Torati 23 (Ibada)

April 5, 2019 in Mwongozo wa Ibada by TGVS

MWONGOZO WA IBADA.
(“Mwongozo wa Ibada” unaoshabihiana na programu ya “Usomaji wa Biblia” kila siku)

April 6, 2019

Mwongozo wa Biblia
5-BSG-23A.1 (Torati 23)
“Njoni, Tuabudu, Tusujudu, Tupige magoti mbele za Bwana aliyetuumba.” (Zaburi 95:6)


 

UFUNGUZI WA IBADA.
Aya ya Mwitikio: Torati 23:9-14
Wimbo wa Ufunguzi: “Nataka nimjue Yesu.”

AHADI ZA MUNGU KWA AJILI YAKO.
Dhima: [Usafi wa Kituo (Nyumba) yako]
“Kwa kuwa Bwana, Mungu wako, yuatembea katika kituo akuokoe, na kukutolea adui zako mbele yako; kwa hiyo na kiwe kitakatifu kituo chako; asije akaona kitu kwako kisichokuwa safi, akageuka na kukuacha.” (Torati 23:14)

JAMBO LA KUMSHUKURU MUNGU.
(1) Mungu ana uwezo wa kugeuza laana kuwa baraka (5)
(2) Bwana, Mungu wako “anakupenda” (5)
(3) Bwana, atembelea kituo changu aniokoe (14)
(4) Bwana, anitolea adui zangu mbele yangu (14)
(5) Mibaraka: Bwana, atakubariki “katika yote utiayo mkono wako” (20)

WAJIBU/ UNGAMO/ USHUHUDA WOWOTE?
(1) “Lakini zaidi ya yote, ndugu zangu, msiape, wala kwa mbingu wala kwa nchi; wala kwa kiapo kinginecho chote; bali ndiyo yenu na iwe ndiyo, na siyo yenu iwe siyo, msije mkaangukia hukumu. (Yakobo 5:12)

(2) “Bali maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu.” (Mathayo 5:37)

DHAMBI ZA KUEPUKA/KUUNGAMA.
Dhambi (Dhambi Mahususi) → (Toari 23)
(1) Uashetari: “Pasiwe na kahaba katika binti za Israeli” (17)
(2) Uashetari: “Usilete ujira wa kahaba,.. katika nyumba ya Bwana” (18)
(3) Riba: “Usimkopeshe ndugu yako kwa riba; riba ya fedha, riba ya vyakula, kitu cho chote” (19)
(4) Nadhiri isiyotimizwa kwa Bwana (21-23)

Je unayo mambo yoyote ya kuombea? Yaandike hapa chini ~ (Angalia “Fomu ya Maombi”), au kwenye Blogu ya “Sauti ya Injili,” na mtu fulani atayaombea. Mlilie Bwana akusamehe dhambi hizi, kisha mwombee mtu fulani awe mshindi katika maeneo haya yaliyotajwa.

KUJIWEKA WAKFU:
Kwa neema ya Bwana, Leo ninaahidi kufanya yafuatayo:
(1) Nitajingatia maagizo ya Bwana katika Torati 23.
(2) Sitatafuta amani ya wadhambi, wala heri yao siku zangu zote, milele (6)
(3) Nitawaalika adui zangu “katika mkutano wa Bwana” (8)
(4) Nitajilinda na “kila neno baya” (9)
(5) Nitajitahidi kuimarisha usafi wa moyo, usafi wa mazingira katika nyumba (kituo) changu. (14)

SALA: Ee Bwana, nisaidie kuimarisha usafi wa moyo, usafi wa mazingira katika nyumba (kituo) changu; “usije akaona kitu kwangu kisichokuwa safi, ukageuka na kuniacha.” Nisaidie pia “nisiwe mlegevu katika kuiondoa’ nadhiri yangu kwako; kwa kuwa “hataacha kuitaka kwangu.” Nimeomba haya katika jina la Yesu Kristo, Bwana wetu, Amina.


 

UWE NA SIKU YENYE BARAKA! “Ni huruma za Bwana kwamba hatuangamii, Kwa kuwa rehema zake hazikomi. Ni mpya kila siku asubuhi; Uaminifu wako ni mkuu.” (Maombolezo 3:22–23)

 

Sauti Ya Injili SDA © 2019

Comments