Hesabu 16: Wazo la Usiku
August 27, 2025 in Usiku by TGVS
4-BSG-16Y.2: IBADA YA USIKU
Mwongozo wa Kujifunza Biblia/ Hesabu 16 (4-BSG-16Y.2)/ Wazo la Usiku/ Kadiri siku hii inavyofika mwisho, kaa kidogo na ruhusu maswali haya yaongoze moyo wako mbele za Bwana:
MASWALI YA KUJIHOJI NA TAFAKARI YA USIKU
[1] Ni wapi katika maisha yangu ninashawishika kupinga mapenzi ya Mungu au mpangilio Wake, na ninawezaje kujisalimisha kikamilifu usiku huu? (Hes. 16:1–3; Math. 6:10)
[2] Ninapowaona wengine wakiheshimiwa au kuitwa kutumikia, je, nawadhihaki kwa wivu kama kundi la Kora, au ninashukuru kwa tuzo (karama) ambazo Mungu huwapa? (Hes. 16:9–10; 1 Kor. 12:18–20)
[3] Ninajibu vipi Mungu anapokabiliana nami kwa kweli? Je, ninainama kwa unyenyekevu kama Musa, au nabishana kama waasi? (Hes. 16:4; Mit. 15:31–33)
[4] Je, niko tayari kusimama “kati ya walio hai na waliokufa” katika maombi kwa ajili ya familia, marafiki, na jamii yangu, kama Haruni alivyofanya? (Hes. 16:46–48; Ezek. 22:30)
[5] Ni manung’uniko au malalamiko yapi yametoka katika midomo yangu leo? Je, naweza kuyabadilisha kuwa shukrani kabla ya kulala? (Hes. 16:41; Wafil. 4:6)
[6] Je, ninatambua uzito wa dhambi na utakatifu wa Mungu, au namchukulia kwa wepesi? (Hes. 16:30–35; Ebr. 12:28–29)
[7] Ni ushuhuda upi wa utukufu na rehema ya Mungu nimeuona leo, na je, nimepata muda wa kumshukuru? (Hes. 16:19; Zab. 103:2)
[8] Ni kwa jinsi gani Kristo, Kuhani wangu Mkuu, amesimama pengoni (‘in the gap”) kwa ajili yangu leo, na ninawezaje kumheshimu kwa imani ya kina zaidi? (Ebr. 7:25; Rum. 8:34)
[9] Je, kuna kiburi, uasi, au kutokuwa na shukrani maishani mwangu—(usiku huu kabla sijalala). Je ninayo shauku yoyote ya kukiri na kutubu dhambi hizi? (1 Yoh. 1:9)
[10] Je kwa Neema ya Mungu naweza kuanza siku mpya ya kesho kwa tofauti—nikiishi kwa unyenyekevu, shukrani, na maombezi—ili masomo ya leo yakazae matunda, na niwe nimepiga hatua mpya ya safari yangu ya imani? (Mika 6:8; Efe. 5:15–16)
Muhtasariw a Tafakari ya Usiku huu:
Uasi wa Kora unanikumbusha kwamba dhambi huleta mauti, lakini maombezi ya Haruni yanaashiria Kristo, anayesimama pengoni ili kunipa uzima. Usiku huu, sipumziki kwa nguvu zangu bali kwa rehema Yake, nikichagua unyenyekevu, shukrani, na maombi huku nikijiandaa kwa siku mpya pamoja Naye.