{"id":1906,"date":"2022-07-25T11:34:59","date_gmt":"2022-07-25T15:34:59","guid":{"rendered":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/?p=1906"},"modified":"2022-07-25T11:34:59","modified_gmt":"2022-07-25T15:34:59","slug":"yoshua-6-maswali-na-majibu","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/archives\/1906","title":{"rendered":"Yoshua 6: Maswali na Majibu."},"content":{"rendered":"<p><em>Mwongozo wa Kujifunza Biblia\/ Yoshua 6, (6-BSG-6J)\/ Katika ibara fupi, jibu maswali au andika mawazo makuu uliyojifunza kuhusu sura hii.<\/em><\/p>\n<hr \/>\n<p>&nbsp;<\/p>\n<p>[1] <strong>Sura hii inahusu nini hasa<\/strong>? &#8212; Sasa tunaingia sehemu mpya katika Kitabu cha Yoshua. Katika Yoshua 1 hadi 5, mada ni &#8220;Kuingia Kanaani.&#8221; Yoshua 6-12 inahusika na &#8220;Kuiteka Kanaani,&#8221; itakayowachukua Israeli kama miaka saba, kwanza kushinda eneo la kati (kuanzia Yeriko), kisha eneo la kusini, na hatimaye eneo la kaskazini. Sura hii inaelezea kutekwa kwa Yeriko. Ukweli mkuu hapa ni kwamba ushindi wa kiroho hupatikana kwa njia zinazoweza kuwa za kipuuzi kabisa na zisizotosheleza katika mtazamo wa hekima ya kibinadamu (1 Kor. 1:17\u201329; 2 Kor. 10:3\u20135).<\/p>\n<p>[2] <strong>Yeriko ilijitayarishwaje kupinga shambulio hilo?<\/strong> (6:1) Mji huu ulifungwa kabisa kwa sababu ya kuwahofia \u201cwana wa Israeli,\u201d hakuna mtu aliyetoka, wala hakuna aliyeingia. Watu wa Yeriko walitazamia kwamba Waisraeli wangeuzingira mji wao (cf. Yos. 2:10\u201311).<\/p>\n<p>Ufalme wa Ogu ulikuwa na &#8220;miji iliyokingwa kwa kuta ndefu, na malango, na makomeo&#8221; (Kumb 3:4-5). Hata hivyo &#8220;iliharibiwa kabisa,&#8221; kama ilivyofanywa miji ile katika ufalme wa Sihoni (Kumb 3:6). Na Yeriko ilijua hatima ya Sihoni na Ogu (Yos 2:10), iliyokuwa imechangia hofu yao ya kwanza.<\/p>\n<p>[3] <strong>Kabla ya anguko la Yeriko, ni mambo gani matatu ambayo Mungu alimwambia ameweka mkononi mwa Yoshua<\/strong><strong>?<\/strong> (6:2) Yeriko, pamoja na mfalme wake na mashujaa wa vita.<\/p>\n<ul>\n<li>Yeriko ilikuwa mojawapo ya miji ya kale zaidi ulimwenguni. Ilikuwa na kuta mbili kubwa sana, zikiachana umbali wa futi kumi na tano, zikiizunguka, pamoja na askari kwenye kuta na walinzi kwenye malango yaliyofungwa; Yeriko iliaminika kuwa ngome isiyopenyeka. Kuiteka, kibinadamu, haikuwezekana (Yos. 6:1). Lakini Mungu anamwambia Yoshua, \u201cNimeiweka\u201d Yeriko mikononi mwako. Si kwamba nitafanya \u201cnimeshafanya hilo.\u201d Kwa maneno mengine, sasa ni yako kabisa na ni milki yako. Je, Yoshua ataamini hili?<\/li>\n<\/ul>\n<p>&nbsp;<\/p>\n<ul>\n<li>Mungu amefanya kazi hizo (Yoshua 1:2; 2:8\u201311; 5:1; 10:8). Yoshua na Israeli wanahitaji kuamini tu (cf. Efe. 2:8\u20139). Mungu anaweza kuleta hakikisho kabla ya vita (Linganisha, Zab. 18:43; 54:7; 56:13; 71:23; 86:13; 116:8)<\/li>\n<\/ul>\n<p>[4] <strong>Ni mara ngapi Waisraeli wangepaswa kuizunguka Yeriko kila moja ya siku sita za kwanza?<\/strong> (6:3) Mara moja kila siku<\/p>\n<p>[5] <strong>Ni makuhani wangapi wangepaswa kulitangulia Sanduku walipouzunguka mji wa Yeriko?<\/strong> (6:4) Makuhani saba<\/p>\n<p>[6] <strong>Makuhani wangepaswa kupuliza kwa ala zipi?<\/strong> (6:4) Matarumbeta saba<\/p>\n<p>Tukio hili pengine lilitokea wakati wa siku saba za Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu (durusu Yos. 5:11).<\/p>\n<ul>\n<li>Kama Pasaka (Yos. 5:10), sherehe hiyo ilikuwa na maana mpya kwa kizazi cha Yoshua.<\/li>\n<li>Namba \u201cSaba\u201d humaanisha ukamilifu au utimilifu.<\/li>\n<li>Siku saba\u201d pia zinaashiria tukio la pekee kwa ajili ya Mungu (Mwa. 7:4, 10; Kut. 7:25; 29:37; 1 Sam 13:8; 1 Flm. 8:65; 2 Nya. 30:22, 23; Neh. 8:18).<\/li>\n<li>Wale makuhani saba, matarumbeta saba, na maandamano saba pia yanasisitiza jambo hilo (6:4, 13, 15, 16).<\/li>\n<\/ul>\n<p>[7] <strong>Ni chombo gani cha hema la kukutania ambacho makuhani wangepaswa kubeba walipokuwa wakiuzunguka mji wa Yeriko?<\/strong> (6:4, 6) Sanduku la Agano.<\/p>\n<ul>\n<li><strong>Kazi ya<\/strong> <strong>Sanduku la Agano:<\/strong> Lilikuwa na mabamba ya Sheria \u2013(Kumb 10:5; Kut. 25:16, 21; 40:20; Kumb 31:24-26; 1 Flm. 8:9; Ebr. 9:4). Gudulia la Mana na fimbo ya Haruni viliwekwa kando ya Sanduku (Kut. 16:34; Hes. 17:10). Mungu alifunua amri Zake kwa Musa kupitia Sanduku (Hes. 7:89; Kut. 25:22; 30:6,36).<\/li>\n<li><strong>Sanduku lilikuwa ishara ya uwepo wa Mungu<\/strong> \u2013(Law. 16:2; Hes. 10:33-36; Yos. 7:6; Amu. 20:27; 2 Sam 7:2; Zab. 132:8). Pia lilitumika katika Siku kuu ya Upatanisho (Law. 16:13-15).<\/li>\n<li><strong>Utakatifu na Matokeo ya Sanduku:<\/strong> Kukosa heshimu juu ya Sanduku hilo kulileta hukumu \u2013 (2 Sam 6:6-7; 1 Nya. 13:9-10; Yos. 3:4; 1 Sam 5:1-4, 8-12; 6:19). Uwepo wa Sanduku ulileta baraka \u2013 (Yos 6; 2 Sam 6:11; 1 Nya. 13:14).<\/li>\n<li><strong>Maana ya Sanduku Kiishara:<\/strong> Makerubi (Kut. 37:9) yalionesha uwepo wa Bwana. \u201cBwana ambaye kwa mujibu wa Zab. 99:1 \u201c<u>huketi juu ya makerubi<\/u>,\u201d pia huwakilishwa na Kiti cha Rehema (Ebr. kapp\u014dre\u1e6f; Kiyunani: hilast\u0113rion), ambapo kiishara iliiruhusu Israeli kuleta damu ya upatanisho karibu na kiti cha enzi cha Bwana kadiri iwezekanavyo (Law. 16:14\u201316; cf. Ebr. 9:23\u201328). Mabawa ya makerubi yalifunika kiti cha rehema kwa kukilinda (cf. Ebr. 9:5), ambapo ingewezekana ikiwa nyuso zao zingekitazama kiti cha rehema (cf. 1 Pet. 1:12). Nafasi ya makerubi pia ilionesha <u>heshima kwa Bwana<\/u>, aliyekutana na kuzungumza na Musa kutoka \u201cjuu ya kiti cha rehema, katikati ya hayo makerubi mawili\u201d (Kut. 25:22). Kwa maneno mengine, Kiti cha Rehema hakikutumika tu kama kifuniko cha Sanduku la Agano bali kilikuwa na umuhimu wake pia.\u201d \u2013 [Allen C. Myers, The Eerdmans Bible dictionary, 1987, 84\u201385].<\/li>\n<\/ul>\n<p>[8] <strong>Ni mara ngapi Waisraeli walitakiwa kuizunguka Yeriko katika siku ya saba?<\/strong> (6:4) Mara saba.<\/p>\n<p>[9] <strong>Matarumbeta saba yalitengenezwa kwa kutumia nini?<\/strong> (6:4) Pembe za kondoo dume. Kupiga matarumbeta kuliitayarisha Israeli kwa ajili ya maandamano matakatifu (Hes. 10:9).<\/p>\n<p>[10] <strong>Ni mlio wa aina gani ungepaswa kupigwa kwa pembe za kondoo dume?<\/strong> (6:5) Sauti ya Tarumbeta. Kelele kuu zilitangaza ushindi katika vita na zikisindikiza maandamano ya Sanduku la Agano (tazama Hes. 10:2\u20136; 1 Sam 4:5\u20136; 2 Sam 6:15\u201316).<\/p>\n<p>Sura hii inadhihirisha tena kwamba Mungu anatumia mambo yanayoweza kuonekana ya kipuuzi ili kuwaaibisha wenye nguvu.<\/p>\n<ul>\n<li>Kwa Gideoni, alitumia mienge na mitungi.<\/li>\n<li>Kwa Daudi, alitumia kombeo na jiwe.<\/li>\n<li>Kwa Yoshua, alitumia matarumbeta na kelele.<\/li>\n<\/ul>\n<p>[11] <strong>Watu waliposikia sauti ya tarumbeta, wangepaswa kufanya nini?<\/strong> (6:5) \u2013 \u201cKupiga kelele kwa sauti kuu (ya vita); na ukuta wa mji utaanguka chini palepale, na hao watu watapanda, kila mtu akiendelea mbele kukabili [akikwea kwenye maangamizi ya mji].\u201d \u2013(AMP).<\/p>\n<p>[12] <strong>Ni nani aliyepita mbele ya sanduku la BWANA?<\/strong> (6:7) Makuhani saba wakibeba matarumbeta saba.<\/p>\n<p>[13] <strong>Yoshua aliwaambia nini watu katika 6:7?<\/strong> \u2013 \u201cSongeni mbele! Uzungukeni mji, na watu wenye silaha watangulie mbele ya Sanduku la BWANA.\u201d<\/p>\n<p>[14] <strong>Waisraeli walipokuwa wakiizunguka Yeriko, walipewa maagizo gani kuhusu kelele?<\/strong> (6:10) \u201cMsipiga kelele [kelele za vita] wala sauti yenu isisikike, wala neno lolote lisitoke vinywani mwenu, hata siku ile nitakapowaambia mpige kelele. Ndipo mtapiga kelele!\u201d \u2013 (AMP)<\/p>\n<p>[15] <strong>Yoshua aliwaambia watu wapige kelele siku gani na saa ngapi?<\/strong> (6:15-16) Siku ya saba.<\/p>\n<ul>\n<li>\u201cManeno ya kisa hicho yamewafanya baadhi kuamini kwamba usemi huu unarejelea siku ya Sabato. Hitimisho kama hilo halioneshwi kabisa. Hatujui ni siku gani ya juma maandamano hayo yalianza. Lakini kwa kuwa Waisraeli walitumia siku saba kufanya mizunguko kwenye mji huu, inaonekana kwamba moja ya siku hizo lazima ilikuwa Sabato. Mtazamo huu huibua swali ikiwa kitendo cha kuuzunguka mji huo kilipatana na kusudi la ibada halisi ya Sabato. <u>Tunaweza kubainisha kwamba Sabato ni siku iliyotengwa kwa ajili ya Mungu, na kwamba chochote anachoweza kuona kinafaa kukiamuru katika siku hiyo hakika kinapatana na kusudi la kuiadhimisha. Kulingana na amri ya kiungu, Sabato haipaswi kutumika \u201ckufanya njia zako mwenyewe, wala kutafuta anasa yako mwenyewe<\/u>\u201d (Isa. 58:13). Lakini tunaweza kutumia saa zake takatifu kwa usalama <u>kufanya kile ambacho Mungu anaamuru kifanywe siku hiyo<\/u> (tazama Mat. 12:5)\u201d \u2013 (The Seventh-day Adventist Bible Commentary, 2:198).<\/li>\n<\/ul>\n<p>[16] <strong>Kwa nini Yoshua aliwaambia watu wapige kelele siku ya 7 kuuzunguka mji wa Yeriko?<\/strong> (6:16) \u2013 &#8220;Maana Bwana amewapeni mji huu.\u201d<\/p>\n<p>[17] <strong>Nini ambacho kingetokea kwenye mji wa Yeriko?<\/strong> (6:17) Kila kitu kingeangamizwa kama (aina ya taadhima) kwa Bwana!<\/p>\n<p>[18] <strong>Ni watu gani wa Yeriko waliokolewa wakati Yeriko ikiangamizwa?<\/strong> (6:17) Rahabu, yule kahaba, na watu wote walio pamoja naye nyumbani mwake.<\/p>\n<ul>\n<li>\u201cRahabu aliepushwa kimahususi kwenye uangamivu huu katika rejea ya kwanza ya kitabu hiki juu yake tangu sura ya 2 (v. 17b). Kuepushwa huku kunakinzana na maagizo ya Yehova ya kushughulika na watu wa Kanaani katika Kumb. 7:1\u20135 na 20:16\u201318. Kumbukumbu la Torati 20:16\u201318 inasema, \u201cLakini katika miji ya mataifa ambayo BWANA, Mungu wako, anawapa kuwa urithi, usiache hai chochote chenye pumzi. Waangamize kabisa\u2014Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi\u2014kama ambavyo BWANA, Mungu wako, amekuamuru. La sivyo, <u>watawafundisha kufuata machukizo yote wanayofanya kwa kuabudu miungu yao, nanyi mtatenda dhambi dhidi ya BWANA, Mungu wenu<\/u>.\u201d Hata hivyo, kama tulivyoona hapo awali, tofauti kubwa kati ya Rahabu na Wakanaani wengine ilikuwa <strong>onesho lake la imani<\/strong>, katika matendo na maneno pia.\u201d \u2013 [<span style=\"color: #ff6600;\">David M. Howard Jr., Joshua, The New American Commentary, (Nashville: Broadman &amp; Holman Publishers, 1998), 5:173<\/span>].<\/li>\n<\/ul>\n<p>[19] <strong>Kwa nini Rahabu na wote waliokuwa katika nyumba yake waliokolewa wakati Yeriko ikiangamizwa?<\/strong> (6:17) Kwa sababu aliwajificha na kuwalinda wale wajumbe (wapelelezi) wawili ambao Yoshua alikuwa amewatuma.<\/p>\n<p>[20] <strong>Ni maagizo gani zaidi waliyopewa Waisraeli? <\/strong>(6:18) \u201cMsichukue chochote miongoni mwa vitu vilivyowekwa wakfu kwa ajili ya uangamivu, msije <u>mkaangamizwa kabisa<\/u>, na kuleta taabu juu ya kambi ya Israeli.\u201d (NLT).<\/p>\n<ul>\n<li>\u201cAya ya 18 hubainisha maelezo zaidi: \u201cLakini jiepusheni na vitu vilivyowekwa wakfu [\u1e25\u0113rem], msije mkajiletea uangamivu [\u1e25\u0101ram] kwa kuchukua chocho miongoni mwa [<u>vitu vilivyowekwa wakfu<\/u> (\u1e25\u0113rem)]. La sivyo, mtaifanya kambi ya Israeli kuwa na hatia ya kuangamizwa [\u1e25\u0113rem] na kuiletua taabu.\u201d Vitu fulani vingepaswa kutengwa kwa ajili ya uangamivu, na kama havingefanywa hivyo, Israeli yenyewe ingepatwa na maafa hayohayo; Israeli yenyewe ingekuwa \u201ckitu hicho kilichowekwa wakfu.\u201d &#8212; (Ibid, p. 173).<\/li>\n<\/ul>\n<p>[21] <strong>Ni vitu gani viliachwa wakati Yeriko ilipoangamizwa?<\/strong> (6:19) Kila kitu kilichotengenezwa kwa fedha, dhahabu, shaba, au chuma.<\/p>\n<p>[22] <strong>Kwa nini hivi viliachwa, na walipelekwa wapi?<\/strong> (6:19) Vilihesabiwa kuwa \u201cwatakatifu kwa Bwana\u201d na vililetwa katika hazina ya nyumba ya Bwana (v. 24).<\/p>\n<ul>\n<li>\u201cAya ya 19 inaendelea kujenga wazo hili. Hazina za Yeriko zingepaswa kutengwa kwa ajili ya Bwana, kwa kuwa zilikuwa wakfu, yaani, takatifu. Kwa hivyo, zilipaswa kwenda kwenye hazina Yake. Neno hapa la &#8220;<strong>hazina\u201d<\/strong> (\u02be\u00f4\u1e63ar) ndilo lilelile linalotumika kwa vile vya hekalu la Sulemani, lililojengwa miaka mingi baadaye (1 Flm. 7:51). Hata hivyo, kwa kuwa hakuna hekalu lililosimama katika siku za Yoshua, hali na mahali kamili pa hazina hiyo haijulikani. &#8220;<u>Hazina ya nyumba ya BWANA<\/u>&#8221; imetajwa katika aya ya 24; huenda ilihusishwa na \u201cnyumba ya Mungu\u201d <strong>huko Gilgali<\/strong> inayotajwa katika 9:23. Hema takatifu la Shilo katika siku za Samweli pia iliitwa \u201cnyumba ya BWANA\u201d (1 Sam 1:7). Hakuna haja ya kudhani kwamba hii ilirejelea, kimakosa, hekalu la baadaye. Katika Zab. 27:4, 6, maneno \u201cnyumba ya BWANA\u201d na \u201cmaskani Yake\u201d yanatumiwa kwa kubadilishana, na marejeo hapa katika Yoshua huenda yalikuwa kwenye maskani kama nyumba ya Bwana, wala si hekalu.\u201d &#8212; (Ibid, uk. 174).<\/li>\n<\/ul>\n<p>[23] <strong>Kuta za Yeriko ziliangukaje? <\/strong>(6:20) Watu waliposikia \u201csauti ya pembe za kondoo dume,\u201d walipiga kelele kwa sauti kuu kadiri walivyoweza. Ghafla, kuta za Yeriko zikaporomoka, na Waisraeli wakaharakisha kuingia moja kwa moja ndani ya mji na kuuteka.<\/p>\n<p>[24] <strong>Nini kilitokea juu ya vyote vilivyokuwa kwenye mji huo, na jinsi gani?<\/strong> (6:21) Waliangamiza kila kitu ndani yake kwa panga zao\u2014wanaume na wanawake, vijana kwa wazee, ng&#8217;ombe, kondoo, mbuzi, na punda.<\/p>\n<p>[25] <strong>Baada ya kumtoa Rahabu na wote waliokuwa nyumbani kwake nje kwa usalama, walikaa wapi?<\/strong> (6:23) Wakawaacha nje ya kambi ya Israeli.<\/p>\n<ul>\n<li>\u201cRahabu aliachwa kwa muda fulani nje ya kambi, bila shaka ili kumwandaa kupokelewa kama mwongofu. Katika wakati mwafaka aliingizwa katika kusanyiko la Israeli, yumkini baada ya yeye na watu wa ukoo wake kufundishwa dini ya Yehova na baada ya kujitakasa dhidi ya njia na imani zao za kipagani. <u>Pengine alikuwa mke wa Salmoni, mkuu wa Yuda, na mama yake Boazi, na hivyo mzazi mmojawapo wa mababu wa Mwokozi wetu<\/u> (angalia maelezo kwenye 1:5). Ni fursa yenye baraka iliyoje inawangoja wale ambao kwa imani wanajiunga na watu wa Mungu. Ni ajabu jinsi gani kujua kwamba injili ya Yesu Kristo inapita hata urithi na mazingira yasiyopendeza kabisa. \u201cYeyote atakaye,\u201d wa rangi au kabila lolote, au cheo chochote maishani, anaweza kushiriki fadhila tukufu za uwana.\u201d \u2013 (The Seventh-day Adventist Bible Commentary, 2:199).<\/li>\n<\/ul>\n<p>[26] <strong>Jinsi gani mji wa Yeriko uliangamizwa?<\/strong> (6:24) Kwa moto.<\/p>\n<p>[27] <strong>Rahabu aliishi Yeriko wakati wapelelezi walipotembelea mji huo. Alikuwa akiishi wapi wakati kitabu cha Yoshua kilipoandikwa?<\/strong> (6:25) Alikuwa akiishi Israeli hadi siku hii!<\/p>\n<p>[28] <strong>Ni laana gani aliyoitamka Yoshua kwa yeyote ambaye angejaribu kuujenga upya mji huu?<\/strong> (6:26) &#8212; \u201cLaana ya BWANA na iwe juu ya mtu ye yote atakayejaribu kuujenga upya mji wa Yeriko. <u>Kwa gharama ya mwanawe mzaliwa wa kwanza<\/u>, ataweka msingi wake. <u>Kwa gharama ya mwanawe mdogo<\/u>, atasimamisha malango yake.\u201d (NLT)<\/p>\n<p>Mungu alikuwa ameamuru kwamba mji wowote ulioangamizwa kwa sababu ya kueneza ibada ya miungu mingine \u2018usingekaliwa tena kamwe. Laana hii ilitimizwa katika 1 Wafalme 16.<\/p>\n<ul>\n<li><strong>Kumbukumbu la Torati 13:16 <\/strong>(<span style=\"color: #0000ff;\">NLT<\/span>) <strong>\u2014 <\/strong><strong>16<\/strong> Kisha mtakusanya nyara zote katikati ya uwanja wa wazi na kuziteketeza. Uteketezeni mji wote kama dhabihu ya kuteketezwa kwa BWANA Mungu wenu. Mji huo lazima ubaki magofu milele; usiweze kujengwa kamwe.<\/li>\n<li><strong>1 Wafalme 16:33\u201334 <\/strong>(<span style=\"color: #0000ff;\">NLT<\/span>) <strong>\u2014 <\/strong><strong>33<\/strong> Kisha akasimamisha nguzo ya Ashera. Alifanya mengi zaidi ili kumghadhibisha BWANA, Mungu wa Israeli, kuliko wafalme wengine wote wa Israeli waliomtangulia. <strong>34<\/strong> Wakati wa utawala wake ndipo Hieli, mtu kutoka Betheli, alijenga upya Yeriko. Alipoiweka misingi yake, ilimgharimu maisha ya Abiramu, mwanawe mkubwa. Na alipomaliza na kuweka malango yake, ilimgharimu maisha ya Segubu, mwanawe mdogo. Hayo yote yalitokea sawasawa na neno la BWANA juu ya Yeriko, lililonenwa na Yoshua, mwana wa Nuni.<\/li>\n<\/ul>\n<p>[29] <strong>Umaarufu wa Yoshua ulikuwa umeenea kiasi gani?<\/strong> (6:27) Sifa yake ilienea katika nchi yote.<\/p>\n<div class='share-to-whatsapp-wrapper'><div class='share-on-whsp'>Share on: <\/div><a data-text='Yoshua 6: Maswali na Majibu.' data-link='https:\/\/tgvs.org\/injili\/archives\/1906' class='whatsapp-button whatsapp-share'>WhatsApp<\/a><div class='clear '><\/div><\/div>","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Mwongozo wa Kujifunza Biblia\/ Yoshua 6, (6-BSG-6J)\/ Katika ibara fupi, jibu maswali au andika mawazo makuu uliyojifunza kuhusu sura hii. &nbsp; [1] Sura hii inahusu nini hasa? &#8212; Sasa tunaingia sehemu mpya katika Kitabu cha Yoshua. Katika Yoshua 1 hadi 5, mada ni &#8220;Kuingia Kanaani.&#8221; Yoshua 6-12 inahusika na &#8220;Kuiteka Kanaani,&#8221; itakayowachukua Israeli kama miaka <a class=\"read-more-link\" href=\"https:\/\/tgvs.org\/injili\/archives\/1906\"><br \/>&#8230;read more<\/a><\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":1561,"comment_status":"closed","ping_status":"closed","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"om_disable_all_campaigns":false,"_monsterinsights_skip_tracking":false,"_monsterinsights_sitenote_active":false,"_monsterinsights_sitenote_note":"","_monsterinsights_sitenote_category":0,"footnotes":""},"categories":[16],"tags":[],"class_list":["post-1906","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-bsg"],"jetpack_featured_media_url":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-content\/uploads\/2020\/10\/Default-Featured-Image-2020.jpg","_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/1906","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=1906"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/1906\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":1907,"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/1906\/revisions\/1907"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/media\/1561"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=1906"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=1906"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=1906"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}