Imani ya Yoshua
July 25, 2022 in Usiku by TGVS
WAZO LA USIKU
Mwongozo wa Kujifunza Biblia/ 6-BSG-6Y, (Yoshua 6:6-7)/ Dhima: Imani ya Yoshua/ Wimbo: (Si Mimi, Kristo –NK 17).
YOSHUA AMTII MUNGU
Aya Kuu: “Bali Yoshua, mwana wa Nuni, akawaita makuhani, akawaambia, Lichukueni sanduku la agano, tena makuhani saba na wachukue tarumbeta saba za pembe za kondoo waume mbele ya sanduku la Bwana. Naye akawaambia watu, Piteni mbele, mkauzunguke mji, na hao watu wenye silaha na watangulie mbele ya sanduku la Bwana.” (Yoshua 6:6-7).
Yoshua alimwamuru makuhani wachukue Sanduku la Agano, na akawanga makuhani saba kuandamana mbele na Tarumbeta saba. Kisha akatoa amri kali kwa askari: Endelea mbele! Hebu zingatia msisitizo juu ya Sanduku, ishara ya uwepo na mwongozo wa Mungu.
Sanduku la Agano limetajwa zaidi ya mara 12 katika sura hii. Uwepo wa Mungu na mwongozo katika ushindi wa Yeriko unasisitizwa katika sura yote. Ushindi ulipaswa kupatikana kupitia uwepo, uongozi, na mwongozo Wake pekee. Ikiwa Yoshua na waisraeli wangemtii Bwana, wangewashinda adui zao. Lakini endapo wasingetii, wangeshindwa (chukuliwa mateka) na kufukuzwa katika nchi ya ahadi.
Hoja Kuu ni hii: “Imani Pasopo Matendo Imekufa.” Haitoshi kusema, “Ninamwamini Mungu,” na kisha kuishi kama unavyotaka. Ikiwa tunamwamini Mungu kweli, tutamtii. Imani yetu itawekwa (itadhihirishwa) kwenye matendo.. Tutafanya kile asemacho Mungu, na Tutazishika amri Zake.
Zingatia Maandiko yafuatayo, tunapohitimisha somo hili:
- “Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.” (Mathayo 7:21).
- Ndugu zangu, yafaa nini, mtu akisema ya kwamba anayo imani, lakini hana matendo? Je! Ile imani yaweza kumwokoa? (Yakobo 2:14)
- “Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja; watenda vema. Mashetani nao waamini na kutetemeka. Lakini wataka kujua, wewe mwanadamu usiye kitu, kwamba imani pasipo matendo haizai? (Yakobo 2:19-20)
- “Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu…. Basi, sasa inadumu Imani, Tumaini, Upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo.”(1 Wakorintho 13:3, 13)
Iweni na Usiku Mwema: “Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa.” (Yakobo 2:26)