Yusufu: Jinsi ya Kushinda Majaribu

February 21, 2022 in Mwongozo wa Ibada by TGVS

Mwanzo 39: Mwongozo wa Ibada/ 1-BSG-39A, (Mwanzo 39:1-23)/ Dhima: Yusufu katika Nyumba ya Potifa/ Wimbo: “Nataka Imani hii: Imani imara” (NK 79)


Uchunguzi: Jinsi ya Kushinda Majaribu Makuu— (Efe. 6:11, 13-17; Yak. 4: 7; 2 Tim 2:22; Mwa. 39: 6-12; Marko 14:38; 1 Pet 5:8-9; 1 Kor. 10:13).

Tafakari: Yusufu alijaribiwa kufanya mapenzi na mke wa bwana wake (v. 7). Kijana ambaye hajaongoka angejitwalia fursa hii mara hiyo, lakini si Yusufu. Sasa, kwa nini Yusufu anaikataa awani hiyo? Kwa sababu hataki kuvunja dhamani ya bwana wake (8b); Kwa sababu hapaswi kufanya uovu mkuu kama huo: Mapenzi haramu ni uovu (9a); Kwa sababu lazima asimtende Mungu dhambi (9b). Yusufu alijaribiwa vikali siku baada ya siku, lakini alijifunza kuinidhamisha nafsi yake. Alijifunza kujikana nafsi: kudhibiti mwili wake na tamaa zake (10a-b). Mtume Paulo anauita mchakato huu kuupatia mwili wangu kipigo na kuufanya uwe mtumwa wangu.” (1 Kor. 9:27, NIV). Mpendwa, hili linawezekana pale tu tunapo “visalimisha viungo vyetu” viwe chini ya Roho Mtakatifu (Rum. 6:13). Ni uchaguzi, vita endelevu vinavyohitaji maombi ya kudumu. Siku moja, Yusufu alipokuwa “akifanya majukumu yake” peke yake nyumbani, alinaswa na kushambuliwa: Mke wa Potifa alikuwa amejaribu kumfanya Yusufu atende dhambi pamoja naye. Yusufu alikimbia jaribu hilo haraka sana kiasi kwamba akaliacha vazi lake (11-12). Yusufu alipokataa kufanya hivyo, mwanamke huyo akatunga uongo wa kumsingizia. Yusufu alikabiliwa na kesi ya ubakaji na mashtaka ya uongo. Aliishia gerezani (v. 15-20). Lakini hata katika kifungo chake hiki cha hila, tunaona jinsi Mungu alivyokuwa pamoja na Yusufu. Alifanikiwa na akawekwa tena katika nafasi ya uongozi (v. 21-23). Katika sura zijazo tutaona jinsi alivyo pandishwa hadi kuwa Kiongozi mkuu katika nchi ya ugenini, Misri.

Maana ya Kiibada: Katika fasili ya 10, tunasoma kwamba Bi. Potifa alipendekeza kwa Yusufu “[kwa dhati] siku baada ya siku, lakini Yusufu hakusikiliza [vishawishi hivyo] alale naye.” (AMP) Jaribu hilo lilikuwa kubwa. Ellen G. White anaandika: kwa taharuki isiyoelezeka, malaika walitazama tukio hilo.” (PP. 217). Malaika walikuwa wanajiuliza iwapo Yusufu angejisalimisha kwenye jaribu hilo. Bila shaka, walifurahi alipochagua kumtii Mungu. Mapema katika sura hiyo, Bw. Potifa anakubali ukweli usiopingika kwamba Yusufu alikuwa mcha-Mungu (Mwa. 39:2-4). Katika katika tukio hili, Potifa hakumwamini mkewe. “Kama (Potifa) angeamini shutuma za mkewe dhidi ya Yusufu, huyo kijana Mwebrania angepoteza maisha yake; lakini staha na unyofu uliobainika sawia kwenye mwenendo wake ulikuwa uthibitisho wa kutokuwa na hatia; na hata hivyo, ili kutunza sifa ya nyumba ya bwana wake, alitelekwa kwenye fedheha na kifungo.” – (Ibid uk. 218).

Dondoo ya pili: Daima kuna gharama ya kulipa ili kutimiza ndoto! Je, unaikumbuka ndoto ya Yusufu katika Mwa. 37:5-7, 8, 9, 10-11? Fikiria vizuizi ambavyo amestahimili hadi sasa: kutoeleweka na familia yake; kuuzwa utumwani na ndugu zake wa damu; kuishi katika nchi ya kigeni, ya kipagani; kushutumiwa kimakosa kwa ubakaji; kutupwa gerezani kimakosa; kusahaulika na yule mnyweshaji mkuu; kukaa gerezani kwa miaka miwili zaidi. Lo! Mpendwa, Je ungefanya nini katika mfululizo huu wa matukio haya ya masahibu? Je, unatupilia mbali ndoto/ maono yako uliyopewa na Mungu? Sikilizeni, marafiki; Yusufu alipata nguvu za kuendelea na kamwe hakukata tamaa katika ndoto yake kwa sababu alijua kwamba Mungu alikuwa pamoja naye!” Mpendwa, wewe pia unaweza kuwa mtakatifu, mshindi na hodari kama Yusufu. Ndiyo, ndoto zako zinaweza kutimia! Uchaguzi ni wako: chagua kwa busara.

Sauti ya Injili: Sehemu hiyo imeandikwa kana kwamba Mungu anazungumza nawe moja kwa moja — kwa sababu Yeye hufanya hivyo. Bwana ananiambia nini asubuhi ya leo? Mwanangu, Dhambi ni hatari; inakutenga Nami (Isa. 59:1-2). Shetani anataka kukutega ili aweze kukuua (kuyaangamiza maisha yako), lakini Mimi nataka kukupa uzima: uzima tele, wenye ushindi, uzima wa milele (Yn. 10:10). Katika sura hii, Yusufu hashindwi na majaribu. Anatambua kwamba dhambi zote zinanichukiza (Zab. 51:4). Kunifuata haimaanishi kwamba hutakumbana na majaribu au dhiki –Utakabiliana nayo (2 Tim 3;12); lakini katika nyakati hizo, ukidumu kuwa waaminifu Kwangu, nitakupa Neema ya kustahimili na kushinda (1 Kor. 10:13; 2 Kor. 12:9; Ufu. 3:10), na mwishowe, bila kujali matokeo, utahesabiwa haki (Kumb. 32:36; Zab. 43:1; Luka 18:7). Ninakualika utii amri Zangu bila kujali hali na mazingira. Je ungependa kufanya hivyo?

Shauku Yangu: Kwa neema ya Mungu –

  1. Nataka kuwa mwangalifu kuzishika Amri zote za Mungu licha ya hali yoyote.
  2. Sitaki kuruhusu Vishawishi vizengee maishani mwangu na kufikia hatua ya kutodhibitika.
  3. Nataka kuomba ili kumsihi Mungu anipe Msaada katika nyakati za Dhiki na Majaribu makubwa
  4. Nataka kukabiliana na Majaribu kwa ujasiri: kuanza kutafuta “mlango wa kutokea” (1 Kor. 10:13)
  5. Nataka Kukesha na Kuomba daima ili nisiingie Majaribuni: “hakika roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu” (Mat. 26:41).
  6. Nataka kujifunza kuwa sawilifu (thabiti) katika makabiliano yangu dhidi ya dhambi: “Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.” (Yakobo 4:7)

Uwe na Siku Yenye Baraka: “Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili.” (1 Wakorintho 10:13)


 

Ibada Kupitia Uimbaji: “Nataka Imani hii: Imani imara” (NK 79)
1
Nataka Imani hii: Imani imara
Ambayo haitetemi Kitu chote Wakati wa shida,
Wakati wa shida.

2
Isiyonung‘unika Huzuni, taabu;
Lakini katika saa ya matata Humwamini Mungu,
Humwamini Mungu.

3
Imani inayo ng‘aa katika tufani;
Isiyoogopa giza, wala shida, Njaa na Hatari,
Njaa na hatari.

4
Haiogopi dunia, Kudharau kwake;
Haiangushwi na hila, na uwongo Dhambi na ogofyo,
Dhambi na ogofyo.

5
Bwana, nipe imani hii, Hivi nita weza
Kuonja hapa chini ulimwenguni, Kurithi furaha,
Kurithi furaha.

Comments