Kuzinduliwa kwa Agano Jipya.

April 6, 2019 in Injili Ya Asubuhi by TGVS

Injili Ya Asubuhi.

 

“MSALABA WA YESU KRISTO.”
“Maana naliazimu nisijue neno lo lote kwenu ila Yesu Kristo, naye amesulibiwa”

[Somo la 6/50]
Kuzinduliwa kwa Agano Jipya.
83Z-006: Neno Kuu: eucharisteō (Eucharist)

AYA KUU YA LEO:
“26 Nao walipokuwa wakila Yesu alitwaa mkate, akabariki, akaumega, akawapa wanafunzi wake, akasema, Twaeni, mle; huu ndio mwili wangu 27 Akakitwaa kikombe, akashukuru, akawapa, akisema, Nyweni nyote katika hiki; 28 kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi. 29 Lakini nawaambieni, Sitakunywa kabisa tangu sasa uzao huu wa mzabibu, hata siku ile nitakapokunywa mpya pamoja nanyi katika ufalme wa Baba yangu.” (Mathayo 26:26-29)

Mawazo Makuu:
Vipengele vya Agano Jipya:
(a) Agizo: “Twaeni, mle.”
(b) Fundisho: “Huu ndio mwili Wangu.”
(c) Fundisho: “Hii ndiyo damu Yangu.”
(d) Fundisho: Kwa “ondoleo la dhambi.”
(e) Kipindi cha Agano: “Hata siku ile.”
(f) Tufanye nini basi na Somo hili?
(g) Sauti ya Injili – (Sauti ya Bwana kwa ajili yako)

SAUTI YA INJILI.
[Kafara ya Kristo inatupatia ujasiri wa kutazamia Marejeo Yake]

“Kadhalika Kristo naye, akiisha kutolewa sadaka mara moja azichukue dhambi za watu wengi; atatokea mara ya pili, pasipo dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa wokovu.” (Waebrania 9:28)


 

BWANA ATUBARIKI SOTE!
Bofya hapo juu ili kusikia Injili ya Asubuhi ya Leo.

Comments