Onyo dhidi ya Kujiamini.
April 7, 2019 in Injili Ya Asubuhi by TGVS
Injili Ya Asubuhi.
“MSALABA WA YESU KRISTO.”
“Maana naliazimu nisijue neno lo lote kwenu ila Yesu Kristo, naye amesulibiwa”
[Somo la 7/50] 83Z-007.
Onyo dhidi ya Kujiamini.
Neno Kuu: Skandalizō (fall away)
AYA KUU YA LEO:
“30 Nao walipokwisha kuimba, wakatoka nje kwenda mlima wa Mizeituni. 31 Ndipo Yesu akawaambia, Ninyi nyote mtachukizwa kwa ajili yangu usiku huu kwa kuwa imeandikwa, ‘Nitampiga mchungaji, na kondoo wa kundi watatawanyika.’ 32 Lakini baada ya kufufuka kwangu, nitawatangulia kwenda Galilaya.”
“33 Petro akajibu, akamwambia, Wajapochukizwa wote kwa ajili yako, mimi sitachukizwa kamwe. 34 Yesu akamwambia, Amin, nakuambia wewe, usiku huu kabla ya kuwika jogoo, utanikana mara tatu. 35 Petro akamwambia, Ijaponipasa kufa nawe, sitakukana kamwe. Na wanafunzi wote wakasema vivyo hivyo.” (Mathayo 26:30-35)
MAWAZO MAKUU:
(a) Utangulizi/ Marudio.
(b) Upeo wa Yesu wa Kujua kila Kitu.
(c) Unabii wa Zakaria.
(d) Uhakikisho wa Mwokozi.
(e) Upumbavu wa Wanafunzi.
(f) Raghba ya kupindukia ya Petro.
(g) Tufanye nini basi na Somo hili?
(h) Sauti ya Injili – (Sauti ya Bwana kwa ajili yako)
SAUTI YA INJILI.
[Ahadi ya Urejeshwaji: Kanisa la Laodikia.]
“17 Kwa kuwa wasema, mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi. 18 Nakupa shauri, ununue Kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona. 19 Wote niwapendao Mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu. 20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti Yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, Nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja Nami.” (Ufunuo 3:17-20)
BWANA ATUBARIKI SOTE!
Bofya hapo juu ili kusikia Injili ya Asubuhi ya Leo.