Israeli Wateswa huko Misri

March 5, 2022 in Mwongozo wa Ibada by TGVS

Kutoka 1: Mwongozo wa Ibada/ 2-BSG-1A, (Kutoka 1:1-22)/ Dhima: Israeli Wateswa huko Misri/ Wimbo: Under His wings, I’m safely Abiding (SDAH 529).


Uchunguzi: Kufuatilia miaka 430 ya utumwa na mateso ya Israeli – Andiko Kuu: Mwa. 15:13-16. Soma – (Mwa. 21:9 cf. Gal. 4:29; Mwa. 27:41–43; 31:2, 21, 29; 37:28; 39:20; Kut. 1:8, 12; Kut. 12:40-41 cf. Gal. 3:16-17)

Tafakari: Karibuni, marafiki, tunapoanza somo jipya katika kitabu cha Kutoka. Mada kuu ni Ukombozi kutoka kwenye Udhalimu – (utumwa, mateso, ukandamizaji). Ili kuelewa kinachotendeka hapa, ni lazima mtu arudie upya kutazama agano la Mungu (unabii) pamoja na Ibrahimu katika Mwanzo 15:13–16. Mungu alikuwa amemfunulia Ibrahimu kwamba wazao wake wangekabiliwa na mateso lakini tendo kubwa la ukombozi lingeondoa utumwa wao. Wamisri wangehukumiwa, na Waisraeli wangeachwa huru ili warudi katika nchi yao.

Kutoka sura ya kwanza ni utimizaji wa unabii huu. Hapa, Israeli wanateswa vikali na mfalme wa Misri. Fasili ya 1-10 huandika kwa undani zaidi sababu za mateso: kustawi kwa Israeli na hofu ya mfalme. Fasili ya 11-22 huonesha mateso yanayotokea: Israeli inafanikiwa na kuongezeka licha ya utumwa mgumu. Katika jitihada zake endelevu za kuzuia ukuaji/nguvu za Israeli, Farao anawaamuru wakunga wa Kiebrania kuwaua watoto wote wa kiume wa Israeli wakati wa kuzaliwa. “Lakini wale wakunga walikuwa wakimcha Mungu, wasifanye kama walivyoamriwa na huyo mfalme wa Misri, lakini wakawahifadhi hai wale watoto wa kiume” (Kut. 1:17). Wakunga hao kwa ujasiri wanachagua kumtii Mungu kuliko wanadamu! Mungu alibariki juhudi za wakunga hawa: watu wa Israeli wakaongezeka sana na kuwa hodari sana! Akiwa amechanganyikiwa sana, Farao aliamuru watu wake wawatupe watoto wote wa kiume wa Waisraeli katika Mto Nile. Katika sura ya pili, tutaona jinsi Mungu alivyomwinua mkombozi, Musa.

Maana ya Kiibada: “Mpango wa mfalme wa kuwaua watoto wote wa kiume ungepata mafanikio makubwa endapo isipokuwa kuingilia kati kwa Mungu. Aliwatumia wakunga hao ili kumfadhaisha mfalme, kama vile ambavyo baadaye alitumia kilio cha mtoto ili kuugusa moyo wa binti wa Farao. Mungu hutumia vitu dhaifu vya ulimwengu huu ili kuwashinda wenye nguvu. Bila shaka, mbinu ya mfalme ilitokana na Shetani, muuaji. Hili lilikuwa tu jaribio lingine la Shetani la kuwaangamiza Wayahudi na kumzuia Masihi asizaliwe. Baadaye, Shetani angemtumia Mfalme Herode ili kujaribu kumuua Mtoto Yesu. Je, ilikuwa sawa kwa hao wanawake kukaidi amri za mfalme? Ndiyo, maana “imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu” (Matendo 5:29). Sheria za nchi zinapokuwa kinyume kabisa na amri za Mungu, basi muumini ana haki na wajibu wa kumtanguliza Mungu. Ingawa Mungu hakuidhinisha udhuru ambao wakunga walimwambia Farao (ingawa maneno yao pengine yalikuwa kweli), aliwabariki kwa ajili ya imani yao. Kumbuka kwamba mtawala huyuhuyu aliyetaka kuwazamisha majini watu wa Mungu, alishuhudia jeshi lake mwenyewe likizamishwa katika Bahari ya Shamu (Kut. 15:4–5). Tunavuna tunachopanda, ingawa mavuno yanaweza kukawia kuja (Mhu. 8:11).” – [Warren W. Wiersbe, Wiersbe’s Expository Outlines on the Old Testament, (Wheaton, IL: Victor Books, 1993), Ex 1].

Sauti ya Injili: Sehemu hiyo imeandikwa kana kwamba Mungu anazungumza nawe moja kwa moja — kwa sababu Yeye anafanya hivyo. Bwana ananiambia nini asubuhi ya leo? Mwanangu, Shetani, alikuwa akifanya kazi kupitia mfalme wa Misri ili kuzuia mpango Wangu kwa watu Wangu, taifa la Israeli. Katika sura hii, huyu mfalme mwovu alifanya majaribio matatu ya kuwaangamiza Waebrania (Kut. 1:7-10, 15-16, 22) ila akashindwa. Hakuna anayeweza kuvuruga mipango Yangu—mpango Wangu wa ukombozi kwako. Pili, utakabiliwa na mateso, maana “wale waishio maisha ya utauwa watateswa” (2 Tim 3:12). Pengine mustakabali ujao ukaonekana kana kwamba hauna uhakika, lakini ninafanyia kazi jambo fulani bora zaidi (Zab. 36:7-8). Ukidumu kuwa mwaminifu Kwangu, nitakubariki, nitakupa amani na nguvu za kustahimili majaribu! Hakika nitakuwa pamoja nawe katika taabu (Zab 23:6; Mat 28:20; Isa. 41:10; Yn. 12:26; Matendo 18:9-10; Filp. 4:13; Ebr. 13:5-6). Je, utaweka tumaini lako chini ya uvuli wa mbawa Zangu?

Shauku Yangu: Kwa neema ya Mungu:

  1. Nataka kumtii Mungu kuliko wanadamu! (Kufuuata mfano wa wale wakunga, Kut. 1:17).
  2. Nataka kudumu kuwa mwaminifu kwa Mungu hata wakati wa majaribu na dhiki kali za maisha.
  3. Nataka kuamini kwamba uwepo Wake utakuwa pamoja nami na kwamba hatimaye, atanitetea (Ayubu 19:25–26).

Uwe na Siku Yenye Baraka: “Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao.” (Yakobo 1:12)


 

Ibada Kupitia Uimbaji: Under His wings, I’m safely Abiding (SDAH 529).

1 Under His wings I am safely abiding;
Though the night deepens and tempests are wild,
Still I can trust Him; I know He will keep me;
He has redeemed me, and I am His child.

Refrain:
Under His wings, under His wings,
Who from His love can sever?
Under His wings my soul shall abide,
Safely abide forever.

2 Under His wings, what a refuge in sorrow!
How the heart yearningly turns to its rest!
Often when earth has no balm for my healing,
There I find comfort, and there I am blest.

3 Under His wings, O what precious enjoyment!
There will I hide till life’s trials are o’er;
Sheltered, protected, no evil can harm me;
Resting in Jesus I’m safe evermore.

 

Comments
Print Friendly, PDF & Email