Tubuni; Mfalme Yu Mlangoni.

April 3, 2023 in Amri Katika Agano Jipya by TGVS

Tafakari ya Dakika Mbili
Amri katika Agano Jipya
Tubuni; Mfalme Yu Mlangoni.
101A-NTC, (Mathayo 3:1–2)

“Siku zile aliondokea Yohana Mbatizaji akihubiri katika nyika ya Uyahudi, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.” (Mathayo 3:1-2)

Toba ni kugeuza mwelekeo—kutoka dhambini na kumuelekea Mungu. Kwa hivyo, mahubiri ya Yohana yalikuwa neno moja tu, “tubuni,” lakini kwa nini? “Kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.” Huwezi kuwa na ufalme bila Mfalme. Mfalme huyu ni Bwana Yesu Kristo. Toba ya kweli ni mojawapo ya sifa muhimu za uraia wa Ufalme wa Mbinguni. Kristo alikuja kuanzisha Ufalme (Mt 6:10), Ufalme wa Neema, ambao punde utafuatwa na Ufalme wa Utukufu, wakati wa Ujio wa Pili, wakati itakapoonekana “ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi. Naye atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda, nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu.” (Mathayo 24:30-31)

Wapendwa, mfalme anakuja, lakini Je Umetubu dhambi zako? Labda unasema, “Tunaokolewa kwa neema tu; Mungu ni mwenye upendo na neem ana huruma nyingi, hatawahukumu wanadamu kwa ajili ya dhambi zao.” Fikiria tena. Usidanganukike mpendwa. Mtume Paulo anaandika, “Tuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi? Hasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi? Kwa maana dhambi haitawatawala ninyi, kwa sababu hamwi chini ya sheria, bali chini ya neema.” (Warumi 6: 1-2, 14). Kisha katika sura ya 14, anatoa kauli hii ya kushangaza, “Basi, kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu.” (14:12)

Inaonekana kwamba Mungu hatanii, humaanisha anpowataka binadamu wote watubu. Sikiliza mpendwa, hakuna mtu ye yote atakayerithi ufalme wa Mungu akingali katika dhambi zake. Soma Aya zifuatazo – (1 Wakorintho 6:9-10; 15:50; Zaburi 34:16; 37:9; Mathayo 25:34, 41; Yohana 3:3; Warumi 1:29-32; Wagalatia 5:21; Waefeso 5:5; Waebrania 12:14; Ufunuo 21:8). Itakuwa busara sana sasa kushughulikia “kila chembechembe ya dhambi” katika maisha yetu kabla ya mlango wa rehema kufungwa na kukosa Mwombezi (Ufunuo 22:11). Wapendwa, wakati pekee tulio nao ni leo (Waebrania 3: 7,15). Fanya uamuzi sahihi leo—Tubu dhambi zako!

Kwa Uwajibikaji binafsi siku ya Hukumu, angalia Maandiko yafuatayo-
A. Mathayo 12:36
B. Mathayo 16:27
C. 1 Petro 4:5
D. Mhubiri 11:9


Hilo ndilo somo letu la “TGV Daily.” Hadi Wakati Mwingine— Bwana Akubariki.

Masomo haya yameandaliwa na The Gospel’s Voice Ministries| P.O. Box 1058, Cordova, TN 38088, USA| Haki zote zimehifadhiwa.

Comments