{"id":1951,"date":"2023-02-17T19:38:56","date_gmt":"2023-02-17T23:38:56","guid":{"rendered":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/?p=1951"},"modified":"2023-02-17T19:38:56","modified_gmt":"2023-02-17T23:38:56","slug":"hakuna-kizuizi-dhidi-ya-rehema","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/archives\/1951","title":{"rendered":"Hakuna Kizuizi Dhidi ya Rehema"},"content":{"rendered":"<p><strong>Hakuna Kizuizi Dhidi ya Rehema ya Mungu<\/strong><\/p>\n<p>Kila Neno: MT- 101A, (Mathayo 1:1-17)\/ Neno Muhimu: genea (1:1) Vizazi<\/p>\n<hr \/>\n<p>\u201cBasi vizazi vyote tangu Ibrahimu hata Daudi ni vizazi kumi na vinne; na tangu Daudi hata ule uhamisho wa Babeli ni vizazi kumi na vinne; na tangu ule uhamisho wa Babeli hata Kristo ni vizazi kumi na vinne.\u201d (Mathayo 1:17)<\/p>\n<p>Nasaba ya Yesu Kristo, miongoni mwa mambo mengine, huwakilisha rehema tukufu ya Mungu. Kama unavyojua, kupata majina ya wanawake katika nasaba za kibiblia siyo kawaida. Lakini hapa, katika ukoo wa Yesu Kristo, inashangaza kuona majina manne yameandikwa katika ubini wa kike. Soma Mathayo 1:1-2, 3-6. Hao wanne ni Tamari, Rahabu, Ruthu, na Bath-sheba.<\/p>\n<p>[a] Yuda alifanya mapenzi maharimu na <strong>Tamari<\/strong>. Tamari alikuwa mshawishi na mzinzi (Mwa. 38:24). Yuda mwana wa Yakobo alikuwa na wana watatu: Eri, Onani na Shela. Mwanamke anayeitwa Tamari aliolewa na Eri, lakini Eri akafa, akamwacha mjane. Kwa kuwa ilitakiwa kwamba jamaa anayefuata amtunze mjane wa nduguye, Tamari alikabidhiwa kwa Onani, lakini naye akafa. Shela alikuwa bado mvulana mdogo na hangeweza kumwoa Tamari, kwa hiyo Yuda akamsihi arudi nyumbani kwa baba yake na kungoja hadi Shela awe mtu mzima. Hata hivyo, Yuda hakuheshimu ahadi yake mara tu Shela alipokuwa na umri wa kutosha. Na hivyo, Tamari alibaki kuwa mwanamke asiyeolewa (au mjane). Siku moja, Tamari akaenda mjini, akijifanya kuwa kahaba. Kwa kumhadaa Yuda, akamnasa na kulala naye. Kisha akapata mimba ya Yuda na kuwazaa wana mapacha walioitwa Peresi na Zera.<\/p>\n<p><u>Taarifa ya Kushangaza<\/u>: Jina Peresi katika Kiebrania humaanisha \u201c<u>uvunjaji<\/u>\u201d au \u201cyule anayeibuka ghafla,\u201d na hurejelea jinsi alivyozaliwa. Peresi, ambaye sasa alikuja kuwa mmoja wa wana wa Yuda &#8212; kupitia mahusiano haramu na mkamwana wake, Tamari &#8212; ameorodheshwa kama akraba wa Mfalme Daudi, lakini muhimu zaidi, Mfalme Daudi mkuu zaidi (Bwana Yesu Kristo).<\/p>\n<p>[b] <strong>Rahabu <\/strong>alikuwa kahaba aliyeokolewa kutoka kwenye hukumu ya Yeriko kwa sababu alionesha imani katika Mungu wa Israeli (Yos. 2:1-2). Soma kuhusu kukiri kwake katika Yos. 2:8, 9, 10, 11, 12, 13. Rahabu alikuwa Mmataifa, na katika siku hizo, hapakuwepo muungano wowote kati ya Wamataifa na Wayahudi (kama vile Wasamaria katika Yohana 4). Lakini kwa sababu ya imani yake, aliingizwa katika familia ya Mungu (Ebr. 11:31; Yak. 2:25)<\/p>\n<p>[c] <strong>Ruthu <\/strong>Ruthu alikuwa raia wa taifa lililochukiwa na Wayahudi, lakini alikuwa mwanamke aliyechagua kuambatana na Mungu wa Waebrania na watu Wake (Ruthu 1:1-4).<\/p>\n<p>[d] Kila mtu anajua kuhusu <strong>Bathsheba<\/strong> ambaye Daudi alizini naye (2 Sam. 11:1, 2, 3, 4, 5). Swali linaulizwa mara nyingi: Je, Daudi alimbaka Bathsheba? Hapana. Ndiyo, Daudi alitumia fursa yake dhidi ya Bathsheba, lakini hakumbaka. Hakuna jambo lolote katika Biblia linaloonesha kwamba Daudi alitumia nguvu, vitisho, au ukatili dhidi ya Bathsheba. Bathsheba alifanya dhambi kwa makusudi pamoja na Daudi, lakini alitafuta msamaha wa Mungu pamoja na Daudi (2 Sam. 12:13, 14). Bwana alimwadhibu Daudi. Mtoto ambaye mke wa Uria alimzalia Daudi alikufa, lakini Mungu hakuwa amemalizana na Bathsheba kwa sababu alimbariki na kumpatia mwana mwingine, Sulemani (2 Sam. 12:24), ambaye angekuwa mfalme wa Israeli baada ya Daudi. Haleluya?<\/p>\n<p>Biblia inasema kwamba Kristo alifanywa kuwa \u201cdhambi kwa ajili yetu,\u201d Yeye ambaye hakuijua dhambi. Pia alifanywa \u201claana kwa ajili yetu.\u201d Naye \u201califanywa katika mfanano wa mwili was dhambi\u201d (soma 2 Kor. 5:21; Gal. 3:13; Rum. 8:3). Angalia kirai hicho tena, \u201ckufanywa katika mfanano wa mwili wa dhambi.\u201d Inawezekanaje Mwanakondoo wa Mungu asiye na doa azaliwe katika hali hii? Kristo alijitwalia udhaifu wa asili yetu ya dhambi. Wakati wa kufanyika mwili, aliutwaa mwili huuhuu \u2013\u201cnyama na damu\u201d (Ebr. 2:14) kama tu sisi (wadhambi) tulivyo, na bado alishinda (Heb 4:15). <strong>Wazo kuu ni hili:<\/strong> watu wote walioorodheshwa katika nasaba hii walikuwa wadhambi (Rum 3:23), waliokolewa kwa Neema. Lakini Mungu aliruhusu waorodheshwe hapa kama somo kwetu\u2014rehema Yake inafikishwa kwa kila mtu.<\/p>\n<p>Wanawake hawa wanne, kwa namna mahususi, hutumika kama <u>onesho la neema ya Mungu (fadhili na rehema) kwa wadhambi<\/u>. Mpendwa, hakuna vikwazo vyovyote dhidi ya rehema ya Mungu. Mungu atamrehemu mtu yeyote, \u201cyeyote atakaye\u201d\u2014licha ya dhambi, historia, jinsi, taifa, au tabaka la kijamii. Huu ndio ujumbe wa Injili: Haijalishi tumetangatanga mbali kiasi gani (Luka 15:20-21). Tunamporudia Yesu na kutubu dhambi zetu, Yeye hutusamehe na kutukubali kama watoto Wake. Hebu Mungu atusaidie kadiri tunapoitikia wito Wake. Katika jina la Kristo, tunaomba, Amina.<\/p>\n<hr \/>\n<p>&nbsp;<\/p>\n<p><strong>Sauti ya Injili<\/strong>: \u201cAlituokoa, <u>si kwa sababu<\/u> ya mambo ya haki tuliyoyatenda, <u>bali kwa sababu wa rehema Yake<\/u>. Aliziosha dhambi zetu, akatupa kuzaliwa upya na maisha mapya kupitia Roho Mtakatifu.\u201d (Titus 3:5, NLT)<\/p>\n<p>&nbsp;<\/p>\n<p><em>Mfululizo wa Podikasti katika Injili ya Mathayo: Dakika Kumi na Yesu kila Alfajiri\/ Neno la Leo: genea (1:1) Vizazi<\/em><\/p>\n<p>&nbsp;<\/p>\n<div class='share-to-whatsapp-wrapper'><div class='share-on-whsp'>Share on: <\/div><a data-text='Hakuna Kizuizi Dhidi ya Rehema' data-link='https:\/\/tgvs.org\/injili\/archives\/1951' class='whatsapp-button whatsapp-share'>WhatsApp<\/a><div class='clear '><\/div><\/div>","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Hakuna Kizuizi Dhidi ya Rehema ya Mungu Kila Neno: MT- 101A, (Mathayo 1:1-17)\/ Neno Muhimu: genea (1:1) Vizazi \u201cBasi vizazi vyote tangu Ibrahimu hata Daudi ni vizazi kumi na vinne; na tangu Daudi hata ule uhamisho wa Babeli ni vizazi kumi na vinne; na tangu ule uhamisho wa Babeli hata Kristo ni vizazi kumi na <a class=\"read-more-link\" href=\"https:\/\/tgvs.org\/injili\/archives\/1951\"><br \/>&#8230;read more<\/a><\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":1561,"comment_status":"closed","ping_status":"closed","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"om_disable_all_campaigns":false,"_monsterinsights_skip_tracking":false,"_monsterinsights_sitenote_active":false,"_monsterinsights_sitenote_note":"","_monsterinsights_sitenote_category":0,"footnotes":""},"categories":[32],"tags":[],"class_list":["post-1951","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-dakika-10-na-yesu"],"jetpack_featured_media_url":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-content\/uploads\/2020\/10\/Default-Featured-Image-2020.jpg","_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/1951","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=1951"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/1951\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":1952,"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/1951\/revisions\/1952"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/media\/1561"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=1951"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=1951"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=1951"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}