Kiri Udhalimu Wako

November 16, 2020 in Usiku by TGVS

Mwongozo wa Kujifunza Biblia/ Jeremiah 3, (24-BSG-3Y)/ Wazo la Usiku Linaloshabihiana na “Mpango wa Usomaji Biblia” wa leo/ Dhima: Kiri Udhalimu Wako/ Wimbo: Jesus, the loving Shepherd, [Mwandishi: W. A. Ogden]


 

Andiko Msingi: Yeremia 3:12–13 12 Enenda, ukatangaze maneno haya kuelekea upande wa kaskazini, ukaseme, Rudi, Ee Israeli mwenye kuasi, asema Bwana; sitakutazama kwa hasira; maana Mimi ni mwenye rehema, asema Bwana, sitashika hasira hata milele. 13 Ungama uovu wako tu; ya kwamba umemwasi Bwana, Mungu wako, na njia zako zimekuwa nyingi kuwaendea wageni chini ya kila mti wenye majani mabichi, wala hamkuitii sauti Yangu, asema Bwana.

UCHUNGUZI: Njia ya Mungu ya Baraka → Ungamo; Toba (kugeuka na kuacha dhambi) — Soma (Isa 1:18-20; 3:10; 55:1-3, 6-7; Yer. 3:12-14; 31:18-20; Hos. 14:1-4; Ayubu 36:12; Yer. 18:7-8; 26:3; Luka 3:8-9; Ufu. 2:5;1 Yohana 1:9)

TAFAKARI: Kuna njia moja tu ya kupata baraka za Mungu; “siyo sharafu (ustahili), au wema, au amali (matendo), au juhudi, bali tu kukiri dhambi. katika kukiri huku, hakuna lolote stahilifu, hakuna lolote ambalo kwa lenyewe linakusudiwa kuvutia au kutufanya tujipatie baraka. Lakini ni njia aliyoteua Mungu; ni mfereji ambao kwao msamaha hupitia; hutuweka katika usawa ule ambapo Mungu pekee anaweza kumbariki mdhambi.”

“Kiri tu”! Haya ni maneno Yake kwetu, akitangaza njia ya baraka. “Kiri tu”! Ndivyo anenavyo kwetu (1 Yohana 1:9).

Vipengele mahususi vya kukiri hufuata: (1.) udhalimu, (2.) uasi dhidi ya Bwana Mungu wetu; (3.) kuifuata sanamu; (4.) kutotii sauti ya Yehova. Zile dhambi mahususi hasa ambazo Israeli ilizitenda. Ni orodha hii mahususi ya dhambi ambayo anatuonesha. Pitia orodha mahususi unapokuja mbele ya Bwana. Jihadhari na maungamo ya jumla. Hayagusi dhamiri, na wala hayamfikii Mungu. Fanya kwa umaalum na kwa kufuata vipengele vidogovidogo vya kina katika yote umwambiayo Mungu kuhusu dhambi yako. Halafu ukiwa na ujasiri kamili wa kupokea msamaha; maana tukiungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki kiasi kwamba atatusamehe dhambi zetu.

MAANA YA KIIBADA: Kiri tu! Hili ndilo jambo moja analouliza Mungu; ni jambo moja ambalo mdhambi anajiepusha nalo. Maana humshusha chini hasa. Humvua kabisa wema wote. Lakini siyo katika usawa mwingineo wowote ambapo Mungu atashughulika na mdhambi yeyote. Ndivyo ilivyokuwa katika suala la Farisayo na mtozaushuru. Hii ilikuwa dhambi mahususi ya Laodikia; kukataa kukiri umaskini. Ni katika hili ndipo ambapo Bwana alimhimiza. Hivyo anatuhimiza. Ni kiburi chetu ndicho husimama katika yetu na baraka. Chukua mahali pa mdhambi na yote yanakuwa yetu.

Hebu tuwajibike Kwake sabab kama wadhambi; Naye ajapo tena atatumiliki kama wana na warithi.” [Horatius Bonar, Light and Truth: Or, Bible Thoughts and Themes, Old Testament, (London: J. Nisbet & Co., 1873), 282–283].


 

Iweni na Usiku Mwema: “Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, Nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu.” (Ufunuo 2:5)

Comments
Print Friendly, PDF & Email