Anza na Bwana, Agosti 4, 2022

August 4, 2022 in Alfajiri, Mwongozo wa Maombi by TGVS

URITHI (MGAWO) KWA WANA WA YUSUFU (Yoshua 16:1-10)

Urithi na Mgawanyo wa Ardhi katika Nchi ya Ahadi ndiyo dhima kuu katika Yoshua sura ya 13 hadi 21. Efraimu na Manase walikuwa wana wa Yusufu, ambao mzee Yakobo “aliwarithi” na kubarikiwa sana (Mwa. 48:15–22). Kwa kuwa kabila la Lawi halikupewa eneo lolote, makabila haya mawili yalizazilishia tofauti ili kuwe na makabila kumi na mawili katika Israeli. Utaratibu wa kuzaliwa ulikuwa “Manase na Efraimu” (Yos. 16:4; 17:1), lakini mzee Yakobo aliubadilisha. Utakumbuka kuwa, Mungu alimkubali Abeli na kumkataa Kaini; Alimkataa Ishmaeli na kumkubali Isaka (mwana wa pili wa Ibrahimu); Alimkataa Esau na kumkubali Yakobo.

Hoja Kuu ni hii: Mungu anakataa kuzaliwa kwetu kwa “Mara Ya Kwanza” na kutupa tuzo ya “Kuzaliwa Kwa Pili.” Kuzaliwa kwa mara ya pili pia hujulikana kama “Kuzaliwa Upya” (Yohana 3: 3), kunahusishwa na urithi wa Nchi ya Ahadi ya mbinguni. Hebu Msihi Roho Mtakatifu akubatize upya na kukupatia haki ya “kuzaliwa upya” katika Kristo Yesu. Mwombe Roho Mtakatifu aingie rohoni mwako, akuzae upya, na aanze kazi Yake ya kukubadilisha kuwa mfano wa Kristo (2 Kor. 5:17). Je utafanya hivyo?

 

Ibada Ya Maombi (Alfajiri).
[1] Ombea masomo endelevu na Injili katika Kitabu cha Yoshua; [2] Ombea wagonjwa, wasiyojiweza, walemavu, na wanaoteswa kwa ajili ya Injili; [3] Omba Roho Mtakatifu aingie rohoni mwako, akuzae upya, na aanze kazi Yake ya kukubadilisha kuwa mfano wa Kristo.

SALA: Baba, asante tena kwa siku mpya ya leo. Sisi ni wakosaji mbele Zako. Tunaomba msamaha kwa ajili ya dhambi zetu. Hebu Roho wako azungumze na kila mmoja wetu na kutuhimiza umuhimu wa Urithi wetu katika Kristo Yesu. Tunapoendelea kujifunza jinsi ulivyowapatia Israeli Urithi wao katika Nchi ya Ahadi, hebu likawe shauku la kila mmoja wetu kuingia katika ile Nchi ya Ahadi (Yohana 14:1-3) tunayoisubiria kwa hamu. Samehe makosa yetu na ututakase kwa ajili ya Ufalme wako. Tumeomba haya katika jina la Yesu Kristo, Mkombozi wetu, Amina.


 

AHADI YA LEO:
Dhima: Matokeo Kuzaliwa Upya

  • Kuingia katika ufalme wa Mungu: “Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu” (Yohana 3:5)
  • Utakatifu wa Maisha: “Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu.” (1 Yohana 3:9)
  • Upendo kwa Watu wengine: “Wapenzi, na mpendane; kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu, na kila apendaye amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu” (1 Yohana 4:7)

TUNAKARIBISHA:

  1. Nyimbo za Injili
  2. Ushuhuda
  3. Maombi (Sala)
  4. Kesha la Asubuhi
  5. Mahitaji (Changamoto za Kuombea).

Au, Jambo lolote la kiroho ambalo unaguswa kushirikisha watu wa Mungu. Bwana Awabariki.

 

Comments
Print Friendly, PDF & Email