Hesabu 16: Mwongozo wa Maombi
August 27, 2025 in Mwongozo wa Maombi by TGVS
4-BSG-16B: MWONGOZO WA MAOMBI
Mwongozo wa Kujifunza Biblia/ Hesabu 16: Mwongozo wa Maombi/ 4-BSG-16B (Hesabu 16)/ Mada Kuu: Kuomba kwa ajili ya unyenyekevu, utii, na kumcha Mungu mbele ya uasi na kiburi.
Tabia za Kukuza:
Unyenyekevu mbele za mamlaka ya Mungu.
Uaminifu katika uongozi na huduma.
Maombezi kwa ajili ya wengine, hata kwa waasi.
Kumcha Mungu kwa utakatifu Wake.
Umoja na amani miongoni mwa watu wa Mungu.
Dhambi za Kuepuka/ Kuungama:
Kiburi na uasi, kama vile Kora, Dathani, na Abiramu (Hes. 16:1–3).
Kunung’unika na kulalamika dhidi ya viongozi wa Mungu (Hes. 16:41).
Kupuuza utakatifu wa Mungu.
Kupinga utaratibu na nidhamu ya Mungu.
Jambo la Kumshukuru Mungu: Mshukuru Mungu kwa—
Viongozi kama Musa na Haruni waliowaombea watu waasi.
Utakatifu Wake unaolinda watu Wake.
Kristo, Kuhani wetu Mkuu, anayesimama kati ya walio hai na wafu (Waebrania 7:25).
Watu wa Kuombea:
Viongozi wa kiroho—wachungaji, wazee, walimu—waende kwa unyenyekevu na uaminifu.
Waumini wanaoshindwa na kiburi au uasi, ili watubu.
Kanisa lisimame kwa umoja ndani ya Kristo.
Waombezi waaminifu (intercessors) Mungu awatie nguvu.
Mambo ya Kuombea:
Amani, umoja, na utii kwa mpangilio wa Mungu kanisani.
Ulinzi dhidi ya mgawanyiko na uongozi wa uongo.
Ujasiri wa kusimama imara kwa utakatifu na kweli.
Rehema juu ya jamii na mataifa yanayopinga mamlaka ya Mungu.
Uamsho—mioyo iliyonyenyekea mbele ya Neno la Mungu.
Dhamira Ya Leo— (Kwa Neema ya Mungu, naahidi/ najitolea):
Kutembea kwa unyenyekevu na kuacha kiburi.
Kuwaombea na kuunga mkono viongozi aliowaweka Mungu.
Kuwaombea wengine, hata wanaopinga.
Kuishi kwa kumcha Mungu katika utakatifu wake.
Ahadi Ya Bwana: “Ikiwa watu Wangu, waliotajwa kwa Jina Langu, watajinyenyekeza na kuomba, na kutafuta uso Wangu, na kuziacha njia zao mbaya; ndipo nitasikia toka mbinguni, Nami nitawasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.” (2 Mambo ya Nyakati 7:14)
Maombi Maalum— (Prayer Requests);
(Endapo una mzigo wowote, uandike hapo chini, tutaliombea):
[1] _________________________
[2] _________________________
SALA YA ASUBUHI (Linaloshabihiana na Hesabu 16):
Baba wa Mbinguni, tunakuja mbele Zako asubuhi hii tukiwa na mioyo yenye unyenyekevu, tukiomba hekima na ufahamu tunapofungua Hesabu 16. Bwana, utulinde dhidi ya roho ya uasi iliyoinuka kwa Kora, Dathani, na Abiramu. Utupatie mioyo ya unyenyekevu inayoheshimu mamlaka Yako na kuwaenzi viongozi uliowaweka.
Baba, tusamehe kwa nyakati ambazo tumenung’unika, kulalamika, au kupinga mapenzi Yako. Tutasafishe na kutuondolea kiburi na majivuno, na kutuvika roho ya utii.
Tunakushukuru kwa viongozi ambao—(kama Musa na Haruni)— waliwaombea watu Wako. Zaidi ya yote, tunakushukuru kwa Kristo Yesu, Kuhani wetu Mkuu, anayesimama kati ya hukumu na rehema, akitoa wokovu kwa wote waaminio.
Asubuhi hii, tunaomba umoja katika kanisa letu, unyenyekevu katika mioyo yetu, na uamsho katika jamii zetu. Tufundishe kuishi kwa kumcha Mungu katika utakatifu Wake na kusimama kama waombezi wa kweli. Hebu siku hii ya leo, kwa uwezo wa Roho Wako, tukatembee katika Neno, utii, na kicho mbele Zako. Na somo la leo (Hesabu 16) likapate kuwa mbaraka kwa kila mmoja wetu.
Tunaomba haya yote kwa Jina la thamani, Jina pekee la Yesu Kristo Bwana wetu. Amina.