Uavyaji Mimba.
April 3, 2023 in Dhambi za Kuungama by TGVS
Dhambi za Kuepuka au Kuungama.
Uavyaji Mimba.
101A-SAC, (Yeremia 1:4–5)
“Neno la Bwana lilinijia, kusema, Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.” (Yeremia 1:4–5)
Uchunguzi: Mungu huwashutumu wale wanaoondoa uhai (Kut. 20:13; 2 Wafalme 1:13; Amosi 1:13–14)
Tafakari: Uavyaji Mimba ni nini? “Kutoka Kilatini abortio, “mimba kuharibika,” neno hili hutumika katika maana mbili: 1. Uavyaji faradhi ni kitendo asili ya kupoteza mimba au kumzaa mtoto kabla ya wakati wake, hivyo kusababisha upotevu wa uhai wake. 2. Uavyaji dhamirifu ni kumwondoa kwa kusudi kitoto tumboni, hivyo kuangamiza uhai wake.” [Alan Cairns, Dictionary of Theological Terms, 2002, 4.]
Biblia inasema nini kuhusu uavyaji mimba? “Biblia huweka thamani kubwa kwenye uhai wa mwanadamu, ikiwa ni pamoja na ule wa mtoto ambaye hajazaliwa. Mafundisho ya Biblia hubaini kwamba maisha ni takasifu, ni tunu itokayo kwa Mungu (Mwa. 1:26–27; 2:7; Kumb. 30:15–19; Ayubu 1:21; Zab. 8:5; 1 Kor. 15:26), hususan uhai wa watoto (Zab. 127:3–5; Luka 18:15–16), na huwashutumu wale wanaouondoa (Kut. 20:13; 2 Wafalme 1:13; Amosi 1:13–14). Makuzi ya uhai wa mtoto tumboni huongozwa na Mungu (Ayubu 31:15; Zab. 139:13–16; Mhu. 11:5; Isa. 44:2; 46:3; 49:5; Yer. 1:5; Luka 1:15; Gal. 1:15). Unasibu wa astafali (kitoto tumboni) hufundishwa bayana katika Kut. 21:22 ambako asiyezaliwa huitwa “mtoto” (yeled) badala ya “astafali” (nephel au golem). Hos. 9:11 humaanisha kwamba uhai huanza wakati wa mimba kutungwa, wakati ambapo Luka 1:41, 44 hubaini utambuzi wa mtoto asiyezaliwa bado.” [Paul H. Wright, Holman Illustrated Bible Dictionary, 2003, 10.]
Maana Ya Kiibada: Ni mwitikio gani unaodhani sura hii ingepaswa kutuhimiza kufanya? Kumbuka kwamba …. [1] Mungu alitujua kabla hajatuumba tumboni; [2] Mungu alifanya kazi amilifu katika uumbaji wetu na kutengeneza mjizazi (Zaburi 139:13-16); [3] Mungu humchukulia mtoto tumboni kama mwanadamu yeyote tu mwenye umri wa utuzima. [4] Kwa waumini, uavyaji siyo suala la haki ya mwanamke kuchagua. Ni suala la uzima au mauti ya mwanadamu aliyeumbwa kwa sura ya Mungu (Mwanzo 1:26-27; 9:6); [5] Mungu huchukia aina zote za mauaji, ikiwa ni pamoja na watoto ambao hawajazaliwa; [6] Utii wa Amri ya Sita: Usiue. (Kut. 20:13) Kwa uchunguzi zaidi kuhusu mada ya uuaji, tafadhali soma: Mwa. 4:8-15, 23; 9:5-6. 27:41, 45; 49:6; Kut. 21:12, 14, 20, 29; 22:2-3; Zab. 10:8-11; 51:14; Mit. 1:11, 18; 28:17; Isa 1:15. 26:21; Yer. 26:15; Mat 5:21-22; 15:19; 19:18; Ufu. 16:6; 17:6; 21:8; 22:15.
Maungamo Ya Dhambi Zetu: Baba, tunakushukuru kwa kutukumbusha tena kwamba uhai ni takasifu, tunu itokayo Kwako, kwamba wana thamani hata kabla hawajazaliwa. Baba, ulitujua, kama ulivyomjua Yeremia, muda mrefu kabla hatujazaliwa au hata mimba yetu kutungwa. Nataka kwa namna mahususi kuwaombea wale ambao wamewahi kutoa mimba: mwanamke ambaye ametoa mimba, mwanamume ambaye amehamasisha utoaji mimba—au hata daktari ambaye ametekeleza jambo hilo. Hebu wakumbuke kwamba uavyaji mimba haina una msamaha siyo pungufu ya dhambi nyingine; maana umesema: “Kila dhambi na kila neno la kufuru [kila uovu, mazungumzo hasirifu na dhurifu, au utwezaji wa mambo matakatifu] watasamehewa wanadamu, ila kwa kumkufuru Roho hawatasamehewa” (Mat 12:31). Tusamehe kwa pamoja kwa dhambi hii, Bwana! Kadiri tunavyoanza mwaka mwingine, hebu tuenende kadiri ya nuru ambayo umetupatia katika neno Lako takatifu. Asante kwa kutusamehe dhambi zetu, makosa yetu, na udhalimu. Tusafishe, tutakase, na kutuandaa kwa ajili ya ufalme Wako. Njoo Bwana Yesu maishani mwetu, katika jina la Yesu, tunaomba, Amina.
Iweni na Siku Yenye Baraka! “Maana Wewe ndiwe uliyeniumba mtima wangu, Uliniunga tumboni mwa mama yangu. Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa Kwa jinsi ya ajabu ya kutisha. Matendo yako ni ya ajabu, Na nafsi yangu yajua sana.” (Zaburi 139:13–14)
Mwaka wa Uamsho & Matengenezo—Ibada, Maombi & Maungano. “Kwa sababu hiyo ninyi nanyi [mnaonifuata Mimi] jiwekeni tayari; kwa kuwa katika saa msiyodhani Mwana wa Adamu yuaja.” (Mat 24:44, AMP)
Hilo ndilo somo letu la “TGV Daily.” Hadi Wakati Mwingine— Bwana Akubariki.
Masomo haya yameandaliwa na The Gospel’s Voice Ministries| P.O. Box 1058, Cordova, TN 38088, USA| Haki Zote Zimehifadhiwa.