Yoshua 16: Maswali na Majibu

August 4, 2022 in Mwongozo wa Biblia by TGVS

Mwongozo wa Kujifunza Biblia/ Yoshua 16, (6-BSG-16J)/ Katika ibara fupi, jibu maswali au andika mawazo makuu uliyojifunza kuhusu sura hii.


 

[1] Nini mada kuu katika Yoshua, sura ya 13 hadi 21? Urithi na Ugawaji wa Nchi ya Ahadi.

 • Yoshua 13: Nchi Iliyobaki; Ugawaji wa Mashariki ya Yordani
 • Yoshua 14: Kugawanywa kwa Nchi ya Magharibi
 • Yoshua 15: Urithi (mgao) wa Yuda
 • Yoshua 16: Urithi (mgao) wa Wana wa Yusufu
 • Yoshua 17: Kugawa kwa Nchi miongoni mwa Familia Zilizobaki za Kabila la Manase
 • Yoshua 18: Uchunguzi wa Nchi kwa Makabila Saba Yaliyosalia
 • Yoshua 19: Mgawanyo wa Mwisho wa Nchi
 • Yoshua 20: Miji ya Makimbilio
 • Yoshua 21: Miji Waliyopangiwa Walawi

[2] Sura hii inahusu nini hasa? Mgao wa kabila la Yusufu: Efraimu na Manase.

 • Yoshua 16 na 17 zinaweza kugawanywa katika sehemu sita — Mgao wa Yusufu: mpaka wa kusini (16:1–4); Mgao wa Efraimu Efraimu & mipaka yake (16:5-9); Maridhiano ya Efraimu: Kushindwa pale Gezeri (16:10); Mipaka ya Manase ya Magharibi (17:1–11); Kushindwa kwa Manase wa upande wa Magharibi kwenye miji yake (17:12–13); na malalamiko ya Yusufu (17:14–18)

[3] Urithi wa makabila (au “wana wa Yusufu”) uliamuliwa na nini? (16:1) Kwa kupiga kura (cf. Yos 14:2).

 • Kumbuka kwamba Yakobo awalipa Efraimu na Manase hadhi ya kabila (Mwanzo 48:5), inayoeleza kwa nini Yusufu anapewa migao miwili kupitia wanawe wawili.

[4] Wazao wa Yusufu walikuwa akina nani? (16:1) Walitokana na Yusufu, kupitia wanawe wawili waliozaliwa Misri – Manase na Efraimu.

 • “Basi kwa Yusufu wakazaliwa wana wawili kabla ya kuwadia ile miaka ya njaa, ambao Asenathi binti Potifera, kuhani wa Oni, alimzalia. Naye Yusufu akamwita mzaliwa wa kwanza Manase [asababishaye kusahau], akasema, Maana Mungu amenisahaulisha taabu na madhila yangu yote, na nyumba yote ya baba yangu. Na wa pili akamwita Efraimu [kuwa na fanaka], maana [alisema] Mungu amenifanya nifanikiwe katika nchi ya mateso yangu.” (Mwanzo 41:50–52, AMP)

[5] Ni sehemu gani ya nchi lililogawiwa kabila ya Yusufu? (16:1-3)

 • “Mgao wa wana wa Yusufu ilianzia Mto wa Yordani karibu na Yeriko, mashariki mwa chemchemi za Yeriko, kupitia nyikani na hata kukwea nchi ya Betheli yenye vilima. Kutoka huko Betheli (yaani, Luzu), kisha ikaendelea hata Atarothi kwenye eneo la Waarki. Kisha ikatelemkia upande wa magharibi hata eneo la Wayafleti, hata mpaka wa Beth-horoni ya chini, halafu kufikia Gezeri na hata kuvuka Bahari ya Mediterania.” (Yoshua 16:1–3, NLT)
 • Ilianzia Mto Yordani karibu na Yeriko. Iliendelea hadi kwenye maji ya Yeriko, kunako mashariki mwa mji huo. Mpaka ukapanda kutoka Yeriko hadi milima ya Betheli.
 • Kumbuka kwamba Yeriko ilikuwa katika mgao wa Benjamini (Yos 18:12), na Betheli pia ilipangwa kwa Benjamini (Yos 18:22).
 • Ingawa Yusufu alikuwa mmoja wa wana 12 wa Yakobo, hakuwa na kabila lililoitwa kwa jina lake kwa sababu, kama mwana mkubwa wa Raheli, mke wa Yakobo, alipokea sehemu maradufu ya urithi waliogawiwa wanawe wawili, Efraimu na Manase, ambao Yakobo aliwachukuliwa kuwa wake mwenyewe (Mwanzo 48:5). Haishangazi kwamba eneo kubwa zaidi na ushawishi mkubwa zaidi katika nusu ya kaskazini ya Israeli ulikuwa wa makabila yao.
 • Kumbuka: Wana wa Yusufu walikuja kuwa makabila makubwa katika ufalme wa Kaskazini wakati wa utawala wa kifalme uliogawanyika, kiasi kwamba jina Efraimu likawa moja ya majina ya ufalme huo (cf. Isa 7:2).
 • “Eneo walilogawiwa makabila haya mawili yenye nguvu [Efraimu na Manase] linajumuisha sehemu ya kati na, bora zaidi kwa kila namna, katika Kanaani magharibi mwa Yordani” ( C. Cook). Hili hushabihiana na baraka ya kishahabu ambayo Yusufu alipokea kutoka kwa Yakobo, baba yake, iliyorekodiwa katika Mwanzo 49:22, 25, 26.” – [John G. Butler, Analytical Bible Expositor: Joshua, Analytical Bible Expositor, (Clinton, IA: LBC Publications, 2010), 135].

[6] Je, “Bethel” na “Luz” ni nini? (16:2). Haya ni maeneo mawili tofauti — pengine Betheli mahali pa ibada, na Luzi mji. Jina la asili la ‘Betheli’ lilikuwa ‘Luzi’ (soma Mwa. 28:19; 35:6; Yos 18:13; Amu. 1:23).

 • “Betheli kihalisia humaanisha “nyumba ya Mungu,” na iliitwa hivyo kwa sababu Yakobo huko alipokea njozi ya kiungu iliyorekodiwa katika Mwa. 28. Kutokana na Mwa. 28:19, inaonekana kwamba eneo hili lilikuwa katika ujirani wa mji wa Luzi, lakini ilikuwa tofauti na mji wenyewe, ukiwa katika mashamba jirani, ambako Yakobo alilala usiku kucha. Miji hiyo miwili ikikaribiana sana kiasi hicho, pengine baadaye sehemu hizo mbili zilitazamwa kwa ujumla kama mji mmoja.” – (The Seventh-Day Adventist Bible Commentary, 2:258).

[7] Je, Atarothi ni nini na ilikuwa wapi? (16:3, 7)

 • Mahali kaskazini-mashariki mwa Efraimu, si mbali na Yeriko; huenda kwa sasa ni Tell Sheikh edh-Dhiab. Baadaye, Atarothi ikawa sehemu ya Benjamini (Yos. 16:5; 18:13).

[8] Vipi kuhusu ARKI? (16:3) Yaonekana huu ulikuwa ukoo. Wao, pia, baadaye walikuja kuwa sehemu ya Benjamini.

 • WAARKI: “Kabila lilitokana na Kanaani (Mwa. 10:17; 1 Nya. 1:15). Waliishi Arka, huko Foinike. Eneo la kisasa ni Tell ’Arka, lililoko karibu kilomita 19 (maili 12) kaskazini mwa Tripolis, nchini Siria.”— (Nelson’s New Ilslustrated Bible Dictionary)

[9] Jina “Beth-Horoni” linamaanisha nini? (16:3) Nyumba, au Hekalu la Horoni. “Horoni” alikuwa mungu wa Wakanaani aliyejulikana kutokana na maandishi kutoka Misri (el-Amarna), Ugarit, na Mari.

[10] Je, Wakanaani waliruhusiwa kuendelea kuishi katika mji upi? (16:10) Gezeri

 • Gezeri iliwekwa chini ya utawala wa Waisraeli pekee wakati farao wa Misri ambaye hakutajwa jina alipompa Sulemani kama mahari ya ndoa ya binti yake (soma 1 Wafalme 9:16)
 • Hii ni mara ya kwanza kutajwa kwa sera mbaya ya kukataa kuwaangamiza waabudu sanamu: “Lakini katika miji ya mataifa haya akupayo Bwana, Mungu wako, kuwa urithi, usikiachie hai chochote kipumuacho.” (Kumbukumbu 20:16, AMP)

[11] Hivi kosa la Efraimu lilikuwa nini kuhusu Gezeri? (16:10) — “Lakini hawakuwatowesha Wakanaani waliokuwa wakikaa Gezeri, hivyo watu wa Gezeri huishi kama watumwa miongoni mwa watu wa Efraimu hata hivi leo.” (Yoshua 16:10, NLT)

 • “Mwishoni mwa maelezo kuhusu mipaka ya Waefraimu, tunaambiwa kwamba wao pia, kama Wayuda, walishindwa kuwafukuza Wakanaani fulani kutoka katika maeneo yao (kuhusu Yuda, tazama 15:63); katika suala hili, wakazi wa Gezeri (angalia pia Amu. 1:29). Hapo awali Yoshua alikuwa ameiteka Gezeri kwa kiasi fulani (Yos 10:33), lakini ni wazi haukuwa ushindi kamili, ama sivyo ulikuwa umeongezeka wakati katika kipindi cha mpito. Gezeri ilibaki nje ya utawala wa Waisraeli hadi wakati wa Sulemani, wakati Farao wa Misri alipouteka na kukabidhi kama mahari kwa binti yake, biarusi wa Sulemani (1 Flm. 9:16).” — [David M. Howard Jr., Joshua, The New American Commentary, (Nashville: Broadman & Holman Publishers, 1998), 5:348].

[12] Jinsi gani Wakanaani waliwatumikia Waefraimu? (16:10) Walikuwa watumwa. — “Hata hivyo, watu wa Gezeri wanaishi kama watumwa miongoni mwa watu wa Efraimu hata leo.” (Yoshua 16:10b, NLT)

 • Waisraeli waliruhusiwa kuwafanya watumwa wakazi wa miji nje ya nchi ya ahadi kuwa watumwa, lakini walipaswa kuwaangamiza wale waliokuwa wakiishi katika nchi hiyo (Kumb. 20:10–16). Kutokana na somo letu la awali, bila shaka utakumbuka kwamba hii ndiyo ilikuwa hatima ya Wagibeoni (Yos 9:21).

 

Comments
Print Friendly, PDF & Email