Sadaka ya Kuteketezwa

April 13, 2022 in Mwongozo wa Ibada by TGVS

Walawi 1: Mwongozo wa Ibada/ 3-BSG-1A, (Walawi 1:1-17)/ Maudhui: Sadaka ya Kuteketezwa/ Wimbo: Jesus Paid It All (SDAH 184)


 

Uchunguzi: Sadaka ya Kuteketezwa, mfano wa Kristo – (tazama Ebr. 7:25, 26; 1 Yn. 3:5; 2 Kor. 5:21; 1 Pet 1:18-19).

Tafakari: Mpendwa, karibu katika kitabu cha Walawi. Mahali – (Israeli iko Mlima Sinai mwaka mzima). Muda (takriban 1446 KK). Maudhui – (Jinsi gani wanadamu wadhambi wanaweza kumkaribia na kumwabudu Mungu mtakatifu). Aya Muhimu – (Law. 16:16; 17:11, 19:2, 20:7-8). Kristo katika Walawi – (Katika kila kafara, kila kaida, kila adhimisho). Walawi 1-17 hujadili ufikiaji wa mdhambi kwa (au njia ya kumwendea Mungu), ilhali Walawi 18-27 husisitiza mtindo wa maisha wa mdhambi (au kuenenda na Mungu). Hapa, Waisraeli walifundishwa taratibu za ibada: jinsi ya kuabudu/ kumkaribia Mungu mtakatifu. Pili, walipewa miongozo sadifu: kuishi maisha matakatifu. Kwa hiyo, Walawi hujulikana vyema kama Kitabu cha Utakaso na Ibada.

Sura hii hujadili kuhusu Sadaka ya Kuteketezwa (1:3–17). Inaweza kuainishwa kama ifuatavyo: Sifa za sadaka ya kuteketezwa (3); Utashi huru wa Mdhambi (3b) na kuhamishwa kwa hatia (4); Utaratibu wa kumtoa Fahali kama sadaka ya kuteketezwa (5–9); Utaratibu wa kumtoa Kondoo au Mbuzi kuwa sadaka ya kuteketezwa (10–13); Utaratibu wa Kumtoa Ndege kama sadaka ya kuteketezwa (14–17).

Maana ya Kiibada: Wazo la dhabihu kwa miungu halikuwa huduma waliyoifanya Israeli tu. Mataifa na tamaduni zingine zilitoa kafara hii; hata hivyo, ni Israeli pekee waliotoa dhabihu kwa Mungu mmoja wa kweli. Waisraeli walijua kwamba dhabihu za wanyama zilitumiwa hasa kama matoleo kwa ajili ya dhambi. Kutoka Edeni, Dhambi ilishughulikiwa kupitia dhabihu. Huu haukuwa mwanzo wa mfumo wa Mungu wa dhabihu. Adamu alijua kuhusu dhabihu hii (Mwa. 3:21), kama alivyofanya Kaini na Abeli (Mwa. 4:3–4) na Nuhu (Mwa. 8:20–21).

Lakini kwa nini kuwaua wanyama ili kumwabudu Mungu? Kila wakati mnyama alipotolewa kafara, iliwakumbusha Waisraeli waziwazi kwamba dhambi ni mbaya sana kiasi cha kufisha (Mwa. 2:17). Wakati uhai wa mnyama ulipotolewa kulipa adhabu ya dhambi, mtu mwenye hatia alisamehewa na kutakaswa. Kwa kuweka mkono wake juu ya kichwa cha mnyama aliyetolewa dhabihu (Law. 1:4), mdhambi alihamisha dhambi zake kwenda kwa mnyama huyo. Mtenda-dhambi aliona jinsi mnyama huyo alivyokuwa akifa “kama mbadala” wa dhambi yake. Damu, iliyowakilisha uhai wa mnyama husika ilikuwa ni wakala wa utakaso ulioondoa dhambi (Law. 17:11). Wazo kuu ni hili: “Uhai umo katika damu” (Law. 17:11), na “pasipo kumwaga Damu, hakuna ondoleo la dhambi” (Ebr. 9:22). Mungu alikuwa akiifundisha Israeli kwamba Mwanakondoo wa Mungu ‘asiye na doa’ angetolewa kafara kwa ajili ya wanadamu wote siku moja. Kafara hizi zililenga kwenye Kafara ijayo—Yesu Kristo. Sadaka ya Kuteketezwa kwa hakika ilikuwa ni mfano (kielelezo) wa Kristo.

Sauti ya Injili: Sehemu hiyo imeandikwa kana kwamba Mungu anazungumza nawe moja kwa moja — kwa sababu Yeye anafanya hivyo. Bwana ananiambia nini asubuhi ya leo? Mwanangu, Yesu Kristo, ni yule Mwanakondoo “asiye na ila” (Law. 1:3; Yn. 1:9; 1 Pet 1:19) aliyetolewa kafara kwa ajili yako pale Kalvari. Siku hiyo alichukua nafasi yako (adhabu) ili uweze kuishi milele. Damu Yake ya thamani ilimwagwa kwa ajili yako! (Marko 14:24). Natamani kukubariki, kukutakasa, na kukutia muhuri kwa ajili ya ufalme Wangu, lakini dhambi zako zimezuia njia (Isa 59:1-2). Laiti ungeungama, ukatubu, na kuja kwa Yesu kwa ajili ya utakaso. Je, utafanya hivyo?

Shauku Yangu: Kwa neema ya Mungu, nataka – 1. Kuja kwenye mlango wa Maskani (Law. 1:3) na kuungama dhambi zangu; 2. Kumwomba Yesu, Mwanakondoo wa Mungu asiye na waa, anisamehe dhambi zangu na kunitakasa; 3. Kumtolea Mungu sadaka yangu, huduma yangu, na talanta zangu kwa hiari kama ambavyo alinipatia uhai Wake kwa hiari

Uwe na Siku Yenye Baraka:Tubuni basi na kuongoka, ili dhambi zenu zifutwe, ili nyakati za burudiko ziweze kuja kutoka uweponi mwa Bwana.” (Matendo 3:19)


 

Ibada Kupitia Uimbaji: Jesus paid it all, All to Him I owe! (SDAH 184)/ Alilipa Bei (NZK 119).

1. Yesu anasema, “Wewe huna nguvu; Kesha ukaombe, Na uje, Mwangu.”

[Pambio]: Alilipa bei, Nawiwa naye; Dhambi ilitia waa, Aliiondoa.

2. Bwana, nimeona; Uwezo wako tu; Waweza ‘takasa; Mioyo michafu.

3. Sina kitu chema; Kudai neema; Hivi nitafua; Mavazi kwa damu.

4. Ninaposimama; Juu ya mawingu; Taji nitaweka; Miguuni pa Yesu!

Comments
Print Friendly, PDF & Email