{"id":1903,"date":"2022-07-24T06:16:02","date_gmt":"2022-07-24T10:16:02","guid":{"rendered":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/?p=1903"},"modified":"2022-07-24T06:27:08","modified_gmt":"2022-07-24T10:27:08","slug":"joshua-5-maswali-majibu","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/archives\/1903","title":{"rendered":"Joshua 5: Maswali &#038; Majibu"},"content":{"rendered":"<p><em>Mwongozo wa Kujifunza Biblia\/ Yoshua 5, (6-BSG-5J)\/ Katika ibara fupi, jibu maswali au andika mawazo makuu uliyojifunza katika sura hii.<\/em><\/p>\n<hr \/>\n<p>&nbsp;<\/p>\n<p>[1] <strong>Je, unaweza kuandika muhtasari wa sura za Yoshua 1 hadi 8? <\/strong>Ndiyo.<\/p>\n<ul>\n<li>Yoshua 1, Utume wa Yoshua.<\/li>\n<li>Yoshua 2, Uongofu wa Rahabu.<\/li>\n<li>Yoshua 3, Kuvuka Yordani.<\/li>\n<li>Yoshua 4, Mawe ya Ukumbusho.<\/li>\n<li>Yoshua 5, Utayari wa Kiroho.<\/li>\n<li>Yoshua 6, Kupiga Kelele Kuiangusha Yeriko.<\/li>\n<li>Yoshua 7, Uasi na Kushindwa.<\/li>\n<li>Yoshua 8, Utii na Ushindi.<\/li>\n<\/ul>\n<p>Kwa ufupi tuliona kuuvuka Mto Yordani kimuujiza. Tukio hili la kuvuka, kwa Waisraeli, lilikuwa muhimu kama kuivuka Bahari ya Shamu. Yoshua aliiongoza Israeli kuvuka Yordani baada ya Mungu kuukausha mto huo. Mawe ya ukumbusho yaliwekwa, wanaume Waisraeli wote wakatahiriwa, na watu wakaadhimisha Pasaka ya kwanza katika Nchi ya Ahadi.<\/p>\n<p>[2] <strong>Sura hii inahusu nini hasa?<\/strong> &#8212; Jensen anaeleza &#8220;Israeli ilikuwa bado haijajiandaa kikamilifu kuingia vitani katika ardhi ya Kanaani. Shughuli ambayo haikuwa imekamilika ilikuwa <u>hali ya kiroho<\/u>. Kwa sehemu, ilihusisha kuishika sheria ya Musa (cf. Yoshua 1:7\u20138); kijumla, ulikuwa uhusiano wa moyoni wa Israeli kwa Yehova.\u201d Sura hii inarekodi matukio manne ambayo Mungu alileta kwa Yoshua na watu hao, kila moja likihusu ishara, au alama: <span style=\"color: #0000ff;\">tohara, damu, tunda, na upanga<\/span>.&#8221;<\/p>\n<p>[3] <strong>Kwa nini mioyo ya Waamori na Wakanaani iliyeyuka waliposikia kwamba Bwana ameikausha Yordani?<\/strong> (5:1) Kwa sababu walijua kwamba Yehova alikuwa upande wa Israeli.<\/p>\n<ul>\n<li>\u201cTaarifa za Mungu kufungua kimuujiza njia ya kuvukia zilizua hofu kwa Wakanaani. Muujiza huo ulikuwa wa kustaajabisha na wa kushtua zaidi kwa vile Mungu aliutenda wakati Yordani imefurika hadi kwenye kingo zake (3:15). Kwa watu katika Nchi hiyo, muujiza huu lilikuwa onesho madhubuti linalothibitisha kwamba Mungu ni mkuu (4:24). Hii ilikuja baada ya ripoti nyingine kuhusu muujiza wa Bahari ya Shamu (2:10).\u201d \u2013 [John MacArthur Jr., Ed., The MacArthur Study Bible, electronic ed., (Nashville, TN: Word Pub., 1997), 309].<\/li>\n<\/ul>\n<p>[4] <strong>Ni vifaa gani vilitumika katika kutekeleza kaida ya tohara?<\/strong> (5:2) Visu vya mawe ya gumegume.<\/p>\n<p>[5] <strong>Kwa nini walitahiriwa?<\/strong> (5:4) \u201cWatu wote waliotoka Misri, waliokuwa waume, hao watu waume wote waendao vitani walikufa katika bara njiani, baada ya wao kutoka Misri.\u201d<\/p>\n<ul>\n<li>Hapa Mungu anamkumbusha Yoshua yale aliyokuwa ameyaona kwa miaka 40: Waisraeli wakifa kila siku jangwani kwa sababu ya \u201ckutokuamini\u201d na \u201ckutotii\u201d kwao&#8211; (kumbuka kwamba maneno haya mawili ni kinyume cha &#8216;kutumani&#8217; na &#8216;kutii&#8217;). Waisraeli walitoka Misri kwa ushindi (tazama Kut. 14: 13) lakini hawakufanikiwa kufika nchi ya Ahadi! Ni aibu iliyoje!<\/li>\n<\/ul>\n<p>[6]<strong> Je, hii ilikuwa tohara ya kwanza au ya pili ya wana wa Israeli?<\/strong> (5:2) \u2013<\/p>\n<ul>\n<li>\u201cMungu alimwamuru Yoshua kuhakikisha kwamba jambo hilo lilifanywa kwa wanaume wote walio chini ya miaka 40. Hawa walikuwa wana wa kizazi kilichokufa jangwani, wahanga (cf. vv. 6, 7) kutoka kwenye kizazi kipya ambacho Mungu aliwaokoa katika Hes. 13, 14. Ishara hii ya tohara ya kujiadhimu kiimani kwenye Agano la Ibrahimu (tazama Mwa. 17:9\u201314) ilikuwa imepuuzwa wakati wa safari nyikani. Sasa <u>Mungu alitaka irejeshwe<\/u>, hivyo Waisraeli wangeanza vyema katika Nchi waliyokuwa wakimiliki.\u201d \u2013 (Ibid, uk. 309).<\/li>\n<li>\u201cJitahirini kwa Bwana, <u>mkaziondoe govi za mioyo yenu<\/u>, enyi watu wa Yuda na wenyeji wa Yerusalemu; <u>ghadhabu Yangu isije ikatoka kama moto<\/u>, ikawaka hata mtu asiweze kuizima, kwa sababu ya uovu wa matendo yenu.\u201d (Yeremia 4:4)<\/li>\n<\/ul>\n<p>[7] <strong>Je, wana wa Israeli walitahiriwa juu ya kilima gani?<\/strong> (5:3) Katika Gibeath-haaralothi\/ au \u201cKilima cha magovi.\u201d<\/p>\n<p>[8] <strong>Nani aliyefia jangwani njiani?<\/strong> (5:5) Watu wote waliotoka Misri waliokuwa wanaume, watu wote wa vita.<\/p>\n<p>[9]<strong> Ni wapi walipofia wanaume wote, watu wa vita?<\/strong> (5:4) Jangwani.<\/p>\n<p>[10] <strong>Ni kaida gani iliyokuwa imetendwa kwa wanaume wote waliotoka Misri?<\/strong> (5:5)<\/p>\n<ul>\n<li>\u201cHuku wakiteseka chini ya \u201cukiukwaji wa ahadi\u201d ya Yehova (Hes. 14:34) na kama ukumbusho wa agano lililovunjwa, <u>watu hao walikuwa wamekatazwa kufanya tohara nyikani<\/u> (PP 406). Kuingia kwao Kanaani ulikuwa ushahidi wa kurejeshwa kwenye fadhila ya kiungu (tazama Hes. 14:23; Zab. 95:7\u201311). Kwa miaka 38 walikuwa wamebeba shutuma ya uasi huko Kadeshi.\u201d &#8212; (The Seventh-day Adventist Bible Commentary, 2:194).<\/li>\n<li>\u201cIngawa <strong>wanaume wote<\/strong> wa Israeli <strong>walikuwa wametahiriwa<\/strong> kabla ya kuondoka <strong>Misri<\/strong>, <strong>walifia<\/strong> nyikani kwa sababu ya kutotii kwao huko Kadesh-barnea (Hes. 20:1\u201313; cf. Hes. 27:14; Kumb. 32:51). <strong>Wana wao<\/strong> waliozaliwa wakati wa kutanga nyikani <strong>hawakutahiriwa<\/strong>, iliyokuwa ushahidi zaidi wa kutojali mambo ya kiroho kwa wazazi wao. Kwa hiyo, kaida hii takatifu ilihitaji kufanywa juu ya kizazi hiki kipya.\u201d \u2013[Donald K. Campbell, <em>The Bible Knowledge Commentary: An Exposition of the Scriptures<\/em>, 1985, 1, 337].<\/li>\n<\/ul>\n<p>[11] <strong>Waisraeli walikuwa wametanga nyikani kwa muda gani?<\/strong> (5:6) Kwa miaka arobaini.<\/p>\n<p>[12] <strong>Nini kiliwapata na kwa nini?<\/strong> (5:6) \u2013 \u201cWalitembea muda wa miaka arobaini barani, hata hilo taifa zima, yaani, watu waume waendao vitani, waliotoka Misri, <strong>walipokuwa wameangamia<\/strong>; kwa sababu hawakuisikiza sauti ya BWANA.\u201d<\/p>\n<ul>\n<li><strong>Taifa Zima<\/strong>. \u201cYaani isipokuwa Kalebu na Yoshua (Hes. 14:30). Inaonekana kwamba makuhani, labda Walawi wote, hawakuhusika na hukumu ya kifo huko Kadeshi na kwamba baadhi yao walisalimika. Eleazari, mwana wa Haruni, anatajwa kipekee kwamba anaingia katika Nchi ya Ahadi (tazama Kut. 6:25; 28:1; Yoshua 24:33). Hakuwepo mwakilishi wa Walawi miongoni mwa wale wapelelezi 12 (Hes. 13:3\u201316), wala miongoni mwa \u201cwatu wa vita.\u201d&#8212; (The Seventh-day Adventist Bible Commentary, 2:194).<\/li>\n<\/ul>\n<p>[13] <strong>Mungu aliwaapia baba za Waisraeli kwamba angewapa nchi, lakini aliwaapia nini wale waliotoka Misri?<\/strong> (5:6) Hangewaruhusu waione nchi hiyo.<\/p>\n<p>[14]<strong> Nchi ya Kanaani inaelezewaje katika sura ya 5?<\/strong> (5:6) &#8212; Nchi yenye [mavuno tele] imiminikayo maziwa na asali!<\/p>\n<p>[15] <strong>Je, Bwana alisema alikuwa ameviringisha nini katika<\/strong> <strong>5:9?<\/strong> \u2013&#8221;Aibu (fedheha, dhihaka, kejeli) ya Misri kutoka kwenu.\u201d<\/p>\n<p>[16] <strong>Aibu ya Misri ni nini?<\/strong> (5:9) \u2013 \u201cKwa sababu ya uasi huko Kadeshi, Mungu hakuweza kuwaongoza Israeli kuingia Kanaani\u2014kusudi lilelile alilokuwa amewaongoza kutoka Misri. Hawakuwa wameruhusiwa kutahiriwa, ishara iliyowatia alama kuwa watu wateule wa Mungu. Kusitishwa kwa kaida hii ulikuwa shahidi wa kudumu kwao kwamba walikuwa wamevunja agano.<\/p>\n<p>Ingawa \u201cMalaika\u201d wa agano aliendelea kuiongoza Israeli katika kutanga kwao jangwani, hata hivyo, hawakurudishwa kikamilifu kwenye uhusiano wa agano katika kipindi hicho kirefu. Kadiri walivyobaki, angalau kwa kiasi fulani, nje ya agano, walibaki katika uhusiano uleule kwa Mungu kana kwamba hawakuwahi kutoka Misri. \u201c<strong>Aibu ya Misri<\/strong>\u201d bado ilikuwa juu yao. Sasa, <u>kwa kurudishwa kwa Pasaka<\/u>\u2014ukumbusho wa kukombolewa kutoka Misri\u2014na kurejeshwa kwa kaida ya tohara, \u201caibu\u201d hiyo iliondolewa kabisa, au \u201ckuviringishiwa\u201d mbali. Tayari miguu yao ilikuwa imepandwa kwenye udongo wa Nchi ya Ahadi. Kuondolewa kwa laana hiyo kulifanyiwa ukumbusho kwa kupaita mahali walipoweka kambi lao la kwanza katika Kanaani, Gilgali, ambalo humaanisha \u201ckuviringisha.\u201d<\/p>\n<p>Kuna kiwango fulani ya aibu inayo juu ya watu wa Mungu leo. Wao pia wangepaswa kuwa katika ufalme muda mrefu uliopita, lakini kama Israeli, wamekuwa wakitanga huku na huko jangwani (GC 458). \u201c<u>Basi, imesalia pumziko kwa watu wa Mungu<\/u>\u201d katika siku zetu (Ebr. 4:9). \u201c<u>Hebu tufanye kazi\u201d kwa bidii \u201ckuingia katika pumziko hilo<\/u>\u201d(v. 11).\u201d \u2013 [Francis D. Nichol, Ed., The Seventh-Day Adventist Bible Commentary, (Review and Herald Publishing Association, 1976), 2:194].<\/p>\n<p>&nbsp;<\/p>\n<p>[17]<strong> Jina la mahali ambapo Waisraeli walitahiriwa lilikuwa lipi?<\/strong> (5:9) Gilgali (kuviringisha)<\/p>\n<p>[18]<strong> Baada ya tohara kukamilika, Waisraeli walikaa mahali pao kambini kwa muda gani?<\/strong> (5:8) Walikaa mahali pao kambini hadi walipopona.<\/p>\n<p>[19]<strong> Wana wa Israeli waliadhimisha sikukuu gani huko Gilgali?<\/strong> (5:10) Pasaka.<\/p>\n<p>[20]<strong> Ni siku gani ya mwezi ambapo Waisraeli waliiadhimisha Pasaka?<\/strong> (5:10) Jioni ya siku ya kumi na nne ya mwezi.<\/p>\n<p>[21]<strong> Ni mahali gani ambapo Waisraeli waliiadhimisha Pasaka katika sura ya 5?<\/strong> (5:10) Kwenye nchi tambarare za jangwa la Yeriko.<\/p>\n<p>[22]<strong> Waisraeli walikula chakula gani siku iliyofuata baada ya Pasaka?<\/strong> (5:11) Baadhi ya mazao ya nchi, Mikate Isiyotiwa Chachu, na Nafaka Iliyookwa.<\/p>\n<p>Mungu alikuwa ameanza kuwapatia MANA tangu wakati wa Kutoka 16 na alifanya hivyo kwa miaka 40 (Kut. 16:35). Kwa vile sasa chakula kilikuwa kingi katika nchi ya Kanaani, wangeweza kujipatia wenyewe mazao kama vile tende, shayiri, na zeituni.<\/p>\n<p>[23]<strong> Je, ni wakati gani ambapo Mungu aliacha kuwapa watu Mana?<\/strong> (5:12) Siku iliyofuata baada ya kula baadhi ya mazao ya nchi.<\/p>\n<p>[24]<strong> Wana wa Israeli wakala matunda ya nchi ya nchi gani?<\/strong> (5:12) Nchi ya Kanaani<\/p>\n<p>[25]<strong> Yoshua alipokuwa karibu na Yeriko, akainuka kichwa kutazama, akamwona Mtu amesimama mbele yake; Mtu huyu alikuwa nani? <\/strong>(5:14) Amiri wa jeshi la BWANA.<\/p>\n<p>Huyu ni Bwana Yesu Kristo katika mwonekano wa kibinadamu kabla hajafanyika mwili (Uhamwilisho). Hapa, Alikuja kama Malaika (Mjumbe) wa BWANA kana kwamba alikuwa mwanadamu (linganisha maelezo kuhusu &#8220;malaika&#8221; watatu katika Mwa. 18).<\/p>\n<ol>\n<li>\u201c<strong>Malaika wa Bwana<\/strong> akamtokea, katika mwali wa moto uliotoka katikati ya kijiti; akatazama, na kumbe! Kile kijiti kiliwaka moto, nacho kijiti hakikuteketea.\u201d \u201cNaye akasema, Usikaribie hapa; vua viatu vyako miguuni mwako; maana mahali hapo unaposimama ni nchi takatifu.\u201d (Kutoka 3:2, 5)<\/li>\n<li>\u201c<strong>Bwana akamwambia Yoshua<\/strong>, Tazama, nimeutia Yeriko katika mkono wako, na mfalme wake, na mashujaa wake.\u201d (Yoshua 6:2)<\/li>\n<li>\u201c<strong>Huyo amiri wa jeshi la Bwana<\/strong> akamwambia Yoshua, Vua viatu vyako miguuni mwako; kwa kuwa mahali hapo usimamapo ni patakatifu. Yoshua akafanya vivyo.\u201d (Yoshua 5:15)<\/li>\n<\/ol>\n<p>[26]<strong> Ni silaha gani ya vita aliyokuwa nayo mkononi Mtu aliyemtokea Yoshua?<\/strong> (5:13) Upanga uliofutwa. Upanga uliochomolewa alani, ulionesha mkao ukidhihirisha kwamba Kapteni wa jeshi la BWANA alikuwa tayari kuwapa Waisraeli ushindi dhidi ya Wakanaani (Josh 6:2; 1:3).<\/p>\n<p>[27]<strong> Baada ya kugundua huyo amiri wa jeshi la BWANA ni nani, Yoshua anafanya mambo gani mawili?<\/strong> (5:14) Akaanguka kifudifudi hadi chini, akasujudu; akamwambia, <u>Bwana wangu ana nini cha kumwambia mtumishi Wake<\/u>?\u201d<\/p>\n<p>[28]<strong> Ni agizo gani ambalo amiri wa jeshi la Bwana alimpa Yoshua?<\/strong> (5:15) &#8212; \u201cVua viatu vyako miguuni mwako; kwa kuwa mahali hapo usimamapo ni patakatifu).\u201d Yoshua akafanya hivyo<\/p>\n<div class='share-to-whatsapp-wrapper'><div class='share-on-whsp'>Share on: <\/div><a data-text='Joshua 5: Maswali & Majibu' data-link='https:\/\/tgvs.org\/injili\/archives\/1903' class='whatsapp-button whatsapp-share'>WhatsApp<\/a><div class='clear '><\/div><\/div>","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Mwongozo wa Kujifunza Biblia\/ Yoshua 5, (6-BSG-5J)\/ Katika ibara fupi, jibu maswali au andika mawazo makuu uliyojifunza katika sura hii. &nbsp; [1] Je, unaweza kuandika muhtasari wa sura za Yoshua 1 hadi 8? Ndiyo. Yoshua 1, Utume wa Yoshua. Yoshua 2, Uongofu wa Rahabu. Yoshua 3, Kuvuka Yordani. Yoshua 4, Mawe ya Ukumbusho. Yoshua 5, <a class=\"read-more-link\" href=\"https:\/\/tgvs.org\/injili\/archives\/1903\"><br \/>&#8230;read more<\/a><\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":1561,"comment_status":"closed","ping_status":"closed","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"om_disable_all_campaigns":false,"_monsterinsights_skip_tracking":false,"_monsterinsights_sitenote_active":false,"_monsterinsights_sitenote_note":"","_monsterinsights_sitenote_category":0,"footnotes":""},"categories":[16],"tags":[],"class_list":["post-1903","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-bsg"],"jetpack_featured_media_url":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-content\/uploads\/2020\/10\/Default-Featured-Image-2020.jpg","_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/1903","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=1903"}],"version-history":[{"count":2,"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/1903\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":1905,"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/1903\/revisions\/1905"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/media\/1561"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=1903"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=1903"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=1903"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}