Walawi 20: Mdokezo wa Sura

May 3, 2022 in Usomaji/ Vidokezo by TGVS

Mwongozo wa Kujifunza Biblia/ Muhtasari wa Sura/ Walawi 20, (3-BSG-20D)/ Dhamira: Adhabu dhidi ya Ibada ya Sanamu & Dhambi wa Upujufu.


Wahusika: Mungu, Musa, Israeli Wote (pamoja na Wageni waishio Israeli)

Andiko Kuu: “Basi zishikeni amri Zangu zote, na hukumu Zangu zote, na kuzifanya; ili kwamba hiyo nchi, ambayo nawapeleka ninyi kukaa, isiwatapike. Nanyi msiende kwa kuziandama desturi za taifa, niitoayo mbele yenu; kwa kuwa wao waliyafanya mambo hayo yote, na kwa ajili ya hayo niliwachukia.” (Walawi 20:22–23)

Neno Kuu: Waliotengwa (fasili ya 24, 26).

Virai Teule —Hakika atauawa; Nitaukaza uso Wangu juu ya mtu huyo; Nitamkatilia mbali na watu wake; Kufunua uchi wake; Mtakuwa watakatifu Kwangu; Mimi ndimi BWANA!

Maandiko Makini: Walawi 20:1-3, 6, 8, 22, 23, 24.

Mgawanyo wa Mawazo Makuu: Adhabu ya Dhambi za Kuabudu Sanamu – Ibada ya Moleki (1–5); Kujihusisha na Ushirikina (6–8); Kuwa Pepo au Mtendaji wa Ushirikina (27)

Adhabu za Dhambi za Uasherati — Laana ya Mzazi (9); Uzinzi (10); Dhambi za Maharimu (11–12); Ushoga (13); Kumwoa Mwanamke na Mamaye (14); Kufanya mapenzi na wanyama (15–16); Dhambi Zingine za Kimapenzi (17–21)

Muhtasari: Kwa nini Mungu aliita Israeli kwenye utakatifu kama huo (22–26)

Matukio ya Biblia: [Matukio yanayofanyika]—

  1. Kutoka Misri, (Kut. 1:8–Kumb 34:8)
  2. Waisraeli wanatanga nyikani (Kut. 12:33–Kumb 34:8)
  3. Waisraeli wanajenga hema la kukutania (Law. 1:1–27:34)
  4. Mungu anamwagiza Musa na Haruni kuhusu ukuhani (Law. 11:1–26:46)
  5. Mungu anamwagiza Musa kuhusu utakatifu (Law. 17:1–24:9)

Mdokezo wa Mambo Muhimu — Utakatifu na nafasi Takatifu katika kambi ya Israeli; Uhalifu ambao Adhabu ya Kifo imeagizwa; Mimi ndimi BWANA!

Uchunguzi wa Muktadha Msingi — Moleki: Miungu ya Wakanaani anayehusishwa na kafara ya watoto.

Mambo ya Kujifunza Zaidi —Ibada ya Sanamu (uzinzi wa kiroho); Umizimu, usihiri (kuwa au kuwasiliana na pepo wabaya); Ukengeufu katika AK; Watoto – (majukumu kwa wazazi); Vipengele vya kimaadili vya Utakatifu; Ukuaji wa waumini katika Kristo (katika Utakatifu); Asili na msingi wa Utakaso; Upinzani wa dhambi na uovu.

Wazo Makini: Dhamira kuu katika sura hii ni “Utakatifu”—Kujitengana na kile kisicho safi, kutakaswa, au kuwekwa wakfu. Ibada ya Moleki lazima ifutiliwe mbali! Kwa ajili ya mjadala kuhusu “Moleki” na kwa nini Mungu alipiga marufuku ibada yake, tazama kipengele cha “3-BSG-20J” katika Mwongozo wa Kujifunza. Ibada ya Moleki, miongoni mwa mambo mengine, ilichukiwa na Yehova kwa sababu ilitia unajisi patakatifu. Kumbuka, uchafu hunajisi, na hivyo, kumfukuza Mungu asikae kwenye kambi la Israeli (Kut. 25:8). Israeli lazima wahukumu na kuwaadhibu wale wanaowatoa kafara watoto kwa Moleki (Law. 20:3a; 18:21). Ikiwa watashindwa kutekeleza hiyo adhabu ya kifo, Mungu atawafanyia karet (kukatiliwa mbali) kwa uzao (Law. 20:4–5).

Mpendwa, Mungu amewatofautisha watu Wake (Israeli wa kale na Sisi) dhidi ya wengine wote kwa “agano takatifu” kupitia Yesu Kristo. Kwa hiyo, ni lazima tujitenge na dhambi na wasioamini; na kuishi maisha matakatifu (utakaso). Hebu sura hii itusaidie sisi sote, tukue katika Kristo, Amina.

Mausia: “Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha.” (2 Wakorintho 6:17)

 

3-BSG-20C: SURA YA LEO
Usomaji wa Biblia kwa Mpango/ Kitabu cha Mambo ya Walawi 18/ Dhima: Adhabu dhidi ya Ibada ya Sanamu & Dhambi wa Upujufu.


MAMBO YA WALAWI 20

1 Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia,
Tena uwaambie wana wa Israeli, Mtu awaye yote miongoni mwa wana wa Israeli, au miongoni mwa wageni waketio katika Israeli, atakayetoa katika kizazi chake na kumpa Moleki, sharti atauawa; wenyeji wa nchi watampiga kwa mawe.
Mimi nami nitamkazia uso wangu mtu huyo, nami nitamkatilia mbali na watu wake; kwa kuwa ametoa katika kizazi chake na kumpa Moleki, ili kupatia unajisi patakatifu pangu, na kulinajisi jina langu takatifu.
Tena kama wenyeji wa nchi wakimfumbia macho mtu huyo kwa njia yo yote, hapo atoapo katika kizazi chake na kumpa Moleki, wasimwue;
ndipo mimi nitamkazia uso wangu mtu huyo, na jamaa zake, nami nitamkatilia mbali, na hao wote wamwandamao katika uzinifu, ili kufanya uzinifu pamoja na Moleki, watengwe mbali na watu wao.
Na mtu yule atakayewaendea wenye pepo, na wachawi, ili kuzini pamoja nao, nitakaza uso wangu juu ya mtu yule, nitamtenga na watu wake.
Jitakaseni basi, iweni watakatifu, kwa kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.
Nanyi zishikeni sheria zangu, na kuzitenda; Mimi ndimi Bwana niwatakasaye ninyi.
Kwa maana kila mtu amlaaniye baba yake au mama yake hakika atauawa, amemlaani baba yake na mama yake; damu yake itakuwa juu yake.
10 Na mtu aziniye na mke wa mtu mwingine, naam, yeye aziniye na mke wa jirani yake, mtu mume aziniye, na mwanamke aziniye, hakika watauawa.
11 Na mtu mume atakayelala pamoja na mke wa baba yake amefunua utupu wa baba yake; wote wawili hakika watauawa; damu yao itakuwa juu yao.
12 Na mtu mume akilala na mkwewe mwanamke wote wawili hakika watauawa; wamefanya yaliyo uchafuko; damu yao itakuwa juu yao.
13 Tena mtu mume akilala pamoja na mtu mume, kama alalavyo na mtu mke, wote wawili wamefanya machukizo; hakika watauawa; damu yao itakuwa juu yao.
14 Tena mtu mume akimwoa mke pamoja na mama yake, ni uovu mkuu; watachomwa moto, yeye mume na hao wanawake pia; ili kwamba usiwe uovu kati yenu.
15 Tena mtu mume akilala na mnyama, hakika atauawa; nanyi mtamwua huyo mnyama.
16 Tena mwanamke akimkaribia mnyama ye yote, na kulala pamoja naye, mtamwua huyo mwanamke, na mnyama pia; hakika watauawa; damu yao itakuwa ni juu yao.
17 Tena mtu mume akimwoa umbu lake, binti ya baba yake, au binti ya mama yake, na kuuona utupu wake, na huyo mwanamke kauona utupu wake huyo mume; ni jambo la aibu; watakatiliwa mbali mbele ya macho ya wana wa watu wao; amefunua utupu wa umbu lake; naye atauchukua uovu wake.
18 Tena mtu mume akilala na mwanamke aliye na ugonjwa wake, na kufunua utupu wake; amelifunua jito la damu yake, naye mwanamke amefunua jito la damu yake; wote wawili watakatiliwa mbali na watu wao.
19 Usifunue utupu wa umbu la mama yako, wala umbu la baba yako; kwa kuwa huyo amefunua utupu wa jamaa yake ya karibu; watauchukua uovu wao.
20 Tena mtu mume akilala na mke wa mjomba wake, ameufunua utupu wa mjomba wake; watauchukua uovu wao; watakufa bila kuzaa mwana.
21 Tena mtu mume akimtwaa mke wa nduguye, ni uchafu; ameufunua utupu wa nduguye; hao watakuwa hawana wana.
22 Basi zishikeni amri zangu zote, na hukumu zangu zote, na kuzifanya; ili kwamba hiyo nchi, ambayo nawapeleka ninyi kukaa, isiwatapike.
23 Nanyi msiende kwa kuziandama desturi za taifa, niitoayo mbele yenu; kwa kuwa wao waliyafanya mambo hayo yote, na kwa ajili ya hayo niliwachukia.
24 Lakini mimi nimewaambia ninyi, Mtairithi nchi yao, nami nitawapa ninyi kuimiliki; nchi iliyojaa maziwa na asali; mimi ni Bwana, Mungu wenu, niliyewatenga ninyi na mataifa.
25 Kwa ajili ya hayo mtapambanua kati ya mnyama aliye safi na mnyama aliye najisi, na kati ya ndege aliye tohara na ndege aliye najisi; nanyi msizifanye nafsi zenu kuwa machukizo kwa njia ya mnyama, au kwa njia ya ndege, au kwa njia ya kitu cho chote ambacho nchi imejaa nacho, niliowatenga nanyi kuwa ni najisi.
26 Nanyi mtakuwa watakatifu kwangu mimi; kwa kuwa mimi Bwana ni mtakatifu nami nimewatenga ninyi na mataifa, ili kwamba mwe wangu.
27 Tena mtu mume au mtu mke aliye na pepo, au aliye mchawi, hakika atauawa; watawapiga kwa mawe; damu yao itakuwa juu yao.

 

Comments
Print Friendly, PDF & Email