Walawi 1: Usomaji/ Vidokezo

April 14, 2022 in Usomaji/ Vidokezo by TGVS

3-BSG-1C: USOMAJI WA BIBLIA.

Usomaji wa Biblia kwa Mpango/ Kitabu cha Mambo ya Walawi 1/ Dhima: Sadaka ya Kuteketezwa.


Walawi 1:

1 Bwana akamwita Musa, na kusema naye kutoka katika hema ya kukutania, akamwambia,
Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Mtu wa kwenu atakapomtolea Bwana matoleo, mtatoa matoleo yenu katika wanyama wa mifugo, katika ng’ombe na katika kondoo.
Matoleo yake kwamba ni sadaka ya kuteketezwa ya ng’ombe, atatoa ng’ombe mume mkamilifu; ataleta mlangoni pa hema ya kukutania, ili akubaliwe mbele ya Bwana.
Kisha ataweka mkono wake juu ya kichwa cha hiyo sadaka ya kuteketezwa; nayo itakubaliwa kwa ajili yake, ili kufanya upatanisho kwa ajili yake.
Naye atamchinja huyo ng’ombe mbele ya Bwana; kisha wana wa Haruni, hao makuhani, wataileta karibu hiyo damu, na kuinyunyiza damu yake kando-kando katika madhabahu iliyo hapo mlangoni pa hema ya kukutania
Kisha atachuna sadaka ya kuteketeza na kuikata vipande vyake.
Kisha wana wa Haruni, watatia moto juu ya madhabahu, na kuzipanga kuni juu ya moto,
kisha wana wa Haruni, makuhani, watazipanga kuni zilizo juu ya moto uliopo juu ya madhabahu;
lakini matumbo yake, na miguu yake, ataiosha kwa maji; na huyo kuhani ataviteketeza vyote juu ya madhabahu, ili iwe sadaka ya kuteketezwa, dhabihu ya kusongezwa kwa njia ya moto, ya harufu ya kupendeza kwa Bwana.
10 Na matoleo yake kwamba ni katika kundi, katika kondoo, au katika mbuzi, kuwa sadaka ya kuteketezwa; atatoa mume mkamilifu.
11 Naye atamchinja hapo upande wa madhabahu ulioelekea kaskazini mbele za Bwana; na wana wa Haruni, hao makuhani, watainyunyiza damu yake juu ya madhabahu pande zote.
12 Kisha atamkata vipande vyake, pamoja na kichwa chake, na mafuta yake; kisha atavipanga vile vipande juu ya kuni zilizo juu ya madhabahu;
13 lakini matumbo yake, na miguu yake, ataosha kwa maji; na huyo kuhani atavisongeza vyote na kuviteketeza juu ya madhabahu; ni sadaka ya kuteketezwa, dhabihu ya kusongezwa kwa njia ya moto, ya harufu ya kupendeza kwa Bwana.
14 Na matoleo yake atakayomtolea Bwana kuwa sadaka ya kuteketezwa, kwamba ni katika ndege, ndipo atakapoleta matoleo yake katika hua au katika makinda ya njiwa.
15 Kisha kuhani atamleta karibu na madhabahu, naye atamkongonyoa kichwa, na kumteketeza kwa moto juu ya madhabahu; na damu yake itachuruzishwa kando ya madhabahu;
16 kisha atakiondoa kile kibofu chake, pamoja na taka zake, na kukitupa kando ya madhabahu upande wa mashariki, mahali pa majivu;
17 kisha atampasua na mabawa yake, lakini asimkate vipande viwili; kisha kuhani atamteketeza juu ya madhabahu, juu ya kuni zilizo juu ya moto; ni sadaka ya kuteketezwa, dhabihu ya kusongezwa kwa njia ya moto, ya harufu ya kupendeza kwa Bwana.

 

3-BSG-1D: MDOKEZO WA SURA.

Mwongozo wa Kujifunza Biblia/ Muhtasari wa Sura/ Walawi 1, (3-BSG-1D)/ Maudhui: Sadaka ya Kuteketezwa.

Wahusika: Mungu, Musa, Makuhani (Wana wa Haruni), Mwabudu/ (mdhambi/ mtoa-sadaka).

Andiko Kuu: “Kisha ataweka mkono wake juu ya kichwa cha hiyo sadaka ya kuteketezwa; nayo itakubaliwa kwa ajili yake, ili kufanya upatanisho kwa ajili yake.” (Walawi 1:4)

Neno Kuu: 1. Upatanisho (Law. 1:4)/ Kiebrania: Kipper = kufunika, kufuta, kukosha, kunadhifisha, au kusibusha. Kiyunani: katallagḗ, “usafianaji.” 2. A “harufi tamu” kwa BWANA (Law. 1:9, 13, 17)/ Kiebrania: Reach Nichoach = manukato yatulizayo.

Virai Teule —Kutoka katika Maskani ya kukutania (1:1); Dhabihu ya Kuteketezwa ya ng’ombe (1:3); Mwanamume asiye na kasoro (1:3); Aliyetolewa “kwa hiari yake mwenyewe” (1:3); mlangoni pa hema ya kukutania, mbele ya BWANA (1:3); Ataweka mkono wake “juu ya kichwa cha sadaka ya kuteketezwa” (1:4); Itakubaliwa kwa ajili yake”  (1:4); “ili kufanya upatanisho kwa ajili yake” (1:4); Dhabihu ya Kuteketezwa — sadaka itolewayo kwa moto, “harufu ya kupendeza kwa BWANA” (1:9, 13, 17).

Maandiko Makini: Walawi 1:1-2, 3-4, 5, 6, 7, 8, 9, 13, 14, 17.

Mgawanyo wa Mawazo Makuu

  1. Dibaji: Mungu anazungumza na Musa kutoka kwenye Maskani, Kiti cha Rehema (1) cf. Kut. 40:34-38.
  2. Aina za matoleo ya kumpendeza BWANA: Mifugo—Ng’ombe, mbuzi na kondoo (2)
  3. Nini cha kufanya Mdhambi anapoleta Sadaka kwa BWANA (3)
  4. Kuungama Dhambi & Kuhamisha Hatia (4)
  5. Utaratibu wa Sadaka ya kuteketezwa — Utaratibu wa kutoa Fahali (5–9); Utaratibu wa kumtoa kafara Kondoo au Mbuzi (10–13); Utaratibu wa kumtoa kafara Ndege (14–17)

Matukio ya Biblia: [Matukio yanayofanyika]—

  1. Kutoka Misri • Kut. 1:8–Dt 34:8
  2. Waisraeli wanatanga-tanga nyikani • Kut. 12:33–Kumb 34:8
  3. Mungu anamwagiza Musa awaelekeze watu kuhusu matoleo • Law. 1:1–7:38
  4. Ukuhani umeanzishwa • Law. 1:1–9:24
  5. Waisraeli wanajenga maskani • Law. 1:1–27:34

Mdokezo wa Mambo Muhimu —Kuuendea uwepo wa mtukufu wa Yehova; Kutokuwa na lawama; Kujiwakifisha/ Kujitakasa kwa Mungu; Kuweka mikono; Sadaka ya hiari; Inayompendeza Mungu (harufu nzuri); Mbadala: Kifo cha mbadala cha Yesu Kristo.

Uchunguzi wa Muktadha Msingi —Kanuni za Sheria za Kale na Walawi; Damu na dhabihu za Agano la Kale; Kafara za wanyama ili kuituliza miungu; Kaida ya Kiyunani ya utakaso vs. utakaso wa Israeli kwa kutumia damu kwenye sehemu ya patakatifu (angalia Law. 1:5).

Mambo ya Kujifunza Zaidi— Upatanisho, Ukuhani wa Walawi, Kazi za Makuhani, Utangulizi wa Walawi, Pentatuki, Jinsi ya Kujifunza Biblia, Aina za Sadaka katika Agano la Kale.

Wazo Muhimu: Katika kiini cha Pentatuki (vitabu vitano vya Musa), msingi wa Biblia nzima, Walawi ina hotuba halani (moja kwa moja) zaidi kutoka kwa Mungu kuliko kitabu kingine chochote cha Biblia. Hapo awali Mungu alizungumza akiwa Mlima Sinai, lakini sasa, anawasiliana kutoka kwenye Kiti cha Rehema (katika Patakatifu). Mungu ana ujumbe maalum kwa watu Wake kuhusu ibada na maisha matakatifu. Ni muhimu kutambua kwamba Mungu, na siyo mwanadamu, ndiye alianzisha na kubuni njia husika ya kuufikia uwepo Wake. Mungu alimteua mpatanishi (Musa) ili kudhihirisha njia (mpango) huu. Mungu alifungua njia kwa ajili ya wote – matajiri, wasio tajiri, na maskini — kutafuta upatanisho kupitia dhabihu. Mungu aliwaambia matajiri jinsi ya kumkaribia (Law. 1:3–9). Alimwambia mtu wa kawaida jinsi ya kumkaribia (Law. 1:10–13). Mwisho, aliwaambia maskini jinsi ya kumkaribia (Law. 1:14–17). Sadaka ya kuteketezwa ilijumuisha mnyama kama vile ng’ombe, kondoo, na ndege. Sadaka za Kuteketezwa ziliwafundisha wadhambi (waliotengwa na Mungu kwa dhambi) kwamba wangeweza tu kuja Kwake kupitia dhabihu kamili ya Mwanawe mpendwa, ambaye angejitoa Mwenyewe “mara moja tu” (Ebr. 7:27; Yohana 1:29; 3:16). Mpendwa, ndivyo Mungu anavyokupenda na anataka urudi Kwake wakati ukiwa umetengwa Naye!

Sura hii inatoa wito kujiwekwa wakfu kikamilifu, kama inavyooneshwa katika Sadaka ya Kuteketezwa (angalia Law. 1:5-9). Wazo la kujiweka wakfu kabisa ni pana sana kwa akili ya kipagani kulielewa, lakini Mungu hakubali kujiweka wakfu kwa sehemu tu. Kujiweka wakfu kwa mtoto wa Mungu ni kuisalimisha nafsi kikamilifu kwa ajili ya utendaji wa Roho Mtakatifu.

Nasaha: “Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa rehema Zake Mungu, kwamba itoeni miili yenu iwe dhabihu hai, takatifu, impendezayo Mungu, ambayo ndiyo ibada yenu makini. Wala msiufuatishe ulimwengu huu, bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, ili mweze kutambua hakika kile ambacho ni chema na kinachokubalika na utashi timilifu wa Mungu.” (Warumi 12:1–2)

 

 

Comments
Print Friendly, PDF & Email