Usiwe na Miungu Mingine!

May 3, 2022 in Mwongozo wa Ibada by TGVS

Ibada ya Alfajiri: Walawi 20. / USIWE NA MIUNGU MINGINE! / Fungu Kuu: Walawi 20:1-3.


Je BWANA anasema nini asubuhi ya leo? Anasema hivi:

Mwisraeli yeyote au mgeni ye yote anayeishi katika Israeli ambaye hutoa watoto wake kwa Moleki (mungu wa Waamoni) [kama dhabihu ya kibinadamu] hakika atauawa; Watu wa nchi watampiga kwa mawe. Nami nitaweka Uso Wangu dhidi ya mtu huyo – [kumpinga, kuondoa ulizi Wangu kwake] Nami nitamkatilia mbali na watu wake; na Upatanisho hautafanywa kwa ajili yake.

Kwanini? Kwa sababu ya ibada ya sanamu! Kwa sababu amewapa baadhi ya watoto wake kwa Moleki; Kwa sababu amechafua Patakatifu Pangu na kulichafua Jina Langu Takatifu.

Wapendwa leo tunarudi tena katika mada ya “Ibada ya Sanamu.” Kitu chochote kinachukua nafasi ya kwanza katika Maisha yetu ni “Ibada ya Sanamu.” Haya mabo yanaweza yakawa ajira, pesa, mapenzi, tamaa, michezo, n.k. Rejea orodha kamili ya “Matendo ya Mwili” Katika Wagalatia 5:19-23. Hachana na waganga, wachawi, n.k. Elekeza nguvu zako zote katika Mungu wa Kweli. Mtumaini Yeye pekee, naye hakika hatakuacha!

MASWALI YA MOYONI:

  1. Je unahitaji Kupatamishwa na Mungu wako?
  2. Je unahitaji Ulinzi wa Bwana dhidi ya Maadui?
  3. Je unahitaji Kusamehewa, Kuoshwa, na Kutakaswa kwa Umilele?
  4. Je unahitaji Kuwa karibu na Uso wa Bwana (uwepo Wake)?

Kama Jibu ni “NDIYO!.” Hachana na Ibada ya Sanamu.

Hebu kila mmoja wetu ajihoji nafsi yake na kuomba msamaha kwa BWANA na huruma Yake. Kumbuka — “Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu.” [Lakini] – “Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.” (1 Yohana 1:8-9].

 

Iweni na Alfajiri Njema: “Kwa ajili ya hayo, wapenzi wangu, ikimbieni ibada ya sanamu.” (1 Wakorintho 10:14).


 

Ibada katika Wimbo
NENA ROHONI YESU– (NK # 15)
(Speak to My Heart Lord Jesus)

1.
Nena rohoni yesu, Nena kwa upole
Sema kwangu kwa pendo, “Huachwi upweke.”
‘Fungua moyo wangu, Nisikie mara;
Jaza roho na sifa, Sifa zako Bwana.

Kila siku unene, Vile kwa upole,
Nong’oneza kwa pole wa pendo:
“Daima utashinda, Uhuru niwako.”
Nisikie maneno: “Huachwi upweke.”

2.
Nena kwa wana wako, Waonyeshe njia,
Wajaze kwa furaha, Fundisha kuomba;
Wajifunze kutoa Maisha kamili,
Wahimize ufalme, Tumwone Mwokozi.

3.
Nena kama zamani, Ulipoitoa
Sheria takatifu: Niiweke pia;
Nipate kutukuza Wewe Mungu wangu,
Mpanzi yako tena, Daima ‘kusifu.

Comments
Print Friendly, PDF & Email