Mungu Yu Pamoja Nasi

August 23, 2020 in Injili Ya Asubuhi by TGVS

Injili ya Asubuhi
IMANUELI: MUNGU PAMOJA NASI.
Andiko Kuu: Matayo 1:23.


 

Shabaha: Utambuzi wa uwepo wa Imanueli kati yetu. Je unatambua kuwa Mungu amekuwa pamoja nasi siku zote? Dhambi zetu ndizo zinatutenga na Mungu wetu (Isa 59: 1-2). Je una tatizo gani asubuhi ya leo? Nenda kwa Emmanueli. Mwamini Yesu Kristo, Naye atakusaidia.

“Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi.” (Matayo 1:23) “Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara. Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Imanueli.” (Isaya 7:14)

Sauti ya Injili: “Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao. Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.” (Ufunuo 21:3-4)

Comments