Dhambi ya Akani

July 26, 2022 in Usiku by TGVS

SAHAMU YA JIONI.

Mwongozo wa Kujifunza Biblia/ 6-BSG-7Y, (Yoshua 7:21)/ Dhima: Dhambi ya Akani/ Wimbo: When Jesus shall gather the nations, [Mwandishi: Harriet Burn McKeever (1885)/ NK #169]

 


Andiko Kuu: “Nilipoona katika nyara joho nzuri ya Babeli, na shekeli mia mbili za fedha, na kabari ya dhahabu, uzani wake shekeli hamsini, basi nalivitamani nikavitwaa; tazama, vimefichwa mchangani katikati ya hema yangu, na ile fedha chini yake.” (Yoshua 7:21)

Historia ya Akani ni fupi na ya kusikitisha sana. Alikuwa mmoja wa askari wa Waisraeli walioingia Yeriko, lakini alichagua kutotii amri bayana kutoka kwa Bwana. Kuna mawazo manne ambayo ninataka kuyaleta kwenu usiku wa leo:

[1] Tamaa Yake: “Niliona, kisha nikavitamani” (v. 21). Dhambi mara nyingi huanza kwa kutazama. Hawa aliona tunda. Lutu aliona nchi tambarare zenye maji ya kutosha. Ahazi aliona madhabahu na kuinakili (2 Wafalme 16:10). Lakini dhambi ya Akani haikuwa katika kuona dhahabu, nk., labda hangeweza kujizuia, bali “alizitamani.” Alipenda mapato yaliyokatazwa hadi tamaa ilipousogeza mkono wake. Anasa za dhambi daima zitavutia mambo mengine zaidi pale mtu anapozitazama kwa tamaa. Wakristo lazima waichunge mioyo yao. Hali fulani zinaweza kuleta matokeo mabaya ikiwa kila wazo “lisipotekwa limtii Kristo” (2 Kor. 10:5).

[2] Uasi Wake: “Alichukua katika kitu kilicholaaniwa” (v. 1). Mungu alikuwa ameionya Israeli, “Jihadharini msije mkatamani kitu chochote katika Yeriko na kuchukua kitu kilicholaaniwa.” (6:18). Akani alitenda dhambi kwa makusudi, si kwa ujinga. Ukweli wa kwamba alificha hazina hizo huthibitisha kwamba alikuwa na ufahamu wa makosa yake. Wengi bado wanamwasi Mungu kwa makusudi kwa kupendelea ulimwengu kuliko Kristo na mara nyingi kudumisha “mwonekano wa utauwa” ili kuwadanganya wengine. Unafiki wa Akani si jambo geni siku hizi, hata miongoni mwa watu wanaodai kuwa wafanyakazi wa Kristo. Ingawa Bwana amesema waziwazi, “Msiipende dunia,” lo, ni kiasi gani ambacho kimefichwa moyoni?

[3] Kugunduliwa Kwake: “Na Akani akatwaliwa” (v. 18). Tambua kwamba dhambi yako itakuumbua (Hes. 32:23), ama wewe ni mtakatifu au mdhambi, Mkristo au la. Alipatikana miongoni mwa maelfu wote wa Israeli kwa sababu hakuna kitu kilichofichwa machoni pa Mungu, ambaye kila mdhambi anawajibika Kwake. Ni ugunduzi taadhimu ilioje, kubainishwa machoni pa watu wote, na kila jambo lililositiriwa likafichuliwa. Ni kiashiria cha namna gani cha ile Hukumu Kuu! (cf. Mat 7:21-23).

[4] Uangamivu Wake: “Na Israeli wote wakampiga mawe” (v. 25). Haikuwepo njia yoyote ya kutorokea. Mtume Paulo anauliza swali muhimu, “tutawezaje kupona?” Zingatia tofauti iliyokuwepo kati ya nyumba ya Rahabu na ile ya Akani: Mmoja aliokolewa, mwingine alipotea (cf. 6:25). Imani ya mmoja ilimuokoa; uasi wa mwingine ulipelekea mauti— “Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, Lakini mwisho wake ni njia za mauti” (Mithali 14:12). Wapendwa, hebu kila mmoja ajiulize yuke upande gani—(wa Rahabu au Akani?) Je mwisho wetu utakuwaje: wokovu au uangamivu? Kuna “dhambi kambini,” Je, imo ndani yangu, Bwana?

Sauti ya Injili:Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.” (Mithali 28:13). Wengi wetu ni kama Akani. Ndiyo, tuko kanisani—tukisoma, tukiimba, tukiabudu, tukihudumu, na hata kuhubiri. Lakini kuna kitu fulani ‘kilichofichwa katika kambi zetu, ndani ya mioyo yetu,’ namaanisha, “ile dhambi mahususi” ambayo hakuna yeyote mwingine ajuaye, isipokuwa Mungu. Kwa nje, tuna “mfano wa utauwa” (2 Tim. 3:5), lakini kwa ndani kabisa, sisi ni wadhambi. Tunaweza kumdanganya kila mtu anayetuzunguka, lakini hatuwezi kumdanganya Mungu God (Zab. 139:1-6). Wapendwa, usiku wa leo sauti ya Mungu inakuita utubu mara moja kabla hujachelewa kabisa! (cf. Matthew 3:10).

 


Uwe na Usiku Mwema:Mambo hayo yaliwapata wao kama mifano kwetu. Yaliandikwa ili kutuonya sisi tuishio mwisho wa zama hizi.” (1 Wakorintho 10:11, NLT). “Tutawezaje kupona tusipojali wokovu mkuu namna hii, ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitishwa kwetu kupitia wale waliomsikia?” (Waebrania 2:3, NKJV)

Comments
Print Friendly, PDF & Email