Kiburi cha Misri.

January 20, 2021 in Usiku by TGVS

Mwongozo wa Kujifunza Biblia/ 26-BSG-29Y, (Ezekieli 29:2-3, 6)/ Vidokezo vya Sahamu vinavyoshabihiana na “Mpango wa Usomaji Biblia” wa leo / Dhima: Kiburi cha Misri.

Andiko Msingi: “Mwanadamu, elekeza uso wako juu ya Farao, mfalme wa Misri, ukatabiri juu yake, na juu ya Misri yote; nena, useme, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, Mimi ni juu yako, Ewe Farao, mfalme wa Misri, joka kubwa aoteaye kati ya mito yake, aliyesema, Mto Wangu ni Wangu Mwenyewe, Nami nimeufanya kwa ajili ya nafsi Yangu.” (Ezekiel 29:2–3, ESV)


 

Kiburi ni nini? Ni imani iliyokithiri jua ya uwezo binafsi ambayo humzuia mhusika kutambua neema ya Mungu. Imetajwa kama dhambi ambamo huibuka dhambi zingine zote.

Lakini habu tujadili kiburi kwa muktadha wa Mausi dhidi ya Misri. Katika Ezekieli 31:1–9, tuna mfano unaoibanisha Misri: Misri inasawiriwa kama mwerezi mkubwa na wa kifahari huko Lebanoni, unaohusudiwa na miti mingine yote. Katika somo letu leo, tunaona bayana Kiburi cha Misri: Farao mfalme wa Misri anahisia anaumiliki Mto Naili – “Naili yangu ni mali yangu; nimeufanya mimi mwenyewe” (29:3b). Pili, Misri inajivunia kuwa mkuu zaidi (31:10); Tatu, inadai kuwa simba miongoni mwa mataifa (32:1–2).

Ufafanuzi: “Katika ulimwengu wa kale, walijionesha kwa watu kama chanzo cha fanaka na ustawi wao. Huko Misri Mafarao walitamka hata madai makubwa zaidi kwa kutahawini kuwa mungu Horusi tahamili. Hili ndilo pengine lilimfanya Farao kutamka kauli za ufidhuli, Naili yangu ni mali yangu; nimeufanya mimi mwenyewe (v. 3b). Naili ilikuwa chanzo cha ukuu wa Misri. Ilikimu udongo wa aluvia wenye rutuba kando ya kingo zake, ambapo ng’ambo yake ilikuwa jangwa. Ilikimu masarufu ya maji endelevu ili kumwagilizia ardhi na kutuliza kiu ya Wamisri na wanyama wao. Ilikimu njia ya usafirishaji ambayo iliwezesha Misri kufikisha sokoni mavuno yake tele. Isingekuwepo Misri bila Naili. Misri, katika uhusika wa Farao, ilikuwa ikidai kwamba yenyewe ni chanzo chake binafsi cha ukuu wake. Madai haya, mara yalipotamka, yalisiliki anguko la Misri.’ [Bruce Vawter and Leslie J. Hoppe, A New Heart: A Commentary on the Book of Ezekiel, International Theological Commentary, (Grand Rapids; Edinburgh: Eerdmans; Handsel Press, 1991), 136–137].

Nabii anataka watu wa uhamisho watambue kwamba matumaini yoyote wanayoweza kuwa nayo kwa ajili ya Yuda kwa msingi wa shirikisho lolote na Misri yatakuwa bure! Kama ilivyokuwa kwa Yuda, Misri vilevile inasimama chini ya hukumu ya Mungu. Utekelezaji wa hukumu hii utadhihirisha utakatifu wa Mungu kwa Misri — “Na watu wote wakaao Misri watajua (watafahamu na kutambua) kuwa Mimi ndimi BWANA [Mtawala Jalali, anayeitisha uaminifu na utumishi mtiifu]” (Ezekieli 29:6a, AMP)

Wapendwa, dhambi ya kiburi ni “dhambi ya dhambi zingine.” Ni dhambi hii, tunaambiwa, ndiyo ilileta anguko la Lusifa: Moyo wako uliinuka kwa sababu ya uzuri wako.” (Eze. 28: 17a). Kwa usomaji zaidi angalia — (Isa. 14:12-15; cf. Eze. 28:12-19).

Kiburi kinaweza kutuingiza kwenye taabu kubwa. Kiburi ni hatari kwenye na humchukiza Mungu. Tunapojawa kiburi, huwa na athari nyingi katika maisha yetu: humhafifisha Kristo maishani mwetu; huharibu mahusiano; na juu ya yote, husema uongo – tunadhani tuko huru na hatuhitaji msaada wa Mungu. Usiwe na kiburi. Kumbuka, Kristo alionya — “Na yeyote atakayejikweza, atadhiliwa; na yeyote atakayejidhili, atakwezwa.” (Mathayo 23:12)


 

Iweni na Usiku Mwema: “Msitende neno lolote kwa mashindano ya ubinafsi wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu wahesabuni wengine kuwa bora zaidi kuliko ninyi wenyewe. Hebu kila mmoja wenu asiangalie tu maslahi yake mwenyewe, bali pia maslahi ya wengine.” (Wafilipi 2:3–4, ESV)

Comments
Print Friendly, PDF & Email