Torati 24 (Maswali na Majibu)
April 7, 2019 in Usomaji/ Vidokezo by TGVS
Maswali na Majibu.
Mongozo wa Biblia
5-BSG-24J.1 (Torati 24)
[1] Matukio yapi ya kibiblia yanapatikana katika sura hii?
A. Matukio yanayofanyika:
(a) Waisraeli wanatangatanga katika nyika • (Kutoka 12:33 – Totati 34:8)
(b) Hotuba ya Musa ya kuagana • (Torati 1:1 – 30:20)
(c) Waisraeli waanza kuishi Kanaani• (Torati 1:1-34:8)
(d) Hotuba ya Musa sehemu ya 4: Sheria • (Torati 17:8 – 26:19)
Matukio yanayotajwa:
(a) Miriamu na Haruni wapinga Musa • (Hesabu 11:35 – 12:15; Torati 24:9)
[2] Ni kwa muda gani “baada ya ndoa,” mtu (mwanaume) aliruhusiwa kwenda vitani? (5) Mwaka Mmoja.
[3] Nini kilipaswa kifanyike watekaji nyara? (7) Adhabu ya Kifo: “Mtu akionekana anamwiba nduguze mmojawapo katika wana wa Israeli, akamfanya kama mtumwa, au kumwuza; na afe mwivi huyo; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako.”
[4] Ni mara ngapi ilipaswa kumlipa mtumishi (mtumwa) ambaye ni maskini? (14-15) “Mpe ujira wake kwa siku yake.”
[5] Kwa ajili ya dhambi ya nani mtu alipaswa kuuawa? (16) Dhambi yake mwenyewe: “Mababa wasiuawe kwa ajili ya watoto wao, wala watoto wasiuawe kwa ajili ya baba zao; kila mtu na auawe kwa ajili ya dhambi yake mwenyewe.”
[6] Nini waliruhusiwa mgeni, yatima na wajane kula? (19-21)
(a) Mganda
(b) Matunda ya mizeituni
(c) Zabibu