Walawi 17: Maswali Na Majibu.

April 30, 2022 in Mwongozo wa Biblia by TGVS

Mwongozo wa Kujifunza Biblia/ Mambo ya Walawi 17, (3-BSG-17J)/ Katika aya fupi, jibu Maswali au Mambo Makuu uliyojifunza katika sura hii.


 

[1] Sura hii inahusu nini? (17:1–16) Sheria muhimu ili kuhifadhi upatanisho: makatazo mawili yenye nguvu, moja dhidi ya ibada ya sanamu, na moja dhidi ya kutumia vibaya damu iliyomwagika ya dhabihu.

[2] Nani alikuwa mtoa sheria? Mungu mwenyewe – (Walawi 17:1) Kumbuka kwamba hii ilitolewa kwa uongozi na watu wa kawaida wa Israeli. Sheria ilikuwa amri kali kutoka kwa BWANA mwenyewe!

 

MAKATAZO DHIDI YA IBADA YA SANAMU

[3] Taja makatazo mawili dhidi ya ibada ya sanamu? (17:3-3, 7)

 • Mwabudu hafai kutoa dhabihu yoyote kwa sanamu (angalia mstari wa 7)
 • Asitoe dhabihu mahali popote isipokuwa mahali palipoamriwa na Mungu: “kwenye mlango wa hema ya kukutania.”

[4] Namna gani mtu alipata “hatia” ya umwagaji damu? (17:4) — Kwa kawaida kirai “hatia ya umwagaji damu” kulimaanisha kuchukua maisha ya binadamu kimakosa (Kut 22: 2-3; Tor. 19:10). Lakini endapo mtu alimuuwa mnyama na kumtoa kama dhabihu mahali popote isipokuwa katika patakatifu  (Torati 12: 10-14), mtu huyo angekuwa na hatia ya uhalifu wa sheria hii.

[5] Je, adhabu ya uvunjaji wa sheria hii ilikuwa nini? (17:4) Kukatiliwa mbali—kuhukumiwa, kukataliwa na kutengwa na watu wake.

[6] Ni masharti gani manne yaliyotolewa kwa waabudu sanamu? (17:5-6)

 • Lazima wamkaribie Mungu wa wa kweli (aliye hai) sio sanamu—kupitia dhabihu.
 • Lazima wamkaribie Mungu kupitia Kuhani Mkuu, mpatanishi pekee wa Mungu (ishara ya Kristo)
 • Lazima watafute kukua katika ushirika na Mungu pekee: Kupitia sadaka ya ushirika.
 • Wanapaswa kunyunyizia damu kwenye madhabahu ya Sadaka ya Kuteketezwa: Lengo –kutafuta upatanisho hapo peke yake

[7] Matokeo yalikuwa nini ikiwa watatii? (6c). Mungu alikubali sadaka yao. Alipendezwa na utii huo “kwa harufu” ya dhabihu.

[8] Je, dhambi ya kutisha ilifanywa nini hasa?  (17:7) Ibada ya sanamu iliyotolewa kwa masanamu. — “Hawatatoa tena dhabihu zao kwa sanamu za mbuzi, au pepo, au roho za shamba ambazo wamecheza na kahaba.” (AMP).

[9] Zungumzia juu ya umuhimu na upeo wa sheria dhidi ya ibada ya sanamu (17: 8-9) Hii ilikuwa sheria ya kudumu: “amri ya kudumu” kwa Israeli wote katika vizazi vyao vyote! Sheria hii ilitumika kwa wageni wote na pia kwa Waisraeli wote. Adhabu [kwa ajili ya ibada ya sanamu] ilitumika kwa wageni wote: lazima waondolewe (wakatiliwe mbali) kutoka kwa Mungu na watu wao wenyewe.

 

MAKATAZO DHIDI YA KUTUMIA VIBAYA DAMU ILIYOMWAGIKA YA DHABIHU

[10] Je, hapa kuma makatazo yapi? (17:10) Hawapaswi kula wala kunywa damu!

[11] Je, adhabu kali ya Bwana ilikuwa nini tena kwa mkosaji?

 • “Kisha mtu awaye yote wa nyumba ya Israeli, au miongoni mwa hao wageni wakaao kati yao, atakayekula damu, ya aina yo yote, Nitakunja Uso Wangu juu ya mtu huyo alaye damu, nami nitamkatilia mbali na watu wake.” (Mambo ya Walawi 17:10).
 • Angalizo: Sheria hii ilitolewa kwanza kwa Nuhu kwa kadiri tunavyojua. Alipewa haki ya kula nyama lakini si kula damu (Mwa. 9:4). Makatazo dhidi ya kula damu yanarudiwa mara kadhaa katika Maandiko (Walawi 3:17; 7:26–27; Kum. 12:16, 23; 15:23; 1 Sam. 14:32–35; Ezek. 33:25).

[12] Inamaanisha nini kwamba ‘Uso wa Mungu uliwekwa’ dhidi ya mkiukaji?

 • Hii inarejelea ghadhabu Yake. Mtu awaye yote akila au kunywa damu ya dhabihu, ghadhabu ya Mungu iliwaka dhidi yake.
 • Maana yake, mtu huyo “angekatiliwa mbali” — kukemewa, kuhukumiwa, kuangamizwa, kutengwa na Mungu na kutoka kwa waumini wengine wote—lakini baya zaidi “kutengwa” na Mungu Mwenyewe!

[13] Nini kusudi la makatazo haya? – Damu ni takatifu; Ni kwa ajili ya maisha ya mwanadamu!

 • Ni damu inayotoa uhai kwa mwili
 • Ni damu inayoihuisha roho (upatanisho, msamaha wa dhambi, kuoshe)

[14] Jadili masharti manne dhidi ya kutumia vibaya damu iliyomwagika (12-14):

 1. Sheria hii lazima ieleweke mara kwa mara: hakuna mtu anayepaswa kula damu (mstari wa 10, 12, 14).
 2. Hakuna mtu anayepaswa kufanya unajisi na wanyama waliowindwa (mstari wa 13). Damu ya wanyama pori lazima iangamizwe na kufunikwa na ardhi. Haipaswi kuachwa juu ya ardhi ambapo inaweza kuliwa na wanyama wengine. Hii ingetumia vibaya utakatifu wa damu, utakatifu wa uzima, maisha ambayo mnyama aliyekufa aliishi. (KUMBUKA: Mungu anaheshimu sana heshima ya maisha yote – (viumbe vyote, wakiwemo Wanyama). Fundisho: Thamani ya maisha inapaswa kuheshimiwa sana, bila kujali ni kuimbe cha aina gani, maana Mungu ndiye Muumbaji).
 3. Kila mtu lazima akumbuke sababu ya makatazo haya: damu inatoa uhai kwa mwili. Damu inapaswa kuheshimiwa (mstari wa 14). Maisha mazuri – maisha yote – hutoka kwa Bwana. Ndiyo sababu tumeamriwa, “USIUE.” Yatupasa kujikita katika kuboresha mahitaji ya watu wengine (kwa mfano, wagonjwa, yatima, n.k.) – si kuhatarisha Maisha yao, au kufupisha (kuuwa) Maisha yao. Ndiyo sababu “Kristo alihisi na kufundisha huruma kwa watu wengine. Kwa kweli, kuingia katika ufalme wa mbinguni kunategemea shauku ya kuwa na maslahi katika, na utunzaji wa, wenye njaa, kiu, uchi, na wale walio gerezani (Mt. 25:34–40). Maisha yao yalitoka Kwake, Muasisi wa uzima, na katika kuwahudumia wengine wangemtumikia.” — (The Seventh-Day Adventist Bible Commentary – vol. 1, p. 783).
 4. Kila mtu lazima akumbuke hukumu ya wale wanaokiuka sheria hii—ikiwa atakula damu, kutumia vibaya damu— “angekatiliwa mbali” (mstari wa 14).

[15] Jadili kanuni inayodhibiti ulaji wa wanyama wanaokutwa wamekufa (17:15-16)

 • Ikiwa mtu alimkuta mnyama aliyekufa na kula, alihesabiwa kuwa najisi.
 • Alilazimika kuosha nguo zake na kuoga kwa maji.
 • Alikuwa najisi mpaka jioni.
 • Ikiwa hakufua nguo zake na kuoga mwenyewe, aliwajibika. Hata hivyo, aliwajibika kwa kukiuka sheria dhidi ya kula damu. Alipaswa kukatiliwa mbali.

 

MWISHO/ Bwana Akubariki/ Sauti Ya Injili/ Maswali na Majibu/ Mambo ya Walawi 17.

Comments
Print Friendly, PDF & Email