Anza na Bwana, July 28, 2022

July 28, 2022 in Alfajiri, Mwongozo wa Ibada by TGVS

Anza na Bwana!
Alhamisi: July 28, 2022.


 

KUFANYA MKATABA NA ADUI (Yoshua 9:3-14)

Katika sura hii, Yoshua kimakosa anafanya mkataba na adui, Wagibeoni. Yoshua alifanya kosa gani katika uamuzi wa kuwakubali watu wa Gibeoni? (9:14) Alichunguza chakula chao, lakini hawakushauriana na Bwana!

Je, tunawezaje kujua mapenzi ya Mungu kwetu? Mungu anafurahia kufunua mapenzi Yake kwa watoto Wake wanapokuwa wanyenyekevu na wenye utayari wa kutii. Mapenzi ya Mungu yanatoka katika moyo wa Mungu (Zaburi 33:11). Wapendwa, hatutafuti mapenzi ya Mungu kama “wateja” wanaoangalia chaguzi (au bidhaa mbalimbali sokoni), lakini kama “watumishi” wanaosikiliza maagizo. “Ikiwa mtu yeyote anashauku ya kufanya mapenzi Yake (radhi ya Mungu), atajua (atakuwa na mwangaza unaohitajika kutambua” – (Yohana 7:17, AMP)

Hii ndiyo kanuni ya msingi ya maisha ya Kikristo ya ushindi. Mungu anaona mioyo yetu na anajua kama kweli tuko makini kuhusu kumtii. Hakika, tunapaswa kutumia akili ambayo Mungu ametupatia, lakini lazima tuzingatie onyo la Mithali 3:5-6 na tusitegemee ufahamu wetu wenyewe.

Ibada ya Maombi (Alfajiri).
[1] “Naomba niombewe Bwana anipatie ratiba ya maombi na familia yangu” (SM); [2] “Umaliziaji wa Nyumba yangu ununuzi wa bati na mbao” (SM); [3] “Wadogo zangu Loius, Samweli, Neema & Veronica- Wapate kuifahamu kweli” (SM); [4] “Naombeni maombi yenu ya kiafya pia, maana nina udhaifu wa kiafya” (MA); [5] Ombea watendakazi wote waliyo shambani mwa Bwana; [6] Ombea huduma hii ya Injili: ili kwamba wengi waokolewe, waingie mbinguni; [7] Ombea fedha kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Injili; [8] Ombea wongofu katika “mikutano ya makambi” inayoendea sehemu mbalimbali; [9] Ombea wagonjwa, walemavu, wanaoteswa kwa ajili ya Injili; [10] Ombea shauku ya kuutafuta uso wa Bwana na kutafuta mapenzi yake kabla hatujafanya maamuzi maishani — Tujifunze kanuni hii muhimu katika sura ya leo: Yoshua 9.

SALA: Baba, asante tena kwa siku mpya ya leo. Sisi ni wakosaji mbele zako. Tunaomba msamaha wa dhambi zetu. Hebu Roho wako azungumze na kila mmoja wetu na kutuelekeza katika kweli za Neno lako. Baba umeona mahitaji ya leo, ukapate kuwabariki Watoto wako sawasawa na Fadhili zako. Tumeomba haya katika jina la Yesu Kristo, Mkombozi wetu, Amina.


 

AHADI YA LEO:

Dhima: Utambuzi wa Mapenzi ya Mungu kwetu

  • “Shauri la Bwana lasimama milele, Makusudi ya moyo wake vizazi na vizazi. Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao, Watu aliowachagua kuwa urithi wake.” (Zaburi 33:11-12).
  • “Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako.” – (Mithali 3:5-6)

Je una Mzigo wowote? Je una Jambo la kumshukuru Bwana? Je unao Wimbo wowote? Je una Ushuhuda wowote? Karibu Mpendwa: Nafasi hii ni yako…


TUNAKARIBISHA:

  • Nyimbo za Injili
  • Ushuhuda
  • Maombi (Sala)
  • Kesha la Asubuhi
  • Mahitaji (Changamoto za Kuombea).

Au, Jambo lolote la kiroho ambalo unaguswa kushirikisha watu wa Mungu. Bwana Awabariki.

 

 

Comments
Print Friendly, PDF & Email