Anza na Bwana, July 27, 2022

July 26, 2022 in Alfajiri, Mwongozo wa Maombi by TGVS

ANZA NA BWANA!
Jumatano: July 27, 2022.

Kipindi cha Ibada ya Maombi.
[1] “Naomba niombewe Bwana anipatie ratiba ya maombi na familia yangu” (SM); [2] “Umaliziaji wa Nyumba yangu ununuzi wa bati na mbao” (SM); [3] “Wadogo zangu Loius, Samweli, Neema & Veronica- Wapate kuifahamu kweli” (SM); [4] “Naombeni maombi yenu ya kiafya pia, maana nina udhaifu wa kiafya” (MA); [5] Ombea watendakazi wote waliyo shambani mwa Bwana; [6] Ombea huduma hii ya Injili: ili kwamba wengi waokolewe, waingie mbinguni; [7] Ombea fedha kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Injili; [8] Ombea wagonjwa, walemavu, wanaotengwa/ teswa na familia zao kwa ajili ya Injili; [9] Ombea ujasiri wa kuanza upya na Bwana… katika sura ya leo– kuwa na “Mwanzo mpya” wa kiroho (Yoshua 8:1-2), na Kufanya “Maagano Mapya” na Bwana wako (Yoshua 8:30–35).

SALA: Baba, asante kwa fursa ya uhai tena. Tunakushukuru sana kwa nafasi unayotupatia tena na tena. Japo Israeli walikuasi na kutanga mabi (7:1), uliwasamehe, na kuwapatia Ushindi mkuu, hadi wakauteka mji wa Ai. Tusaidie tusiwe kama Akani, lakini tutubu na kuleta dhambi zetu Kwko kwa ajili ya utakaso. Saidi mtu mmoja atakayesoma Mafundisho haya siku hii ya leo –apate kutubu, kuokolewa na kuurithi ufalme Wako. Pamoja na hayo, tuna mizigo mizito, na changamoto mbalimbali za Maisha. Ninasihi utuangalie kwa jicho la huruma, na ukawatendee watoto wako sawasawa na Mapenzi Yako. Tumeomba haya katika jina la Yesu Kristo, Mkombozi wetu, Amina.


 

AHADI YA LEO:

Dhima: Ahadi ya Mianzo Mipya na Bwana.

  • “Hatua za mtu zaimarishwa na Bwana, Naye aipenda njia yake. Ajapojikwaa hataanguka chini, Bwana humshika mkono na kumtegemeza.” (Zaburi 37:23-24)
  • “Msiyakumbuke mambo ya kwanza, wala msiyatafakari mambo ya zamani. Tazama, nitatenda neno jipya; sasa litachipuka; je! Hamtalijua sasa? Nitafanya njia hata jangwani, na mito ya maji nyikani.” (Isaya 43:18-19)

Je una Mzigo wowote? Je una Jambo la kumshukuru Bwana? Je unao Wimbo wowote? Je una Ushuhuda wowote? Karibu Mpendwa: Nafasi hii ni yako…

 

Comments
Print Friendly, PDF & Email