{"id":1961,"date":"2023-04-03T07:57:48","date_gmt":"2023-04-03T11:57:48","guid":{"rendered":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/?p=1961"},"modified":"2023-04-03T07:57:48","modified_gmt":"2023-04-03T11:57:48","slug":"mtini-tasa-walaaniwa","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/archives\/1961","title":{"rendered":"Mtini Tasa Walaaniwa"},"content":{"rendered":"<p>Aya za Biblia Kuhusu\u2026<br \/>\n<span style=\"color: #0000ff;\"><strong>Mtini Tasa Walaaniwa<\/strong><\/span><br \/>\n101-BVA, (Mathayo 21:18-22)<br \/>\nLengo: Imani Ihamishayo Mlima!<\/p>\n<p>\u201cHata asubuhi alipokuwa akienda mjini, aliona njaa. Akaona mtini mmoja kando ya njia, akauendea, asione kitu juu yake ila majani tu; akauambia, Yasipatikane matunda kwako tangu leo hata milele. Mtini ukanyauka mara. Wanafunzi walipoona, walistaajabu, wakisema, Jinsi gani mtini umenyauka mara? Yesu akajibu, akawaambia,<span style=\"color: #ff00ff;\"> Amin, nawaambia Mkiwa na imani, msipokuwa na shaka,<\/span> mtafanya si hilo la mtini tu, lakini hata mkiuambia mlima huu, Ng&#8217;oka, ukatupwe baharini, litatendeka. <span style=\"color: #ff0000;\">Na yoyote mtakayoyaomba katika sala mkiamini, mtapokea<\/span>.\u201d (Mathayo 21:18\u201322)<\/p>\n<p><strong>Matumizi Maishani:<\/strong> Ikiwa tuna imani\u2014imani thabiti kwa Mungu Mweza Yote, bila kuwa na shaka, na kuamini kwamba Yeye anatusikia, tunaweza kuihamisha milima! Imani ni muhimu ili kumpendeza Mungu. Katika sura ya kumi na moja ya Waebrania, tunaona jinsi ambavyo watu hao wa Agano la Kale waliona maajabu yaliyofanywa kwa imani. Habili, Henoko, Nuhu, Ibrahimu, Sara (aliyejifungua akiwa na umri wa miaka 90), na hata Rahabu, kahaba, walimwamini Yehova, Mungu wa Biblia, naye akaokolewa wakati wa anguko la Yeriko! Iwapo Mungu anaweza kuheshimu imani ya Rahabu asiye muumini, vipi kuhusu wewe? Je, wewe si mtoto Wake?\u2014 (Linganisha Mathayo 6:30). Lakini ngoja kidogo\u2014hivi unaomba kwa imani? Na kumbuka, \u201cimani pasipo matendo imekufa\u201d (Yak 2:17). Imani na Utii vinaenda pamoja (Rum. 1:5; Ufu 14:12).<\/p>\n<p>Tunahitaji kukumbuka mambo kadhaa ili Mungu ajibu maombi yetu. Kwanza, kuungama\/kutubu dhambi; usadikisho wa ukweli kwamba chochote kinachoombwa kiko ndani ya eneo la mapenzi ya Mungu; sala ya dhati na ya kudumu kutoka moyoni; imani katika Neno la Mungu (ahadi) juu ya kile kinachoombewa; mwisho, imani ihamishayo Mlimani, ambayo \u201chuamini\u201d matokeo ya dua inayowasilishwa kwa Mwenyezi Mungu hata kabla ya ombi hilo mahususi \u201ckupokelewa,\u201d kujibiwa, au kubainika maishani. Ndiyo maana \u201chaki\u201d ilihesabiwa (ilihawilishwa kwenye akaunti ya Ibrahimu) kwa sababu aliamini na kupokea ahadi husika\u2014ahadi zilizomshikilia Masihi ajaye (Mwa 12:3; 15:5; Rum 4:3). Beloved, today God desires that we demonstrate such faith. Je, utafanya hivyo?<\/p>\n<p>Angalia hatua tatu za Utekelezaji wa Imani (Mat 21:22):<br \/>\nA. <strong>Omba\u2014<\/strong> \u201cOmbeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa.\u201d (Mathayo 7:7)<\/p>\n<p>B.<strong> Amini\u2014<\/strong> \u201cBasi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.\u201d (Waebrania 11:1)<\/p>\n<p>C. <strong>Pokea\u2014<\/strong> \u201cNiite, Nami nitakuitikia, Nami nitakuonesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua.\u201d (Yeremia 33:3)<\/p>\n<hr \/>\n<p>&nbsp;<\/p>\n<p>Hilo ni somo letu la \u201cTGV Kila Siku.\u201d Hadi wakati ujao, Hesabu Baraka zako nyingi!<\/p>\n<div class='share-to-whatsapp-wrapper'><div class='share-on-whsp'>Share on: <\/div><a data-text='Mtini Tasa Walaaniwa' data-link='https:\/\/tgvs.org\/injili\/archives\/1961' class='whatsapp-button whatsapp-share'>WhatsApp<\/a><div class='clear '><\/div><\/div>","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Aya za Biblia Kuhusu\u2026 Mtini Tasa Walaaniwa 101-BVA, (Mathayo 21:18-22) Lengo: Imani Ihamishayo Mlima! \u201cHata asubuhi alipokuwa akienda mjini, aliona njaa. Akaona mtini mmoja kando ya njia, akauendea, asione kitu juu yake ila majani tu; akauambia, Yasipatikane matunda kwako tangu leo hata milele. Mtini ukanyauka mara. Wanafunzi walipoona, walistaajabu, wakisema, Jinsi gani mtini umenyauka mara? <a class=\"read-more-link\" href=\"https:\/\/tgvs.org\/injili\/archives\/1961\"><br \/>&#8230;read more<\/a><\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":1561,"comment_status":"closed","ping_status":"closed","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"om_disable_all_campaigns":false,"_monsterinsights_skip_tracking":false,"_monsterinsights_sitenote_active":false,"_monsterinsights_sitenote_note":"","_monsterinsights_sitenote_category":0,"footnotes":""},"categories":[35],"tags":[],"class_list":["post-1961","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-aya-za-biblia-kuhusu"],"jetpack_featured_media_url":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-content\/uploads\/2020\/10\/Default-Featured-Image-2020.jpg","_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/1961","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=1961"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/1961\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":1962,"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/1961\/revisions\/1962"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/media\/1561"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=1961"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=1961"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tgvs.org\/injili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=1961"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}