>9\u00a0<\/sup><\/em><\/strong>Yuda ni mwana-simba, Kutoka katika mawindo, mwanangu, umepanda; Aliinama akajilaza kama simba, Na kama simba mke; ni nani atakaye mwamsha?<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #003366;\"> <strong><em><sup>10\u00a0<\/sup><\/em><\/strong>Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, Wala mfanya sheria kati ya miguu yake, Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki, Ambaye mataifa watamtii.<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #003366;\"> <strong><em><sup>11\u00a0<\/sup><\/em><\/strong>Atafunga punda wake katika mzabibu, Na mwana-punda wake katika mzabibu mzuri. Amefua nguo zake kwa mvinyo, Na mavazi yake kwa damu ya zabibu.<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #003366;\"> <strong><em><sup>12\u00a0<\/sup><\/em><\/strong>Macho yake yatakuwa mekundu kwa mvinyo, Na meno yake yatakuwa meupe kwa maziwa.<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #003366;\"> <strong><em><sup>13\u00a0<\/sup><\/em><\/strong>Zabuloni atakaa pwani ya bahari, Naye atakuwa kama pwani za kuegesha merikebu, Na mpaka wake utakuwa kando ya Sidoni.<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #003366;\"> <strong><em><sup>14\u00a0<\/sup><\/em><\/strong>Isakari ni punda hodari, Ajilazaye kati ya mazizi ya kondoo;<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #003366;\"> <strong><em><sup>15\u00a0<\/sup><\/em><\/strong>Akaona mahali pa raha, kuwa pema, Na nchi, ya kuwa ni nzuri, Akainama bega lake lichukue mizigo, Akawa mtumishi kwa kazi ngumu.<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #003366;\"> <strong><em><sup>16\u00a0<\/sup><\/em><\/strong>Dani atahukumu watu wake, Kama moja ya makabila ya Israeli;<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #003366;\"> <strong><em><sup>17\u00a0<\/sup><\/em><\/strong>Dani atakuwa nyoka barabarani, Bafe katika njia, Aumaye visigino vya farasi, Hata apandaye ataanguka chali.<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #003366;\"> <strong><em><sup>18\u00a0<\/sup><\/em><\/strong>Wokovu wako nimeungoja, Ee Bwana.<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #003366;\"> <strong><em><sup>19\u00a0<\/sup><\/em><\/strong>Gadi, jeshi litamsonga, Lakini atawasonga wao mpaka visigino.<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #003366;\"> <strong><em><sup>20\u00a0<\/sup><\/em><\/strong>Asheri, chakula chake kitakuwa kinono, Naye atatoa tunu za kifalme.<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #003366;\"> <strong><em><sup>21\u00a0<\/sup><\/em><\/strong>Naftali ni ayala aliyefunguliwa; Anatoa maneno mazuri.<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #003366;\"> <strong><em><sup>22\u00a0<\/sup><\/em><\/strong>Yusufu ni mti mchanga wenye kuzaa, Mti mchanga wenye kuzaa karibu na chemchemi, Matwi yake yametanda ukutani.<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #003366;\"> <strong><em><sup>23\u00a0<\/sup><\/em><\/strong>Wapiga mishale walimtenda machungu, Wakamtupia, wakamwudhi,<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #003366;\"> <strong><em><sup>24\u00a0<\/sup><\/em><\/strong>Lakini upinde wake ukakaa imara, Mikono yake ikapata nguvu, Kwa mikono ya Mwenye Enzi wa Yakobo; Kwa jina la mchungaji, yeye jiwe la Israeli,<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #003366;\"> <strong><em><sup>25\u00a0<\/sup><\/em><\/strong>Naam, kwa Mungu wa baba yako atakaye kusaidia; Kwa mibaraka ya mbinguni juu. Mibaraka ya vilindi vilivyo chini, Mibaraka ya maziwa, na ya mimba.<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #003366;\"> <strong><em><sup>26\u00a0<\/sup><\/em><\/strong>Mibaraka ya baba yako Imepita mibaraka ya milima ya kale, Vitu vinavyotamanika vya vilima vya milele; Na vikae juu ya kichwa cha Yusufu, Juu ya utosi wa kichwa chake aliye mkuu kati ya ndugu zake.<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #003366;\"> <strong><em><sup>27\u00a0<\/sup><\/em><\/strong>Benyamini ni mbwa-mwitu mwenye kurarua-rarua Asubuhi atakula mawindo, Na jioni atagawanya mateka.<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #003366;\"> <strong><em><sup>28\u00a0<\/sup><\/em><\/strong>Hizo zote ndizo kabila za Israeli kumi na mbili. Na hayo ndiyo aliyowaambia baba yao, na kuwabariki; mmoja mmoja kwa mbaraka wake aliwabariki.<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #003366;\"> <strong><em><sup>29\u00a0<\/sup><\/em><\/strong>Akawaamuru, akasema, Mimi ninakwenda kukusanywa pamoja na watu wangu; mnizike pamoja na baba zangu, katika pango iliyomo shambani mwa Efroni, Mhiti;<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #003366;\"> <strong><em><sup>30\u00a0<\/sup><\/em><\/strong>katika ile pango iliyomo shambani mwa Makpela, iliyo mbele ya Mamre katika nchi ya Kanaani, aliyoinunua Ibrahimu pamoja na shamba kwa Efroni Mhiti, pawe milki yake ya kuzikia.<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #003366;\"> <strong><em><sup>31\u00a0<\/sup><\/em><\/strong>Humo walimzika Ibrahimu, na Sara mkewe; humo wakamzika Isaka, na Rebeka mkewe; nami humo nikamzika Lea;<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #003366;\"> <strong><em><sup>32\u00a0<\/sup><\/em><\/strong>shamba na pango iliyomo lililonunuliwa kwa wazawa wa Hethi.<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #003366;\"> <strong><em><sup>33\u00a0<\/sup><\/em><\/strong>Basi Yakobo alipokwisha kuwaagiza wanawe, akakunja miguu yake kitandani, akafa, akakusanywa pamoja na watu wake.<\/span><\/p>\n<p>&nbsp;<\/p>\n<p>&nbsp;<\/p>\n<p><strong>MASWALI YA KUJADILI:<\/strong><\/p>\n<hr \/>\n<p>1. Je, ni wajibu wa mzazi kuwajulisha watoto yatakayowapata siku za mwisho? Je maneno ya mwisho ya mzazi yana mchango gani katika kuyaongoza maisha ya mtoto? Je, ni vizuri kutamka laana kwa mtoto?<\/p>\n<p>2. Mtoto wa kwanza kuzaliwa anatarajiwa kuchukua nafasi gani katika familia? Kwa nini watoto wengine wa kwanza wameshindwa kufikia matarajio ya wazazi?<\/p>\n<p>3. Je, kosa alilolifanya Reubeni halikuwa na uwezekano wa kusameheka kwa baba yake? Je lilitosha kumuondolea sifa ya mzaliwa wa kwanza?<\/p>\n<p>4. Wanadanu wote watakaokombolewa watapewa hadhi ya kuwa wazaliwa wa kwanza. Unadhani wanastahili sifa hiyo? (Waebrania 12:22-23)<\/p>\n<p>5. Je kile alichofanya Yuda kumtetea mdogo wake Benjamini na baba yake na kujitoa ili a achukue adhabu iliyomstahili mdogo wake (Mwanzo 44) kilichangia kumpandisha hata likawa ndiyo kabila linalotoa viongozi?<\/p>\n<p>6. Je, uongozi unasomewa au uongozi unawahusu wazaliwa wa kwanza au huwa mtu anazaliwa nao? ( Zaburi 89:27).<\/p>\n<p>7. Je, wapiga mishale gani unaowakumbuka maishani mwako waliokutenda machungu lakini bado uliendelea kusimama?<\/p>\n<p>8. Ili kuiokoa familia na kutimiza makusudi ya Mungu maishani wakati fulani huwa ni lazima kujitenga mbali na familia na marafiki zako na kwenda kuishi uhamishoni kama Yusufu?<\/p>\n<p>9. Je ni vizuri kuwa na mazoea ya kuwaombea watoto wako baraka? Je baraka unazowatamkia watoto wako zina uwezekano wa kuwapata?<\/p>\n<p>10. Je, ni lazima ukifa ukazikwe kwenye eneo walikozikiwa wazazi wako? Kwa nini baada ya kumaliza hotuba yake kwa wanawe Yakobo alifariki. Je alijua kuwa saa yake ya kuondoka duniani imefika?<\/p>\n<div class='share-to-whatsapp-wrapper'><div class='share-on-whsp'>Share on: <\/div><a data-text='Mwanzo 49: Usomaji wa Biblia' data-link='https:\/\/tgvs.org\/injili\/archives\/1862' class='whatsapp-button whatsapp-share'>WhatsApp<\/a><div class='clear '><\/div><\/div>","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Mwanzo 49: \u00a0 1 Yakobo akawaita wanawe, akasema, Kusanyikeni, ili niwaambie yatakayowapata siku za mwisho. 2\u00a0Kusanyikeni, msikie, enyi wana wa Yakobo, Msikilizeni Israeli, baba yenu. 3\u00a0Reubeni, u mzaliwa wangu wa kwanza, Nguvu zangu, na malimbuko ya uwezo wangu. Umewapita wengine kwa ukuu na kwa nguvu. 4\u00a0Umeruka mpaka kama maji, basi usiwe na ukuu, Kwa sababu <a class=\"read-more-link\" href=\"https:\/\/tgvs.org\/injili\/archives\/1862\"><br \/>&#8230;read more<\/a><\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":1561,"comment_status":"closed","ping_status":"closed","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"om_disable_all_campaigns":false,"_monsterinsights_skip_tracking":false,"_monsterinsights_sitenote_active":false,"_monsterinsights_sitenote_note":"","_monsterinsights_sitenote_category":0,"footnotes":""},"categories":[23],"tags":[],"class_list":["post-1862","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-usomaji-vidokezo"],"jetpack_featured_media_url":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-content\/uploads\/2020\/10\/Default-Featured-Image-2020.jpg","_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/1862","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=1862"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/1862\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":1863,"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/1862\/revisions\/1863"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/media\/1561"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=1862"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=1862"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=1862"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}