Yoshua 9: Maswali na Majibu

July 28, 2022 in Mwongozo wa Biblia by TGVS

Mwongozo wa Kujifunza Biblia/ Yoshua 9, (6-BSG-9J)/ Katika ibara fupi, jibu maswali au andika mawazo makuu uliyojifunza kuhusu sura hii.


[1] Je, unaweza kuandika muhtasari wa sura za Yoshua 1 hadi 9? Ndiyo.

 • Yoshua 1, Utume wa Yoshua.
 • Yoshua 2, Uongofu wa Rahabu.
 • Yoshua 3, Kuvuka Yordani.
 • Yoshua 4, Mawe ya Ukumbusho.
 • Yoshua 5, Utayari wa Kiroho.
 • Yoshua 6, Kupiga Kelele hadi Kuiangusha Yeriko.
 • Yoshua 7, Ai: Uasi na Kushindwa.
 • Yoshua 8, Ai: Utii na Ushindi.
 • Yoshua 9, Mkataba Potofu na Wagibeoni.

[2] Sura hii inahusu nini hasa? Waisraeli wapigana na wafalme ng’ambo ya Yordani (9:1–27)

 • “Baada ya kuyahadaa majeshi huko Ai, Israeli ikakabiliwa na hila ya Wagibeoni. Huku wakijifanya wanatoka katika nchi za mbali, Wagibeoni wenye wasiwasi wanashinikiza majeshi ya Israeli kufanya mapatano nao mara moja. Baada ya kukubaliana, Israeli inakasirishwa na ghiliba ya Wagibeoni lakini hawatabatilisha kiapo chao cha kutowadhuru (tofauti na Sauli; 2 Sam 21:2). Matokeo yake, Wagibeoni wanalazimika kutumikia Israeli na madhabahu ya Bwana kwa kukidhi kuni na maji. (Sulemani mwenyewe atatumia madhabahu ya Gibeoni katika 1 Fal. 3.) Kwa kufanya hayo yote, Wagibeoni yaelekea walivunja imani na muungano wa Waamori ulioongozwa na mfalme wa Yerusalemu na kuzusha migogoro ijayo.” – [Douglas Mangum, Ed., Lexham Context Commentary: Old Testament, Lexham Context Commentary, (Bellingham, WA: Lexham Press, 2020), Jos 9:1–27].

[3] Akina nani waliokusanyika katika muungano ili kupigana na Yoshua na Israeli? (9:1-2) Wafalme wote walio magharibi mwa Yordani katika vilima na mabonde na kando ya pwani ya bahari ya Mediterania kaskazini kuelekea Lebanoni—Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi, Wagirgashi, na Wayebusi.

[4] Wenyeji wa Gibeoni walifanya nini waliposikia yale Yoshua aliyoyatenda Yeriko na Ai? (9:4) Walitenda kwa hila na ujanja na kwenda kwa Yoshua, wakijifanya kuwa mabalozi.

[5] Wanaume wa Gibeoni walifanya matayarisho gani kwa ajili ya safari yao kwenda kwa Yoshua huko Gilgali? (9:4-5) Walichukua mahitaji yafuatayo:

 • Magunia chakavu juu ya punda wao.
 • Viriba vilivyochakaa (chupa za ngozi) vilivyopasuka na kushonwa.
 • Viatu vilivyochakaa venye viraka miguuni pao.
 • Nguo – (zilizochakaa).
 • Na masurufu ya vyakula vyao vyote yalikuwa yamekauka na kugeuka makombo.

[6] Walipofika kwenye kambi ya Israeli huko Gilgali, Wagibeoni walimwambia nini Yoshua na wanaume wa Israeli? (9:6) “Tumetoka nchi ya mbali; basi sasa fanyeni agano (mapatano) nasi.”

[7] Nini ambacho Waisraeli walisema na kuwaambia Wagibeoni wawachunguze wao na nia zao? (9:7) “Pengine mnaishi katika nchi yetu; basi tufanyeje agano (mapatano) nanyi?”

[8] Watu wa Gibeoni walimwambia Yoshua wao ni nani? (9:8) “Sisi ni waja wako.”

[9] Swali la Yoshua lililofuata kwao lilikuwa lipi? (9:8b) “Ninyi ni nani, na mnatoka wapi?”


Yoshua 9:9–11 9 Wakamwambia: “Watumishi wako wametoka nchi ya mbali sana kwa ajili ya jina la BWANA, Mungu wenu; maana tumesikia habari Zake, na mambo yote aliyoyatenda huko Misri, 10 na yote aliyowatendea wafalme wawili wa Waamori waliokuwa ng’ambo ya Yordani, Sihoni mfalme wa Heshboni, na Ogu mfalme wa Bashani, aliyekuwa huko Ashtarothi. 11 Kwa hiyo wazee wetu na wakazi wote wa nchi yetu wakasema nasi, wakisema, ‘Chukueni vyakula vya safarini, mwende kuwalaki, na kuwaambia, Sisi ni watumishi wenu; basi sasa fanyeni agano nasi.”

 

[10] Je, Wagibeoni walitokea wapi na kwa sababu gani wakaja kwa Yoshua? (9:9-10) Kutoka nchi ya mbali sana; Kufanya mkataba nao!

[11] Ni mambo gani mawili ambayo watu wa Gibeoni walikuwa wamesikia kuhusu Mungu wa Waisraeli? (9:9-10) Umashuhuri Wake, na yote aliyoyafanya Misri.

[12] Ni wafalme gani wawili wa Waamori ambao watu wa Gibeoni waliwajua? (9:10) Mfalme Sihoni wa Heshboni na Mfalme Ogu wa Bashani (aliyeishi Ashtarothi).

[13] Watu wa Gibeoni walisema wametumwa na nani kwa Yoshua? (9:11) Wazee wao na wananchi wenzao.

[14] Chunguza mambo manne ya uongo ambayo Wagibeoni walimwambia Yoshua (9:6-13)

 1. Kwanza, walisema walikuwa “wakitokea nchi ya mbali sana” (Yos. 9:6, 9) ilhali waliishi maili ishirini na tano tu kutoka hapo.
 2. Pili, walidanganya kuhusu mavazi na chakula chao: “Mkate huu ulikuwa wa moto kutoka kwenye oveni tulipotoka nyumbani. Lakini sasa, kama unavyoona, ni kavu na kuingia koga.” (Yoshua 9:12, NLT)
 3. Tatu, walidanganya kuhusu wao wenyewe na kueleza mambo yasiyo sahihi kwamba walikuwa wajumbe muhimu kwenye misheni rasmi ya amani kutoka kwa wazee wa mji wao.
 4. Nne, walijiita pia “watumishi wako” (Yos. 9:8, 9, 11), ilhali kihalisia walikuwa maadui wa Israeli.

Kumbuka: “Shetani ni mwongo na baba wa uongo (Yohana 8:44), na asili ya mwanadamu ni kwamba watu wengi wanaona ni rahisi kusema uongo kuliko ukweli. Kwa dhihaka, kiongozi wa kisiasa Marekani Adlai Stevenson alisema, “Uongo ni chukizo kwa Bwana—na ni pia msaada unaopatikana tele wakati wa taabu.” Wagibeoni walisema uongo kadhaa katika jitihada yao ya kujinasua kwenye matatizo.” – [Warren W. Wiersbe, Be Strong, “Be” Commentary Series, (Wheaton, IL: Victor Books, 1996), 107–108].

 • “Mambo haya manne ya uongo yalikuwa mabaya vya kutosha; lakini wageni hao waliposema wamekuja “kwa sababu ya jina la Bwana” (v. 9), ilikuwa kufuru. Kama raia wa Yeriko (2:10), watu wa Gibeoni walikuwa wamesikia kuhusu maandamano ya ushindi ya Israeli (9:9–10); lakini tofauti na Rahabu na jamaa zake, hawakuweka imani yao kwa Bwana. Watu hawa walikuwa na hekima ya kutosha kutotaja ushindi wa Israeli huko Yeriko na Ai; maana habari hiyo isingeweza kufika “nchi yao ya mbali” kwa haraka hivyo. Mabalozi wa Shetani wanaweza kusema uongo unaoshawishi zaidi kuliko baadhi ya Wakristo wawezavyo kusema ukweli!”
 • “Shetani anajua jinsi ya kutumia “uongo wa kidini” ili kudhihirisha kwamba watu wanajaribu kumjua Bwana. Katika huduma yangu ya kichungaji nimekutana na watu ambao wamejitambulisha kuwa watafutaji; lakini kadiri walivyozungumza kwa muda mrefu, ndivyo nilivyoshawishika zaidi kwamba walikuwa wanyemeleaji, wakijaribu kubaini kitu fulani kutoka kwangu na kanisani. Walikuwa wakifanya “maungamo ya imani” na na kisha kuanza kuniambia kisa chao cha madhila ya kuhuzunisha, wakitegemea kuuvunja moyo wangu na kisha wanitapeli. Miongoni mwa waongo wote, “waongo wa kidini” ndio wabaya zaidi. Ikiwa unahitaji kusadikishwa na hili, soma 2 Petro 2 na Waraka wa Yuda.” – [Warren W. Wiersbe, Be Strong, “Be” Commentary Series, (Wheaton, IL: Victor Books, 1996), 108–109].

[15] Je, Yoshua alifanya kosa gani katika uamuzi wa kuwakubali watu wa Gibeoni? (9:14) Alivichunguza vyakula vyao, lakini hakutafuta ushauri wa Bwana!

 • “Kwa nini walifanikiwa (Yos. 9:14–15). Sababu ni rahisi: Yoshua na wakuu wa Israeli walikuwa na harara na wala hawakutumia muda kupata mashauri ya Bwana. Walitembea kwa kuona na wala si kwa imani. Baada ya kusikiliza hotuba ya wageni hao na kuchunguza uthibitisho huo, Yoshua na viongozi wake walikata kauli kwamba watu hao walikuwa wakisema kweli. Viongozi wa Israeli walikubali “mtazamo wa kisayansi” badala ya “mtazamo wa kiroho.” Walitegemea fahamu zao wenyewe, wakachunguza “taarifa,” wakajadiliana kuhusu jambo hilo, na kukubaliana katika hitimisho lao. Yote yalikuwa ya kimantiki na yenye kushawishi, lakini hayakuwa sahihi kabisa. Walikuwa wamefanya kosa lilelile kule Ai (sura 7) nao hawakuwa wamejifunza kumngoja Bwana na kutafuta mwongozo Wake.” – [Warren W. Wiersbe, Be Strong, “Be” Commentary Series, (Wheaton, IL: Victor Books, 1996), 109].

[16] Yoshua alifanya mapatano gani pamoja na watu wa Gibeoni? (9:15) Mkataba wa amani na adui; aliwahakikishia usalama wao, na viongozi wa jamii hiyo wakaidhinisha makubaliano yao kwa “kiapo taadhimu.”

 • “Endapo kikundi cha watu hawa kingekuwa wajumbe rasmi, kingejumuisha kundi kubwa zaidi lenye mahitaji ya kutosha, ikiwa ni pamoja na masurufu ya kutosha kwa ajili ya safari ya kurudi nyumbani. Mabalozi wa kweli wangetupilia mbali mkate wao “mkavu na wenye koga” kwa sababu watumishi wao wangewaokea mikate safi. Kama maofisa, wangekuwa wamesheheni mavazi yanayofaa ili waweze kuleta mvuto bora zaidi kadiri iwezekanavyo wakati wakijadiliana na adui. Kama Yoshua na viongozi wake wangetulia ili kufikiria na kuomba juu ya kile walichokiona, wangekata kauli kwamba tukio hilo zima lilikuwa hila. “Lakini yeyote miongoni mwenu akipungukiwa na hekima, hebu aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei, naye atapewa” (Yakobo 1:5, NKJV).”
 • “Imani ya kweli inahusisha kuwa na subira (Ebr. 6:12). “Yeye aaminiye hatatenda kwa harara” (Isa. 28:16, NKJV). Musa alikuwa amewaambia Wayahudi, “Jihadharini msifanye mapatano na wale wakaao katika nchi mnayoiendea, la sivyo watakuwa mtego miongoni mwenu” (Kut. 34:12, NIV). Lakini katika harara yao Yoshua na viongozi Wayahudi walivunja Sheria ya Mungu na kufanya agano pamoja na adui. Kwa kuwa kiapo chao kiliapwa kwa jina la Bwana (Yos. 9:18), hakingeweza kuvunjwa. Yoshua na wakuu wa Israeli walikuwa wameapa wakichelea madhara juu yao wenyewe (Zab. 15:4; Mhu. 5:1–7), na haikuwepo njia ya kubatilisha kiapo chao au kuachiliwa kwenye ahadi yao.”
 • “Kama Yoshua na taifa la Israeli, watu wa Mungu leo ​​wanaishi katika eneo la adui na wanapaswa daima kuwa waangalifu. Unapomwamini adui badala ya kutafuta nia ya Bwana, unaweza kutarajia kujitosa kwenye masaibu.” – [Warren W. Wiersbe, Be Strong, “Be” Commentary Series, (Wheaton, IL: Victor Books, 1996), 109–110].

[17] Ni siku ngapi zilikuwa zimepita kabla Yoshua na watu wa Israeli hawajajua kwamba wale waliodhaniwa kuwa “wajumbe rasmi” kutoka “nchi ya mbali” walikuwa walaghai, majirani, na maadui? (9:16) Siku tatu baada ya kufanya agano hili.

[18] Basi, nini kilitokea baadaye? (9:17) Wana wa Israeli walivunja kambi na kuondoka; siku tatu baadaye wakafika miji ya Wahivi, Gibeoni, Kefira, Beerothi, na Kiriath-yearimu.

[19] Kwa nini Waisraeli hawakuwapiga Wahivi? (9:18) “Kwa sababu wakuu wa kusanyiko walikuwa wamewaapia kwa Bwana, Mungu wa Israeli [kutowadhuru]. Na kusanyiko lote likanung’unika [kuonesha kutoridhika kabisa] dhidi ya viongozi hao.” (AMP).

[20] Ikiwa Waisraeli wasingewaacha Wahivi waishi nini kingewapata na kwa nini? (9:20) Hawakuwa na chaguo linginelo, ila “kuwaacha waishi!” Iwapo wangewashambulia, basi ghadhabu ya Mungu ingewapataa kwa kukiuka kiapo walichofanya baina ya pande hizo mbili.

[21] Nani aliamua hatima ya Wahivi na hatima hiyo ilikuwa ipi? (9:21) Viongozi wa Israeli. Walifanya pendekezo la kuruhusu Wahivi waishi kama watumwa wa Israeli — “Basi wakawa wakataji na wakusanyaji kuni na watekaji wa maji kwa ajili ya kusanyiko lote, kama vile viongozi walivyosema juu yao.” (AMP).

[22] Je, Yoshua aliwabariki au kuwalaani watu wa Gibeoni waliowadanganya watu wa Israeli? (9:23) Aliwalaani.

[23] Ni watu wangapi wa Gibeoni wangeachiliwa wasiwe watumwa wa Israeli? (9:23) Hakuna.

[24] Nini walichokuwa wameambiwa Wahivi kilichowafanya wahofie sana maisha yao? (9:24) Waliambiwa kwa hakika kwamba Yehova “alimwamuru Musa mtumishi Wake awape ninyi nchi yote, na kuwaangamiza wenyeji wote wa nchi mbele yenu; tulihofia sana maisha yetu kwa sababu yenu, ndipo tukafanya jambo hili [la udanganyifu].”

[25] Je, watu wa Gibeoni walijitia mkononi mwa nani? (9:25) Mikono ya Israeli. Angalia jinsi walivyosihi —

[26] Wahivi walimwomba Yoshua awatendeeje? Kwa nini? (Yoshua 9:25) “Sasa tazama, sisi tumo mikononi mwako; utufanyie kama unavyoona kuwa ni vyema na sawa machoni pako.” (AMP).

[27] Nini ambacho Yoshua aliwazuia wana wa Israeli wasiwatendee watu wa Gibeoni? (9:25) Aliwaokoa ili Waisraeli wasiwaue.

[28] Je, utaratibu mpya wa kazi ya Wahivi ungekuwaje? (9:27) walifanywa kuwa wapasuaji na wakusanyaji kuni; na wabebaji wa vyombo vya kunywea maji kwa ajili ya kusanyiko na kwa ajili ya madhabahu ya Bwana – “hadi leo” – katika mahali ambapo angepachagua.

Comments
Print Friendly, PDF & Email