Maombi: Yoshua 7
July 25, 2022 in Alfajiri, Mwongozo wa Maombi by TGVS
ANZA NA BWANA!
Jumanne: July 26, 2022.
Kipindi cha Ibada ya Maombi- (Alfajiri)
[1] “Naomba niombewe Bwana anipatie ratiba ya maombi na familia yangu” (SM); [2] “Umaliziaji wa Nyumba yangu ununuzi wa bati na mbao” (SM); [3] “Wadogo zangu Loius, Samweli, Neema & Veronica- Wapate kuifahamu kweli” (SM); [4] Ombea watendakazi wote waliyo shambani mwa Bwana; [5] Ombea huduma hii ya Injili: ili kwamba wengi waokolewe, waingie mbinguni; [6] Ombea fedha kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Uchapishaji; [7] Ombea wagonjwa, walemavu, wanaotengwa/ teswa na familia zao kwa ajili ya Injili; [8] Ombea ujasiri wa kumpinga Shetani & kuikataa dhambi: Katika sura ya leo (Yoshua 7), Israeli alishindwa kuuteka mji wa Ai kwa sababu ya dhambi. Durusu dhambi ya Akani (Yoshua 7:1).
SALA: Baba yetu mpendwa, tunatoa shukrani zetu za dhati kwa zawadi ya uhai tena leo. Sisi ni wadhambi, tena wasiofaa kabisa mbele Zako. Tusamehe Bwana na kutusafisha kwa damu ya Kristo. Tazama mahitaji yaliyoletwa hapa Bwana na ukatende sawasawa na fadhili Zako. Hebu Injili katika Yoshua 7, ikapate kubadilisha Maisha yetu, tunapojiandaa na marejeo ya Kristo. Tumeomba haya katika jina la Yesu Kristo, Nahodha wetu, Amina.
Je una Mzigo wowote? Je una Jambo la kumshukuru Bwana? Je unao Wimbo wowote? Je una Ushuhuda wowote? Karibu Mpendwa: Nafasi hii ni yako…
AHADI YA LEO/Dhima: Wokovu kwa Mdhambi.
“Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika Yeye.” (Yohana 3:17) – “Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa Yeye; maana Yu hai sikuzote ili awaombee.”(Waebrania 7:25)