Waamuzi 2: Usomaji, Vidokezo

August 21, 2022 in Usomaji/ Vidokezo by TGVS

WAAMUZI 2D: MDOKEZO WA SURA. 

Mwongozo wa Kujifunza Biblia/ Muhtasari wa Sura/ Waamuzi 2, (7-BSG-2D)/ Dhima: Kushindwa kwa Israeli, rehema ya Mungu


 

Kifupi: Sura hii ina maelezo ya kuvutia ya kutokea kwa Malaika, yenye ujumbe kutoka kwa Yehova kwa Israeli. Sura hiyo inazangatia mtazamo wa matukio ya zamani katika mwenendo wa Israeli chini ya Yoshua kwa njia ya kuonesha kuondoka kwao kwa kuhuzunisha baada ya kifo chake, matokeo ya utii usio kamili, na kusimikwa kwa “waamuzi.”

Wahusika: Mungu, Malaika wa Bwana, Yoshua, Israeli.

Andiko Kuu: “Hata hivyo, BWANA akawainulia waamuzi ambao waliwaokoa kutoka mikononi mwa wale waliowateka nyara. Lakini hawakuwasikiliza hao waamuzi wao, maana walifanya ukahaba na miungu mingine na kuwasujudia. Wakageuka upesi na kuiacha njia waliyoiendea baba zao, katika kuzitii amri za BWANA; hawakufanya hivyo.” (Waamuzi 2:16–17)

Neno Kuu: ‘Wakageuka,’ Waamuzi 2:17 (Ebr. Sur) = kugeukia kando, kwenda zao, na kuondoka.

  • [a] kumwacha Mungu, kutoka kwenye ibada yake –(Sam. 12:20; 2 Falm. 10:29; 18:6; 2 Nya. 25:27; Eze. 6:9; Yer. 17:5).
  • [b] kuiacha sheria ya Mungu –(Kumb. 17:20; 28:14; Yos. 23:6; Dan. 9:5, 11; Zab.119:102)

Neno husika linamaanisha “kwenda katika uelekeo fulani, kwa kuzingatia kwamba kuna badiliko katika mwelekeo kutoka kwenye mapito au njia (Kut. 3:3).’ — (James Swanson).

Maneno/Virai Teule — Malaika wa Bwana; Sitalivunja agano Langu kamwe; Israeli ilifanya maovu machoni pa Bwana; Bwana akawainua Waamuzi; Lakini walifanya ukahaba; Bwana akawahurumia kwa kuugua kwao; Walimkasirisha Bwana (12, 20); Ili niwajaribu (Israeli).

Maandiko Makini: Waamuzi 2:1, 2, 3, 4, 5, 18, 20, 21, 22.

Mgawanyo wa Mawazo Makuu — Onyo kutoka kwa Mungu (2:1–5); utii wa Israeli (2:6–10); miungu ya kigeni ya Israeli (2:11–15); Miamsho na maanguko ya Israeli (2:16–18); Kujaribiw kwa Israeli (2:19 -3:4).

Matukio ya Biblia: [Matukio yanayofanyika]—

  1. Yoshua awaongoza Waisraeli • Amu. 1:3–2:5
  2. Israeli Kuiteka Kanaani • Amu. 1:3–2:9
  3. Israeli yashindwa kuteka maeneo kadhaa • Amu. 1:21–2:5
  4. Malaika wa Bwana awakemea watu huko Bokimu • Amu. 2:1–5
  5. Yoshua afa na kuzikwa • Amu. 2:6–9
  6. Yoshua na Eleazari wafa • Amu. 2:6–9

Mdokezo wa Mambo Muhimu — Malaika wa Yehova (2:1); agano la Yehova na Israeli; Amri ya Yehova ya kuvunja Sanamu; Ukombozi (kuokolewa kutoka katika madhara au hatari);

Uchunguzi wa Muktadha Msingi — Taratibu za Misiba na Maziko; Miungu ya kipagani katika Agano la Kale (2:13)

Mambo ya Kujifunza Zaidi — Ugumu wa moyo; Ukengeufu; Ibada ya Sanamu; Kujaribiwa kwa Israeli (katika Waamuzi 2:22).

Wazo Muhimu: “Dhambi maishani mwetu tunayoshindwa kuidhibiti hatimaye itatushinda. Watu wa Israeli walijikuta wamefanywa watumwa na taifa moja baada ya lingine kwa vile Bwana alishika neno Lake na kuwaadhibu watu Wake. Fikiria dhambi za kizazi kipya — Walisahau yale ambayo Bwana alikuwa amefanya (vv. 6–10). Waliacha kile ambacho Bwana alikuwa amesema (vv. 11–13). Walipoteza kile ambacho Bwana alikuwa ameahidi (vv. 14–15). Walishindwa kujifunza kutokana na yale ambayo Bwana alifanya (vv. 16–23).”

“Mungu aliwakomboa watu Wake kwa kuinua waamuzi, waliomshinda adui na kuiweka huru Israeli. Neno la Kiebrania linalotafsiriwa “mwamuzi” linamaanisha “kuokoa, kunusuru.” Waamuzi walikuwa wakombozi walioshinda mapambano mkubwa kijeshi kwa msaada wa Bwana. Lakini waamuzi pia walikuwa viongozi waliowasaidia watu kusuluhisha migogoro yao (4:4–5). Waamuzi walitoka katika makabila tofauti na walifanya kazi katika maeneo mahalia badala ya kitaifa; na katika baadhi ya matukio, muda wao wa madaraka ulipishana. Neno “mwamuzi” linatumika kwa watu wanane tu miongoni mwa kumi na mbili ambao kwa kawaida huwaitwa “waamuzi,” lakini wote walifanya kazi kama washauri na wakombozi. Watu hao wanane ni: Othnieli (3:9), Tola (10:1–2), Yairi (10:3–5), Yeftha (11), Ibzani (12:8–10), Eloni (12:11–12), Abdoni (12:13–15), na Samsoni (15:20; 16:31).

Mzunguko wa kutotii, kuadhibiwa, kukata tamaa, na ukombozi unaonekana leo wakati wowote watu wa Mungu wanapogeuka, wakaliacha Neno Lake na kuiendea njia yao wenyewe. Ikiwa kutotii huko kusipofuatiwa na adhabu ya kiungu, basi mtu huyo hakika si mtoto wa Mungu; kwa maana Mungu huwarudi watoto Wake wote (Ebr. 12:3–13). Mungu ana huruma nyingi kwa watu Wake, lakini ana hasira dhidi ya dhambi zao.” – [Warren W. Wiersbe, Be Available, “Be” Commentary Series, (Wheaton, IL: Victor Books, 1994), 18, 19–20].

 

WAAMUZI 2C: SURA YA LEO

Usomaji wa Biblia kwa Mpango/ Kitabu cha Waamuzi sura ya 2, (7-BSG-2C)/ Dhima: Kushindwa kwa Israeli, rehema ya Mungu

Waamuzi 2:

1 Kisha malaika wa Bwana alikwea juu kutoka Gilgali kwenda Bokimu. Akasema, Mimi nimewaleta ninyi mkwee juu kutoka nchi ya Misri, nami nimewaleta hata nchi niliyowaapia baba zenu; nami nilisema, Mimi milele sitalivunja hilo agano langu nililoagana nanyi;
nanyi msifanye agano lo lote na hawa wenyeji wa nchi hii; zipomosheni nchi madhabahu zao; lakini hamkuisikia sauti yangu; je! Mmefanya haya kwa sababu gani?
Basi kwa ajili ya hayo mimi nilisema zaidi, Mimi sitawafukuza watoke mbele zenu; lakini watakuwa kama miiba mbavuni mwenu, na miungu yao itakuwa ni tanzi kwenu.
Ikawa, hapo huyo malaika wa Bwana alipoyanena maneno haya, kuwaambia wana wa Israeli wote, ndipo hao watu wakainua sauti zao na kulia.
Nao wakaliita jina la mahali pale Bokimu; nao wakamchinjia Bwana sadaka huko.
Basi hapo Yoshua alipowapa watu ruhusa waende zao, wana wa Israeli wakaenda kila mtu kuuendea urithi wake, ili kuimiliki hiyo nchi.
Watu hao wakamtumikia Bwana siku zote za Yoshua, na siku zote za hao wazee walioendelea siku zao baada ya Yoshua, hao waliokuwa wameiona hiyo kazi kubwa ya Bwana yote, aliyokuwa ameitenda kwa ajili ya Israeli.
Kisha Yoshua mwana wa Nuni, mtumishi wa Bwana, akafa, naye alipata umri wa miaka mia na kumi.
Nao wakamzika katika mpaka wa urithi wake katika Timnath-heresi, katika nchi ya vilima vilima ya Efraimu, upande wa kaskazini wa mlima wa Gaashi.
10 Tena watu wote wa kizazi hicho nao walikusanywa waende kwa baba zao; kikainuka kizazi kingine nyuma yao, ambacho hakikumjua Bwana, wala hawakuijua hiyo kazi ambayo alikuwa ameitenda kwa ajili ya Israeli.
11 Wana wa Israeli walifanya yaliyokuwa ni maovu mbele za macho ya Bwana, nao wakawatumikia Mabaali.
12 Wakamwacha Bwana, Mungu wa baba zao, aliyewaleta kutoka katika nchi ya Misri, wakafuata miungu mingine, baadhi ya miungu ya watu wale waliokaa karibu nao pande zote, wakajiinamisha mbele yao; wakamkasirisha Bwana, akaghadhibika.
13 Wakamwacha Bwana, wakamtumikia Baali na Maashtorethi.
14 Hasira ya Bwana ikawaka juu ya Israeli, naye akawatia katika mikono ya watu waliowateka nyara, akawauza na kuwatia katika mikono ya adui zao pande zote; hata wasiweze tena kusimama mbele ya adui zao.
15 Kila walikokwenda mkono wa Bwana ulikuwa juu yao kuwatenda mabaya, kama Bwana alivyosema, na kama Bwana alivyowaapia; nao wakafadhaika sana.
16 Kisha Bwana akawainua waamuzi, waliowaokoa na mikono ya watu hao waliowateka nyara.
17 Lakini hawakuwasikiliza hao waamuzi wao, maana walifanya uasherati kwa kuifuata miungu mingine, wakajiinamisha mbele yao; wakageuka upesi, na kuiacha njia ile waliyoiendea baba zao, waliozitii amri za Bwana bali wao hawakufanya hivyo.
18 Na wakati Bwana alipowainulia waamuzi, ndipo Bwana alikuwa pamoja na mwamuzi huyo, akawaokoa na mikono ya adui zao siku zote za mwamuzi huyo; maana Bwana alighairi kwa ajili ya kuugua kwao kwa sababu ya watu wale waliowaonea na kuwasumbua.
19 Lakini ikawa, wakati alipokufa mwamuzi huyo, wakarudi nyuma wakafanya maovu kuliko baba zao, kwa kuifuata miungu mingine ili kuitumikia, na kuinama mbele yao; hawakuacha matendo yao, wala njia zao za ukaidi.
20 Basi hasira ya Bwana ikawaka juu ya Israeli, naye akasema, Kwa kuwa taifa hili wamelihalifu agano langu nililowaamuru baba zao, wala hawakuisikiliza sauti yangu;
21 mimi nami tokea sasa sitalifukuza taifa mojawapo la hayo aliyoyaacha Yoshua alipokufa;
22 ili kwa njia ya hayo nipate kuwajaribu Israeli, kwamba wataishika njia ya Bwana kwenda katika njia hiyo, au sivyo.
23 Basi Bwana akawaacha mataifa yale, wala hakuwafukuza kwa upesi, wala hakuwatia katika mikono ya Yoshua.

Comments
Print Friendly, PDF & Email